Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Umenikumbusha mbali sana.....

Splash to

Bounce to

Bend down to

Drop to

Barua za songea galz na machame huku zikinitaja mwanafunzi wa PCB..... Hazikukauka! Mpk nahitimu

Kingine

I need your reply asap
Acha tu jumatatu hiyo mchana pale paredi ya boyz yule jamaa wa social alikuaga na sauti kubwa anawaita Moja Moja utaskia from Ashira....😂 form v akipokea wanasema kajiandikia
 
Dah umeme..... Buza nako, hapo sioni kids au alikuwa anatumia uzazi wa mpango hope kama she's alive basi kapitia mengi
Kuhusu watoto sijataka kuizungumzia ila hana uwezo wa kupata mtoto aliniambia kizazi chake sijui kina shida gani sikumfatilia sana upande huo.
 
Kuhusu watoto sijataka kuizungumzia ila hana uwezo wa kupata mtoto aliniambia kizazi chake sijui kina shida gani sikumfatilia sana upande huo.
siwezi judge anything hapo kwa ujumla

Japo wengi watasema njaa na nn !

Lkn alikosa malezi ya mama hasa nadhani umesema alikuwa mtukutu flani ...... wapo wazazi mtoto akiwa against na wengine basi inakuwa advantage ya kumwona kama sio....

She needs a deepest hugs, for her difficulties....... happened to her life... Though she's strong enough aseeh...

Hugs to your friends.....
 
Acha tu jumatatu hiyo mchana pale paredi ya boyz yule jamaa wa social alikuaga na sauti kubwa anawaita Moja Moja utaskia from Ashira....😂 form v akipokea wanasema kajiandikia
Kabisa kabisa Ila Raha sana japo simu tulikuwa nazo lkn ujumbe wa barua still ulkuwa una raha yake
 
Bora wewe hata unaelewa
 
Bora wewe hata unaelewa
hata mimi nina yangu nikiyasema hapa ni huzuni kweli kweli...... though najipa moyo everything will be okay.....

so nikiona story km hiii au mtu anachopitia siwezi cheka, zaidi ni kumwonea huruma kwa anayopitia muda huo!

watu wengi wanahitaji hata kukumbatiwa, ama kuambiwa hongera unaweza..... lakini hakuna wa kumwambia awe mzazi, mke, mume, mchumba na jamii ndo usiseme kabisa! Tunahitaji kufarijiana.....

na kuchukuliana kama familia....
 
Daah inahuzunisha sana
 
SEHEMU YA 7
Nilitegemea baada ya kumpatia alichotaka basi mzee wangu angetulia lakini ilikua tofauti. Furaha ndani haikudumu kwa muda mrefu hata mwaka haukupita matatizo yakaanza upya.

Weekend moja alfajiri Mzee aliniaga anaenda kazini, "kazini weekend" nilijihoji ila ningefanyaje sasa.

Muda wa mchana nikaona namba mpya imenitumia picha WhatsApp ikisindikizwa na ujumbe "bwana ninaye"

Hivi vidole navijua! hili shati nalijua ni la mzee wangu na ndilo ameondoka nalo Leo alfajiri.

Nikaview dp, Mimi sio msahaulifu huyu mwanamke namfahamu, huwa namuona hapa mtaani lakini anapoishi sipajui.
Nikanyanyuka kwa hasira nikiwa na simu yangu natembea kwenda kumtafuta huyu mwanamke.

Nikafika uwanjani kulikua na watoto wa makamo wameweka kijiwe chao.
Nikawafata, nikawaonyesha picha "nani anapajua kwa huyu Dada" nikawauliza
Wote walionekana wanapajua, ni Mimi tu kushinda ndani sana sipajui majumbani kwa watu.

...............................
Ni nyumba yenye vyumba vingi lakini nimeambiwa niende vyumba vya uani
"Jamani za saa hizi! Nimemkuta Angel" niliwauliza wakina mama waliokua wanapiga umbea pale uani

"Chumba chake ni hicho! Lakini sijui kama mwenyewe yupo" mmoja alinijibu

"Asante" nikamjibu

Ni hasira tu ndio zilinifanya niende kwa mwanamke niliyeambiwa anaitwa Angel, lakini naamini mzee wangu yupo hapa na kama hayupo nataka Angel aniambie kwanini anatembea na mpenzi wangu.

Nikabisha hodi Mara kadhaa lakini mlango haufunguliwi ndani sauti ya mwanamke imekazana kuuliza "nani anayegonga"
Na Mimi sijibu naendelea kugonga.

Mlango ulifunguliwa, aliponiona akashtuka sana bila kutegemea nikapandisha jazba nilifoka nikisema namtaka mume wangu.

"Mume wako yupi? Mbona Mimi ndani nipo peke yangu, sitaki matatizo naomba uende bibie" Angel nae akapayuka

Nikaona ananichelewesha nikamsukumia ndani tukatokea sebleni ila hakukua na mtu nikafungua pazia kuingia kwenye chumba nilichojua kinatumika kwa ajili ya kulala nako kulikua tupu.

"Hapana! Siwezi kuondoka chooni kuja mtu nataka kujua ni nani" nikasema
Muda huo watu wamejaa mpaka chumbani.

"Unaona hizi nguo ni za mume wangu" nikawaambia

"Bwana hakutaki wewe ndiye unamng'ang'ania" Angel alisema

Wapambe wakatuambia tunazidi kujaza watu ebu tukae tuyamalize.

Kauli ya Angel iliniuma tukaanza kupigana huku watu wanatugombelezea.
Inaonekana mjumbe alipewa taarifa sababu alikuja nikatolewa nje lakini Kule chooni mzee hakutoka mpaka baadae mjumbe alipoamuru tuongozane nae kwake.

Mzee wangu alitoka kwenye kile chumba huku amekasirika, akaanza kunifokea "utoto utaacha lini? Kwani nyumbani nisingerudi"

Moyo uliniuma nikaanza kupayuka mbele ya umati wa watu
"Mungu atakulaani wewe! Huna shukrani umeniharibia maisha yangu umeniambukiza ukimwi kila siku unaniingilia kinyume na maumbile lakini uachi kunisaliti"

Watu waliokuwepo pale wakaanza kuzomea, wengine wakawa wananiambia ninyamaze hayo ni mambo ya siri ila Mimi sikujali niliendelea kuzimwaga siri.
Nikimtupia jicho Angel naona na yeye anashtuka na hii taarifa ya ukimwi.

.................. ...............
BABA EMMY: Hesabu hizi pesa

TINA: Ni laki tano

BABA EMMY: Hiyo ni nauli ya kwenda kwenu na chenji inabaki. Tulipofikia hatuwezi kuendelea kua wote umejua kunitia aibu Leo.
Hii nyumba nimejenga nitaishi hapa siku zote lakini umenivua nguo nitawezaje kuwatizama watu machoni.

TINA: Naomba unisamehe ni hasira sitorudia tena.

Mzee alimaanisha alichokisema alinifukuza jioni ileile na Mimi sina pa kwenda.
Kwetu wanajua nipo Dar nafanya kazi ila narudi vipi nikiwa nimechoka sina mbele wala nyuma.

Nikapata wazo la kumpigia shoga yangu barmaid, alinielekeza alipo niende sababu alishahama kufanya kazi kwenye Bar X.

BARMAID: Usijali shoga yangu nitaongea na manager akupe na wewe kazi hapa Bar, ujichange uwe na kwako siunaniona Mimi nahudumia kijijini kwetu kwa kazi hiihii.
.............

Mzee wangu huwa hafungi milango ya nyumba na funguo, miaka yote tuliyoishi pamoja tukitoka huwa tunafunga geti kubwa tu.
Huwa anasema Hamna wezi wa kuiba.

Sasa Leo mwizi naenda kua Mimi haiwezekani aniache na laki tano tu kwa hasara alizonipa na huu ushauri nimeupata kwa shoga yangu.

Nilipofika nje ya nyumba taa zote zilikua zimezimwa nikajua huyu hayupo nikaruka ukuta shoga yangu nikamuacha nje nikaingia ndani nilipoona nyumba nzima hamna mtu nikachukua funguo ya akiba ya geti kubwa nikafungua kisha nikawapigia simu watu wa gari waje tupakie vitu.

Nilibeba friji, TV, king'amuzi na ungo wake, kitanda, masofa na vyombo vya udongo.

Shoga yangu akaniambia nibebe mpaka mapazia na mashuka nikatii hao tukaondoka zetu.

Kesho yake mzee alinipigia sana simu nikapokea
BABA EMMY: Hujambo

TINA: Sijambo

BABA EMMY: Wewe ndiye umechukua vitu vyangu?

TINA: Ndio

BABA EMMY: Vizuri! Natumaini hutonisumbua kwa vyovyote vile, mahusiano yetu yamefikia tamati hivyo vitu nimekuachia bila kinyongo naona vimekupa faraja.

Alipokata simu nililia sana shoga yangu alinibembeleza akaniambia wanaume ndivyo walivyo.
Nikapanga chumba nikiwa na kila kitu ndani nikaanza kuishi na shoga yangu huku nasubiri kazi ya bar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…