Paula Paul
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,649
- 13,607
- Thread starter
- #2,541
Thank you very much for this reply Nowonmai. Umeandika vizuri.Samahani kwa kukawia Paula na Pendael24.
Kwenye edition ya kwanza(1952), mwandishi alitoa utangulizi ambao nadhani twaweza sema ndiyo malengo yake kwa huu utunzi.
View attachment 1754047
Kama tunavyoona hapo, moja ya dhana alizotaka kuwasilisha mwandishi ni wema na uovu.
Dhana ya wema na uovu ni ya zamani zaidi kuliko dini tunazo practice wakati huu na hivyo kwa maoni yangu East of Eden hakina udini ndani yake licha ya kuwa na maudhui kadhaa ya kibiblia.
Angalia namna mwandishi anavyotumia irony kufikisha ujumbe:-
Lee na wasomi wa kichina wanaibua suluhisho linalokubalika toka biblia ya kiibrania.
Cathy/Kate hatimaye anampenda sana mmoja wa watoto wake aliowatelekeza wakiwa wachanga na kumwachia urithi wa mali ingawa hakubadilika kabisa katika aspects zake nyingine za uovu.
Charles pia anabadilika ukubwani na kuweza kuishi kwa amani na Adam baada ya kuwa na chuki kali sana dhidi ya huyu ndugu yake.
Angalia pia jinsi familia ya Samuel Hamilton ilivyojaa contradictions.
Kwangu mimi basi hiki kitabu kina maudhui mengi lakini sio hilo la udini au kama lipo sio la muhimu sana.
BTW Kuna mahali mwandishi analinganisha ujio wa waeneza dini na makahaba mjini na ni kama vile wote wana ushawishi sawa au pengine ushawishi wa makahaba una uzito kuliko ule wa wainjilisti!
Don’t know why I feel so much at loss after writing this.
Paula and others please let me have your views.
Mimi kikubwa nimeona ni the struggle between good and evil na tupo na maamuzi ya kuchagua ni yapi tufanye juu ya maisha yetu na yapi tusifanye huo uwezo tunao bila shaka ndio maana ya Timshel. So it's our choice whether to embrace goodness or evil.
Japo natamani angeendelea kuandika zaidi tuone maisha ya Cal na watoto wake kama history iliendelea kujirudia.