Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Nakukubali sana bro, my intentions were pure.

Sijawahi kuwa na wasiwasi na intentions zako, ila kunishtukiza hivyo siyo powa. Maana ningeweza kutoa boko ikawa so, nikaanza kujitetea ooh, sikujua kama ni wewe.

Baada ya Paula Paul kuanza kuwa active, niliona kabisa pengo lako wewe na yule dada alikuwa so deep kwenye International Forum.
 
Ushawahi kumsikia Abu Yusuf Al-Kindi wa Baghdad ??? Alikuwa ni msomi mkubwa aliyasaidia kuimarisha

Huyu simfahamu, ukinipa habari zake itakuwa nzuri zaidi.

Mimi nawafahamu akina Fakhru Diin Raazi, Abul Hamiid al Ghazal, Abu Maal al Juwainiy, al Amiid ila hao wote katika masiku yao ya mwisho wa uhai wao walijutia kupoteza muda wao mwingi katika kujifunza Logic (Ilm al Kalam) na Falasifa (Philosophy).
Yeye alisoma vyote hivi na mpaka leo hii anasifikia kwa mchango wake mkubwa kwenye taaluma ya ujasusi hasa kwa kuanzisha vitu kama Cryptography, Coding and Code Breaking na Ciphers.
Vipi kuhusu itikadi yake ? Je ilisalimika ? Kwa maana alikuwa anaamini nini kuhusu uwepo wa Mola ? Kuhusu chanzo cha uhai ? Kuhusu sifa za Mola muumba ?
Kiujumla alisomea Falsafa ya Kiislamu na Falsafa ya Kigiriki hasahasa Aristotelianism. Huyu unamuweka kwenye kundi gani ?

Kwangu mimi kaka, siamini kama kuna Falsafa ya Kiislamu, sababu asili ya hao wanao itwa Wanafalsafa wa Kiislamu walitoa misingi yao kwa Aristosto na wao waliitoa kwa Sabeans, na wale Wakristo wa Damascus matokeo yao zilifisidika itikadi zao.

Unapo sema Falsafa ya Kiislamu ina tofauti gani na Falsafa ya Kimagharibi ?
 
Bro wewe ni mstaarabu sana ndiyo maana mpaka sasa hujashusha boko lolote lile.
 

Falsafa ya Kiislamu ni ile ambayo msingi wake uko kwenye kitabu cha Quran lakini inajikita sana katika kupitia shule mbalimbali za kiislamu mfano kwenye sheria mtu akisomea sheria za Kiislamu (Muslim Jurisprudence) basi tunasema amesoma sehemu ndogo ya Falsafa ya Kiislamu.

Pia nikuhakikishie kwamba Al-Kindi alisalimika sana (He was a devout muslim) na ndiye alikuwa moja ya vinara wakubwa waliolisaidia Dola la Kiislamu kuwa na nguvu ambazo lilikuwa nalo hasa kwenye taaluma ya kijeshi.

Falsafa ya Magharibi hapa naongelea ile ya Greco-Romano Philosophy (Classical Greece, Hellenic Greek and Ancient Rome) japo leo hii imekuwa pana zaidi.

Ukipata muda mtafute Al-Kindi na umsome utajifunza mengi sana. Nikipata wasaa ntaviweka vitabu vinavyoongelea mchango wake kwenye taaluma ya Ujasusi, Hesabu na Jeshi.
 
I do remember Don.
Ila wewe unasema kwamba watu (pamoja na wewe,) mnaacha akili zenu nje mnaingia huku na akili ya kusoma tuu.
 
Pia nikuhakikishie kwamba Al-Kindi alisalimika sana (He was a devout muslim) na ndiye alikuwa moja ya vinara wakubwa waliolisaidia Dola la Kiislamu kuwa na nguvu ambazo lilikuwa nalo hasa kwenye taaluma ya kijeshi.

Nilikuuliza kujua kasalimika au la, ni kuangalia itikadi yake juu ya chanzo cha ulimwengu, anasemaje kuhusu sifa za Mola na mfano wa hayo.

Ngoja nikupe mfano, kuna mtu alikuwa anaitwa Ja'ad bin Dirham, huyu aliathiriwa na Falsafa za waabudu nyota na masanamu katika kuelezea chanzo cha maumbile "Origin of bodies" (Huduuth al ajsam) huyu katika hilo hakupita katika mapito ya kiislamu bali mapito ya Sabean yaani Wapagani. Hii ikampelekea kukanusha sifa za Mola wetu mlezi.

Hapa bila shaka una maanisha madhehebu ya kifiqhi, kama sijakuelewa uzuri utaniweka sawa.

Unaweza kutuwekea aya kutoka katika Qur'aan ukaonyesha msingi wa Falsafa ya Kiislamu ulipo ?

Unajua kama kuna tofauti kati ya "Fiqh" , "Usul al Fiqh" na "Qawaid al Fiqhiyyah" ? Hizi zote zinaelezea Sheria za Kiislamu.
Falsafa ya Magharibi hapa naongelea ile ya Greco-Romano Philosophy (Classical Greece, Hellenic Greek and Ancient Rome) japo leo hii imekuwa pana zaidi.
Ndio maana huwa najiuliza pale unapo sema kuna Falsafa Kiislamu, ilhali hao Wanafalsafa waitwao wa Kiislamu wachukua misingi toka kwa Wagiriki, rejea zile "Ten Categories" (Maqulast al Ashar) za Aristoto na wao ndio wanapita humo humo.
Ukipata muda mtafute Al-Kindi na umsome utajifunza mengi sana. Nikipata wasaa ntaviweka vitabu vinavyoongelea mchango wake kwenye taaluma ya Ujasusi, Hesabu na Jeshi.
Leo nitamchimba huyu mtu ili nipate kumjua uzuri.

Lakini kitu kimoja unachotakiwa ukijue ni kuwa salama ya mtu sio katika ushujaa wake au elimu yake salama ya mtu nikusalimika kwa itikadi yake.
 
kwanini Waislamu wengi wa kizazi hiki wanakuwa wanapinga sana elimu za Magharibi hasa zile za Ugiriki ya kale wakati waislamu wengi wa kipindi hicho walizisoma sana ??

Wanazipinga sababu ziliwapelekea kuharibika kwa itikadi zao na itikadi ndio hujulisha hatima ya mtu.

Ukisoma kitabu kama "Swawn al Mantiq" cha Imaam Suyuti ameelezea hayo kwa jinsi walivyo juta kwa kupoteza muda na ukisoma kitabu cha al Imaam Harawi kitwacho "Dham al Kalaam wa ahlihi".

Nikipata wasaa nitakupa mifano na shuhuda zao.
 
I do remember Don.
Ila wewe unasema kwamba watu (pamoja na wewe,) mnaacha akili zenu nje mnaingia huku na akili ya kusoma tuu.

Kuna kipindi humu huwa panaboa kwa sababu watu hawataki arguments za kutumia akili, hivyo unajikuta kila ukiingia unakutana na topics famba.

Kuna muda mtu anaandika kitu unashangaa sana inakuwaje mtu anakuwa na mawazo mabovu hivi, ukisema umrekebishe anaona kama umemu-offend. Kwa hiyo ili kuendana na character hizo inabidi ufate muziki huo huo. Ndiyo mantiki ya kuacha akili nje.

Halafu humu kuna muda mtu anakurupuka hajaelewa kilichoandikwa anakuponda kwa sababu zake binafsi, sasa unaweza kupanic ukajibu mtu vibaya ikawa umeanzisha mengine.
 
Hahaha. Hii ni spinoff ya Love in the time of Cholera.
Nilimsoma Gabriel Marquez na kitabu chake cha death foretold. He is a great story teller.


Sent using Jamii Forums mobile app

He is.

Nimesoma One Hundred Years of Solitude.

Ni kama vile msomaji unaishi katika hivyo vijiji vya Latin America enzi hizo za wababe wa kivita, bandidos na passionate love between men and women.
 
Hello guys,

I just finished reading Frankl's 'Man's Search For Meaning' yesterday. OMG what an amazing read it was!
The book was interesting and could hardly put it down. That was an amazing read and it really changed my outlook on life.

Life means to take responsibility, to find the right answer to its problems and to fulfill its tasks.
Frankl indentify 3 categories of things which giving meaning to our lives and inspire us to to continue through hardship.

1.Working towards your goals.
2. Enduring one sufferings.
3. Caring for another person.

So the meaning in life can be found in those three things.

Dostoevski said once, "There is only one thing I dread: not to be worthy of my sufferings." Sufferings is an inherent and integral part of life and we need to find meaning in it. We should stop saying "Why me". We should walk through it with dignity.
You see, let's embrace suffering BUT it only bearable when there is meaning attached to it. Don't suffer for the sake of suffering that will be masochistic rather than heroic.

Each man's life is unique and as such the meaning of life is inevitably different for each individual person.

Here are some quotes which I liked ,
" So live as if you were living already for the second time and as if you had acted the first time as wrongly as you are about to act now!"
" Those who have a 'why' to live, can bear with almost any 'how'""

" In some ways suffering ceases to be suffering at the moment it finds a meaning, such as the meaning of a sacrifice."

" I do not forget any good deed done to me & I do not carry a grudge for a bad one."

" To draw an analogy: a man's suffering is similar to the behavior of a gas. If a certain quantity of gas is pumped into an empty chamber, it will fill the chamber completely and evenly, no matter how big the chamber. Thus suffering completely fills the human soul and conscious mind, no matter whether the suffering is great or little. Therefore the "size" of human suffering is absolutely relative."

" when someone loves another person, he or she can see the potential of that person and the meaning the person ought to strive to find. By loving someone, one has the opportunity to help that person find his or her purpose in life."

WOW, I cannot recommend it enough for those who haven't read it. I would say this is one of the must read book for everyone.

And BTW "...Everything can be taken from a man but one thing; the last of the human freedoms—to choose one's attitude in any given set of circumstances, to choose one's own way." -- Viktor Frankl, Man's Search For Meaning
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…