Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 3,506
- 6,305
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wewe hapoNani mlokole?
Mh hii hatari sana aisee na inaogpesha sana anyway ngoja tuendelee kujifunzaSEHEMU YA 5
Kiukweli nilichukia sana!
Nilianza kumtumia Mzee msg za matusi kwasababu simu zangu alikua hapokei
"Hivi wewe unanichukuliaje, mabaya yote uliyonisababishia nilidhani utatulia ikibidi unioe lakini hufungi zipu unaruhusu malaya wa ko ananifata hadi nyumbani
Kaa ukijua mwanaume haupo peke yako na mimi sijajikatia tamaa kiasi hicho ms3nge wewe" nilimtumia hii msg lakini hakujibu.
Nilishinda ninalia nikijua mzee atarudi muda wowote, nia yangu ni arudi nyumbani anikute ninalia lakini nilishinda mpaka saa 4 usik u ndio akarudi na muda huo machozi yashanikauka.
BABA EMMY: Umeshindaje?
Ghafla nikaanza kulia upya huku namwambia "nataka kwenda kwetu umeniharibia maisha yangu, hunipendi una wanawake chungu nzima"
BABA EMMY: Nikupe nauli ya kwenu kiasi gani? Ukiondoka utakua umenipunguzia matatizo, kukaa na mtoto wa mtu huku wazazi wake hawajui ni mtihani.
TINA: Kumbe kweli hunipendi! Wanaume wengi wananitaka ila nawakataa kisa wewe angalia usije kujutia kunipoteza.
BABA EMMY: Ebu nipe namba za hao wanaume.
TINA: Wewe za nini mpaka nikupatie?
Niliongea huku nimefurahi nikijua hili biti limemtikisa.
BABA EMMY: Niwapigie waje kukuchukua wao siwanakutaka!
Niliishiwa pozi, nikatoka kama nilivyokua na kipensi changu juu ya magoti nikaanza kutembea njiani, nilitembea mpaka akili zikanirudi kuangalia saa ni 6 usiku.
Nikapata wazo niende kwenye Bar X ambapo mara nyingi naendaga na Mzee haipo mbali sana na kwetu ni kama vituo viwili tu.
........................................
BARMAID: Dada nikuhudumie nini?
Nikaganda kwa dakika kadhaa lakini Barmaid akarudia swali lake lile lile.
Nikaanza kuangua kilio, ilibidi mdada wa watu akae akaniangalia kwa makini kisha akaniuliza "Leo umekuja mwenyewe? inaonekana haupo sawa, bwana ako yupo wapi?"
Wahudumu wa hii Bar wananifahamu na mzee, sababu huwa tunakuja sana.
Kilio changu hapa Bar kimebeba mengi, nakumbuka mzee anayonifanyia pia nipo hapa sina hata shillingi 50.
Mzee huwa hanipatii pesa zaidi ya chakula kuhusu kusuka ananipa inayotoshea bila ya nyongeza.
TINA: S ijui niagize nini sababu sins hata pesa na bwana angu unayemuulizia nimegombana nae ndo nalia hapa.
BARMAID: Eeeh! Shoga unakaa unamlilia mzee kama yule kwa kipi? Mbona wewe ni mzuri!
TINA: Tatizo tumetoka mbali, nimefeli mpaka chuo kwa sababu yake.
BARMAID: Nipe namba yako tutazidi kuwasiliana siwezi kuendelea kukaa, hapa nipo kazini.
TINA: 07....
BARMAID: Wewe tulia hapohapo huwezi kukosa wa kukununulia pombe mimi nitakua napita kukuangalia ila usiondoke bila kuniaga.
Nilifurahi nimepata shoga mpya nimemuelezea shida yangu na kanielewa haraka.
Haukupita muda mrefu shoga yangu akanirudia.
BARMAID: Sikia! Twende ukakae Mesa ile pale, unamuona yule kaka aliyekaa peke yake.
TINA: Ndio! Nimemuona
BARMAID: Naomba nikuitie, twende ukakae unywe pombe zake ila akitaka kwenda kulala na wewe usikubali hata namba usimpe. Yule ni chawa ila Boss wake atakuja muda sio mrefu Hugo ndiye wa kudeal nae.
Nikatii amri! "Nawezaje kukaa kwenye Bar ya watu bila kuagiza chochote? Acha nikamwage mboga kama mzee alivyomwaga ugali" nikajisemea.
Na kweli yule chawa alianza kunipa maneno lakini nilimpuuzia huku nikiangaza macho kumsubiri huyo Boss na alifika.
Shoga yangu akaja haraka kwenye Meza yetu akamwambia Boss "Kila siku ananiambia mimi mchoyo Sasa leo mtoto huyo hapo"
Nilishtuka na ile kauli ilibidi nimkate jicho barmaid na yeye akaniangalia akanikonyeza.
Boss akamuuliza "Nilidhani ni shemeji yangu kwa Y"
Y akimaanisha mkaka ambae nimeambiwa ni chawa.
Barmaid akamjibu "Huyu wa kwako, mtoto anataka hela"
Boss akanigeukia akaniuliza "kweli?"
Nikamjibu "Ndio"
Akatuambia wote tuagize tunachotaka nikaagiza kitimoto na bia.
Simu yangu ikatoa mlio wa msg nikaifungua nikaona namba ngeni imeniambia CHANGAMKA SHOGA MSAADA WANGU NDIO HUO.
"Ukinifurahisha na mimi nitakufurahisha, usipige simu mpaka nikupigie, tuma msg whatsApp mimi ni mume wa mtu nina familia" Haya ni maelekezo napewa na Boss tukiwa gesti baada ya kuvunja amri ya 6.
Akanipa laki moja kisha akaondoka, Tina mimi sio mchoyo nikaenda kumuaga shoga yangu mpya na kumuachia elfu 20. Sasa naianza safari kwenda kupambana na mzee.
......................
TINA: Naomba tutumie kondomu
BOSS: Kwani huniamini? Nina mke nawezaje kua na ukimwi?
TINA: Hamna sio hivyo
BOSS: Ila? Au wewe unao?
TINA: Hapana sina ila kondomu inazuia hata mimba.
BOSS: Mimi nataka kavukavu, kuhusu mimba P2 zipo.
Mimi ni nani nimkatalie Boss wakati nishaambiwa ana hela?
Muda huo simu nimeweka Do not disturb ili nisisikie simu na msg za Mzee anayeniuliza nipo wapi.
Katika watu wote humu wewe ndie mtu pekee unanishawish kukuona siku.moja stor yako ya jeshi niliipendq sana
Pale huyu dada kaandika...... nyuzi zake ni kama zina sumaku fulani hivi ya kumvuta msomaji..... Watu wanajua kuandika.... Hongera sana ephenKatika watu wote humu wewe ndie mtu pekee unanishawish kukuona siku.moja stor yako ya jeshi niliipendq sana
Hutaki kuniita ukipandisha episode, hv una nn we bintiiii????Nimefanyaje tena?
Safi dada mzuri naomba tamu 😋😋😋Poa za wewe
We jinsia gani mkuu 😂ephen_ good night dada mzuri 😋