Black Panther X
JF-Expert Member
- Sep 4, 2014
- 230
- 659
Lessons nyingi na uzuri kina mifano ya biashara aina mbalimbali hivyo unajifunza kwa kuangalia lessons in action.tupe summary ya madini mawili matatu uliyookota kutoka kwenye kitabu icho.
So big lessons ni
- Huitaji ofisi wala big presence ili kuanza biashara bali inabidi utafute tatizo unaloweza kutatua kwa watu wengi na WATU WAKUAMINI kuwa unaweza kulitatua
- Kama huna mtaji kabisa anza biashara ya huduma ambayo inahitaji skill zako au ujuzi wako ili ukusanye capital. Mfano ufundi ama accountancy ana ususi na kadhalika
- Kipato chako kinavyoongezeka punguza kazi ambazo za kujirudia au usizopenda. Mfano kuosha vifaa vyako vya kazi ama kupokea wateja. Hii itakuwezesha kukua kwa kasi zaidi kwa kuwa una muda zaidi
- Tambua soko lako vizuri. Ingia kwa undani umchambue mteja wako. Ni jinsia gani, anafanya kazi gani, ana umri gani na kadhalika. Ukimtambua vizuri unaweza kuandika maneno ya kumuuzia. (Hii ndio the biggest thing nimeona impact yake. Mfano tu jana na leo nimeingiza 100,000 kwa message ambazo niliandika 3 years ago baada ya kumchambua mteja)
- Jifunze kuuza. Ndio skill moja ambayo itahakikisha haulali njaa. Kuna mbinu nyingi zinaongelewa vema usome kitabu.