SEHEMU YA 9
Siku hiyo rafiki yangu hakurudi lakini nilizidi kumtumia ujumbe wa kumuelewesha na kumuomba msamaha.
Nilichungulia akiba yangu nikaona bado haijafika 1M ili niweze kwenda kuwasalimia wazazi wangu.
Hiki kitu kilininyima amani, nikahisi shauku ya kumtafuta Emmy ili kama ana laki 4 anipatie niongezee nikaone wazazi.
Sikua na shaka juu ya Emmy sababu alikua rafiki yangu tuliyependana pia ana moyo mzuri.
Nilipiga simu yake haikupokelewa nikamtumia ujumbe MAMBO EMMY! UKIPATA NAFASI NAOMBA UNIPIGIE NINA MATATIZO.
Baada ya muda mchache akanipigia simu, nikapokea
EMMY: Una tatizo gani Tina? Umenishtua.
TINA: Maisha hayako sawa kwa upande wangu, nimejikuta napoteza kula kitu.
EMMY: Naomba usilie! Niambie wapi nije tuongee.
TINA: Njoo Tabata Barakuda, ukifika niambie ili nimtume boda akulete kwangu.
EMMY: Kwako? Kwani hukai tena na baba?
TINA: Ni mwaka sasa sipo nae.
EMMY: Mmmh! Sawa nakuja.
Mida ya mchana Emmy aliniambia ameshafika ila akasema niende tuongelee kwenye restaurant iliyopo hapo barabarani, sijui kwanini alikataa kuja ndani kwangu.
Nilipomuona rafiki yangu kwa mbali tu nikianza kulia. Emmy amenawiri huhitaji kujiuliza kuhusu maisha take anaonekana tu kila kitu kwake kipo Sawa.
"Mbona unalia Sawa, njoo tukae uniambie" Emmy alisema
Nilimueleza Emmy kila kitu
EMMY: Kumbe hadi chuo umefeli?
TINA: Ndio
EMMY: Ungeniambia tokea mwanzo kabla hujaanza mahusiano na baba yangu hakika ningekukataza kivyovyote vile. Sasa cheki umeathirika na hujapata faida yoyote.
Nikaanza kulia Emmy ananibembeleza
EMMY: Kwanini usirudi nyumbani kwenu ukaanze upya kuliko kuendelea kujiuza hapa Dar.
TINA: Ndio maana nimekuita! Naona aibu kurudi kuwatizama wazazi wangu ila nilitaka japo nikawasalimie halafu nirudi Dar kupambana. Ila hela haitoshi nimepungukiwa laki 4 nataka nirudi hats na zawadi kwa ajili yao kama nilivyokuambia wanajua ninafanya kazi kurudi mikono mitupu itawapa wasiwasi.
EMMY: Nipe wiki moja tu nitakupa hiyo pesa lakini naona urudi kwenu moja kwa moja ukakae huko mpaka akili yako ikitulia pia upone maumivu yako.
Nenda nyumbani uwaambie kila kitu wazazi, naamini hawatokutupa kwa sababu wewe ni binti yao.
TINA: Mmmh! Yaani niwaambie kua nimeathirika?
EMMY: Sio lazima kuwaambia kuhusu ugonjwa kama haupo tayari ila ni vyema uwaambie kua chuo ulifeli hip itakueka huru kwenye hatua yako ya kupona haraka.
Nenda kwenu Tina ukajipange kujikwaa sio kuanguka.
TINA: Naogopa Emmy natamani bats nife.
EMMY: Naelewa wakati unaoupitia najisikia vibaya kuona unateseka sababu ya baba yangu. Lakini nakulaumu kunificha tokea mwanzo.
TINA: Kwani ulijuaje baba yako ameathirika?
EMMY: Kuna likizo nilikua kwake, akaja binti mdogo tu akawa analia anamlalamikia hapo ndipo nilipojua.
Nakuomba ujisamehe Tina kwa yote uliyojisababishia ili uweze kufungua milango yako ya baraka. Hili lishatokea usizidi kujihukumu.
Nikaagana na Emmy kila mtu akaondoka, nilihisi faraja na maneno yake yaliniingia nikakubali niondoke Dar nikajipange upya kwetu.
Nilimkuta rafiki yangu amesharudi, tukaongea tukayamaliza pia hasira zake zilikua zishaisha na kabla wiki haijaisha Emmy alinitafuta tukaenda kariakoo.
Emmy alininunulia zawadi za mama, baba na wadogo zangu pia akanipatia laki 5.
Nilimshukuru sana, nikamuomba twende kwangu ili nimuachie vitu nilivyochukua kwa baba yake sababu sivihitaji tena Mimi nimeamua kusamehe yote lakini Emmy alikataa.
.................................
TINA: Hallow! Shikamoo
BABA EMMY: Marhaba! Umenipigia una jambo gani?
TINA: Naomba unisamehe popote pale nilipokukosea katika kipindi cha kujuana kwetu na Mimi nimesamehe yote ambayo naona ulinikosea.
Nakutakia mafanikio mema.
BABA EMMY: Mbona kama unanipa laana sasa?
TINA: Hapana usifikirie hivyo! Naona msamaha utaniweka huru ni hilo tu.
BABA EMMY: Kwani wewe upo wapi? Au unaumwa unakaribia kufa sababu ghafla sana kunipigia na kuanza kuombana msamaha.
TINA: Mimi nipo sehemu naendelea na maisha yangu na wala siumwi.
Pia naomba nirudishe vitu nilivyochukua kwako nilivichukua kimakosa.
BABA EMMY: Kuhusu vitu wewe baki navyo, nishanunua vingine.
TINA: Sawa kwaheri.
Vitu nikamuachia rafiki yangu niliyekutana nae bar.
Mimi Tina nina tiketi yangu mkononi, kesho nitaanza safari ya kurudi kwetu kwa wazazi wangu, japo naogopa sana macho ya mama yangu ila sina budi kwenda kukabiliana nayo na kuanza maisha yangu upya.
~MWISHO~