SMART GHOST
JF-Expert Member
- Feb 3, 2020
- 2,657
- 10,356
CONFESSIONS OF AN ECONOMIC HITMAN, kimeandikwa na jamaa wa kuitwa John Perkins.Tuelezee kidogo, SMART GHOST.
Huyu jamaa alikua recruited na wanausalama wa marekani NSA, kisha akapewa kitengo kama chief economist at the Major International Consulting firm (MAIN).
Anaelezea kazi yao economic hitmen, ilikua ni kuchunguza nchi zenye rasilimali muhimu kama mafuta na madini, kisha wanazishawishi zichukue mikopo mikubwa kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo kiuhalisia haikua na manufaa nchi husika (white elephant projects).
Hii miradi ilikua inanufaisha makampuni ya kimarekani ambayo ndiyo yaliyohusika katika utekelezaji wake. Baada ya nchi husika kushindwa kulipa madeni, basi tayari inakua imeingia kwenye mfumo wao wa "economic colony"
Hapo wangeweza kurudi na kutaka miradi mingine ili kufidia, au nchi hiyo kutumika kama asset kwenye masuala ya kiuchumi na kiusalama kwa maslahi ya marekani.
Walikua wanashawishiwa vipi kuchukua mikopo wasioweza kuilipa? Nini kilitokea endapo wangegomea hiyo mikopo? Nini kilitokea endapo nchi hizo zingeenda kinyume na maslahi ya Marekani? Yote hayo ameelezea kwa mifano mizuri aliyohusika mwenyewe
Kuanzia mgogoro wa Panama canal, deals za kuchimba mafuta kwenye maeneo ya msitu wa Amazon, mpaka deals za mafuta na ujenzi wa Saudi Arabia.
Ukisoma hiki kitabu, utaelewa vizuri project ya bandari ya Bagamoyo. Baadae nikitulia nitaweka PDF file yake hapa!
Adios