Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

No sio mvivu wa kuongea basi tu sina wongi wa maneno hata hayo machache siwezi kuyawasilisha mbele za watu. Sasa nashangaa huyu ndugu yy maneno anatoa wapi
hahaaa huyo ndiye Zurri
kipaji chake akitumie kuandaa nakala
 
Kajaliwa sana..mwalimu itakua alipata tabu kusahisha ese zake

Ilikuwa kazi ngumu sana kuandika "essay" haya ya kuandika sana nimeyakuta ukubwani, ila udogoni nilikuwa siwezi kuandika maneno mengi.

Pili, huwa naandika sana kulingana na jambo husika, na huwa nafanya hivyo ili kufunga mianya ya kuulizwa maswali yasiyo na msingi, yaani huwa najitahidi kujibu maswali ya kitoto humo humo katika ninacho kiandika.

Ahsante.
 
Yupo vyema sana
sijui hizo References huwa anaziwekaje Kichwani!
Binafsi uwezo wa kutunza vitu kama vilivyo siwezi kabisa,
Nampa Kongole Mkuu Zurri

Vitabu pekee ambavyo nimejikuta nakuwa na references kichwani ni vile nakuwa navirudia rudia.

Mfano vitabu vya Mario Puzo, hivyo navikumbuka vingi sana, ila kwa marudio. Ila huyu mjamaa namsomaga namwacha alivyo.
 
umenifanya nicheke
huwa nasoma Vitabu Ila Mara nyingi ukiniuliza author ama Tittle sikumbuki
ninakumbuka tu contents.
 
Vitabu pekee ambavyo nimejikuta nakuwa na references kichwani ni vile nakuwa navirudia rudia.

Mfano vitabu vya Mario Puzo, hivyo navikumbuka vingi sana, ila kwa marudio. Ila huyu mjamaa namsomaga namwacha alivyo.

Tangu nafundishwa niko mdogo, niliambiwa haya yafuatayo kuhusu vitabu na usomaji wake.

1. Adabu za kusoma vitabu na kutunza vitabu.
2. Kabla hujasoma kitabu yaani kujua nini kimeandikwa ndani, lazima ujue yafuatayo kuhusu kitabu :

a. Jina la kitabu
b. Muandishi wa kitabu
c. Kuna chapa ngapi mpaka kufikia hicho kitabu ulicho nacho na kimechapishwa na kampuni gani ?
d. Kitabu bora ni kile ambacho kipo katika "Hard Copy" hivi vya "Soft Copy" kwa ajili ya dharura.

Kwahiyo ukiishi katika somo la "Adabu la usomaji wa vitabu" suala la kuhifadhi majina na mambo muhimu ya juu ya vitabu ni rahisi sana, wala sio jambo la ajabu.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom