Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mfanyabiashara Mohamed Dewji ameripotiwa kutoa shinikizo la kujiuzulu nafasi zao kwa wajumbe wote aliowateua yeye ambapo mpaka sasa wajumbe watatu wamejiuzuli huku wengine watatu wakigoma.
Wajumbe waliogoma kutii amri ya tajiri mpaka sasa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Salim Abdallah Muhene 'Tryagain', Rashid Shangazi ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo na Hamza JOHARI ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mamlaka za viwanja vya ndege Tanzania.
#KitengeSports