Unajua nchi hizi za wenzetu unaweza ukajua karibia kila kitu kuhusu kwao kwa kutumia mtandao tuu, na zina ripotiwa na sources tofauti tofauti ukisoma source hii ukienda hii ukienda hii, ukiona taarifa zimefanana unaweka tiki "hiyo ni uhakika".
Tofauti na Tz, taarifa nyingi hazipo mtandaoni nikimaanisha nje ya Instagram na Twitter. Yaani ukiwa nje ya Tz kupata mambo yanayoendelea TZ labda utumie Instagram na Twitter. Cha ajabu hata ukisema ufuatilie Mbuga au vivutio vya utalii haupati taarifa za kutosha. Na ndio maana leo Mtz anakuelezea Caribbean vizuri kama vile amewahi kufika lakini sio Zanzibar, sio serengeti , sio ngorongoro.