Bora kuwa huru ukiendesha bodaboda Tanzania kuliko kuwa mfagia vyoo wa Canada

Utanishtua tuingie wote Toronto
 
Kwa kifupi huna akili
 
Hakuna mtu anafanya kazi ya bodaboda Kwa mapenzi yake

Wengi wao ni hakuna kitu kingine cha kufanya
Hiyo nikazi ambayo umekosa mbadala.
Kazi hiyo sio yakujivunia hata kidogo tuache kupotosha
 
Ww Hebu tuache, kuna viongoz wakubwa wa siasa walikimbilia huko Canada kubeba mabox, Ww Nani usifanye kazi Hiyo
 
Wenyewe wasema "heri kuwa mbwa ulaya kuliko kuwa mwana wa Inchi!!"
 
Siungi mkono hoja ya mtoa mada ila hayo ya Lema kukunua usafiri wa Anga, nayo ni mapya?
Hivi unajua bei ya ndege? au labda una ongelea Mabasi ya kwenda Dar?
Hiyo hela uliyotaja inaweza kuleta Yutong 5 au Scania Marcopolo 3
Una kichaa wewe, hawezi kukodi lazima anunue cash?
 
Siungi mkono hoja ya mtoa mada ila hayo ya Lema kukunua usafiri wa Anga, nayo ni mapya?
Hivi unajua bei ya ndege? au labda una ongelea Mabasi ya kwenda Dar?
Hiyo hela uliyotaja inaweza kuleta Yutong 5 au Scania Marcopolo 3
Au pengine alimaanisha 3B USD (ambayo si rahisi hata hivyo ukizingatia kina Mo Dewji tu wana Net worth za 1.5bn USD na ndiyo tajiri no 12 Africa) Lakini kama ni hii pesa yetu,nakubaliana na wewe mambo siyo rahisi kihivyo kwa huo mtaji kuwekeza kwenye biashara ya usafiri wa anga.
 
Mkuu hata kama umekerwa na Lema ila this is too much. Mfagia vyoo Canada ana hela kuliko Graduate aliyeajiriwa na Halmashauri TZ. Nakumbuka kuna jamaa mhindi alikuwa houseboy Qatar mshahara wake ulikuwa USD 3500 kwa mwezi. Mponde Lema kwa facts.
 
kazi ni kazi tu alimradi uchumi unasonga mbele. Wanaofanya hizo kazi iwe hapa au nje ya nchi inafaa tuwaheshimu sana kwani wanatoa huduma muhimu kwa jamii.
 
Kila mtu aheshimu kazi ya mwenzake ili mradi ni kazi halali, Bodaboda zenyewe zinasaidia sana kwenye usafiri.
 
Lema kazi anayo aiseee ina onekana katoa boko kweli kweli
 
Sasa sote tukiwa wanasiasa nani atakuwa bodaboda? Nani atakuwa mwalimu? Nani atakuwa nurse? Nani atakuwa mwanasheria? N.k. Ifike sehemu tuheshimu kazi ya kila mmoja. Tunategemeana.
HAKIKA
 
Lema amechemsha sana
 
Yaan wewe unajiona uko huru na huna hela. Bro acha utani tafuta hela uwe huru mzee. Huwez kuwa huru ukiwa mchovu hata kwako utapaona jehanam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…