Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

SEHEMU YA 4
Mimi na chuo tushamalizana lile boom nililokua napewa halipo tena, nyumbani siwezi kurudi, nyumbani kwa shangazi siwezi kwenda na hostel siwezi tena kuendelea kukaa nitaishi wapi kwenye jiji hili LA Dar.

BABA EMMY: Fanya tu urudi nyumbani kwenu.
TINA: Naendaje nyumbani na hali hii? Chuo nimefeli bado Nina maambukizi
Naongea huku nalia.
BABA EMMY: Aisee unajua nilikua nimeshasahau.
Aliongea huku anacheka!
Nikamuangalia nikamwambia "Naomba niishi nyumbani kwako"

BABA EMMY: Kwangu hutopaweza, hapakauki wageni ndugu zangu kila siku wanakuja.
TINA: Sasa Mimi nitaishi wapi? Basi nipangie chumba.
BABA EMMY: Kipindi hiki sina hela kabisa.

Nilianza kuangua machozi huku nasema "basi acha nirudi nyumbani nimuelezee baba ukweli wote"

Baba Emmy alishtuka sana "umwambie nini?
" kua nimefeli chuo ikiwezekana na afya yangu" nikamjibu

Nilikua radhi nimuambie ukweli baba kuliko mama, baba yangu ananidekeza sana ila mama ni mkali.

Kwa jinsi nilivyojielezea kwa mzee wangu nilimuona ameogopa akakubali nikaishi kwake kwa masharti wageni wakija nijifungie chumbani kwake.
.......................

Maisha hayakua marahisi upweke uliniandama, nafikiria hatma yangu ni ipi baada ya kudisco chuo
Mzee yeye yupo busy na kazi ni kawaida mimi kulala peke yangu hata Mara 4 kwa wiki nikiuliza naambiwa ubusy wa kazi.

Miezi ilikatika nyumbani wakinipigia simu "vipi masomo" nawajibu "salama kabisa" uzuri wazazi wangu hawana utamaduni wa kuulizia matokeo.

Niligundua mzee amekua na tabia mpya ya kutonizingatia, nilianza kuona gap ya umri wetu kosa kidogo utasikia ananiambia "Acha utoto" au "watoto wa siku hizi bhana" Haya ni maneno ya rejareja yalikua yananiudhi .
Simu yake kila app ameweka pattern, nilikua natupa jicho mpaka nikajua pattern yake lakini changamoto ilikuja sijui password ya simu.

Nataka kukagua simu yake sababu muda wote akishinda nyumbani vidole vinachat tu.
..............................
Natembea kurudi nyumbani huku ninalia macho yote kwenye simu ya mzee wangu.
Siamini ninachokiona WhatsApp imejaa chats za wanawake tofauti wengine namba hazijaseviwa, magroup ya wanawake wanaojiuza yamejaa kwenye simu yake.
Nimefeli chuo, nina maambukizi kisa huyu mzee. Ana umri sawasawa au kumzidi baba yangu lakini Mimi nampenda na nilijua tunapendana kumbe mwenzangu huyu ni Malaya.

"Tina! Chukua simu hii kanisaidie kutoa pesa kwa wakala, namba ya siri ni 1971 tembea huku unachezea screen ili simu isijizime" Mzee wangu aliniambia.

Hii nafasi nilikua naisubiri sana ili nikague simu yake, amejiamini kwasababu ana uhakika kila app ina pattern bila kujua Mimi naifahamu.

BABA EMMY: Shida nini mbona umerudi unalia? Umeibiwa au?
TINA: Kumbe wewe hunipendi! Una wanawake zako chungu nzima unachat nao WhatsApp.

Akanipokonya simu yake akaikagua kisha akaniambia "Utoto sitaki tena ukiendelea na hii tabia yako itabidi urudi tu nyumbani kwenu, ningekua sikupendi nisingekaa na wewe hapa bila kujali ukipata matatizo Mimi ndiye nitakua na msala"

Akavaa akaondoka, nilikaa siku mbili bila yeye kurudi wala kunipigia simu hats msg.
Nilikaa na hasira niliwaza au nimpigie Emmy nimuhadithie jinsi baba yake anavyonitesa? Ila nikaona atanishangaa nitachekesha.

Nilimkumbuka mzee wangu nikaona bora nijishushe nimtumie msg ya kumuomba msamaha ili arudi nyumbani na kweli alinijibu kua atarudi jioni muhimu hataki kelele.

Nilifungua ukurasa mpya kwenye mahusiano yangu, ukurasa wa mateso Mtu ananiaga anatoka lakini harudi nyumbani na najua kabisa anaenda kwa wanawake wengine nikiuliza inakua kosa najiliza lakini ananiambia "Fanya uende kwenu"
Narudije nyumbani na hali hii nimeshakua mchafu vya kutosha au nitafute mwanaume mwingine? Lakini na hali yangu hii nani atanikubali?

Mimi na Emmy atuwasiliani Mara kwa Mara! Anaishia kuview status zangu na Mimi hivyohivyo ila Leo nakuta ujumbe wa shoga yangu huyu wa zamani

EMMY: Mambo Tina! Naomba nikualike kwenye dinner siku ya graduation yangu. Tar 10 siutakua na nafasi? Sherehe itafanyika hotel X kwenye rooftop
Mimi ni nani nikatae kwenda kwenye sherehe ya rafiki yangu wa zamani, sherehe ya mtoto wangu wa kambo?

TINA: Nitakuja usijali.

Nilimpa hiyo taarifa mzee wangu na yeye hakua na neno Mimi kwenda japo aliniambia yeye hatokuepo kwenye sherehe hiyo ila gharama zote yeye ndo kalipia.
............................
Nilijitahidi kupendeza sababu najua naenda kukutana na mabinti wa rika langu japo naamini nimewazidi dhambi.

Emmy alifurahi kuniona nilifurahi pia kumuona rafiki yangu amekua mrembo haswaa.
Nilitupa jicho mbele nikaona pamepambwa
"Beauty with brain,
Upper Second Class,
Congratulations Emilliana"

Nilishindwa kuvumilia nikanyanyuka kwenda chooni, nimefikia kioo najiangalia huku ninalia.

Kwanini nalia? Nalia sababu najiona Mimi ni mchafu, nilikua ni binti kwenye ndoto nyingi kama Emmy.
Niliamini nitasoma na kumaliza chuo, nipate kazi nisaidie familia yangu haswaa wadogo zangu ambao macho yao yapo kwangu.
'Beauty with brain' natamani ningekua mimi
Lakini kwanini sijawa? Sijawa kwasababu ya baba Emmy.

Ameharibu maisha yangu huku akitengeneza ya mtoto wake.

"Jitahidi usome kwa bidii, mtu yeyote asikudanganye huko chuo ukiwa na shida ya pesa niambie na usijiunge kwenye makundi ya hovyo" Hays ni maneno ambayo Mara nyingi baba Emmy alikua anamwambia Emmy kwenye simu.
...............................
MAMA EMMY: Tina umekua, hujambo?
TINA: Sijambo mama
MAMA EMMY: Mbona umekaa kihuzuni vipi na wewe chuo?

Haya ni maongezi na mama Emmy wakati nimetoka chooni kulia.

TINA: Chuo sijamaliza nilisitisha mwaka nilikua naumwa.
MAMA EMMY: Pole sana mwanangu, Mungu atakusaidia.

Huyu ni mama mtu mzima ambaye tunafahamiana nilitambulishwa kwake na Emmy kipindi tupo sekondari.
Nilitamani nimshike mkono nimuhadithie jinsi mzazi mwenzake anavyonitesa.
.........................
Wazazi wanajua binti yao nimeshamaliza chuo wananiuliza kila siku ni lini narudi nyumbani? Nawapiga chenga sababu zikiwa nyingi ikiwemo nipo Dar natafuta kazi hata ya kujitolea na baba anaridhika na jibu hili.

Hiyo siku nipo zangu jikoni napika nikasikia geti limebamizwa kwa nguvu sana nikashtuka ila sikwenda kujificha kama kawaida wakija ndugu zake na mpenzi wangu.
Ndugu sake huwa wanatoa taarifa kabla ya kuja lakini siku hiyo taarifa hamna hivyo nina shauku ya kujua ni nani huyo kaja nyumbani kwangu?

Mwanamke mweupe mrefu kwa kukadiria umri ni 30's aliniangalia kwa umakini kisha akaniuliza "Wewe ni nani"
Nikabaki nimemtizama bila jibu
"Usiniambie Alex amefikia hatua hii ya kuleta Malaya wachanga nyumbani kwake" akaongezea

Sasa mpaka japo nikajiongeza huyu atakua ni mchepuko wa mzee tu.

"Binti! Unajipenda kweli? Unajua nilikuja kwa Shari nilikua nakuja kuua mtu Leo, lakini baada ya kukuona nimeishiwa pause" akaniambia

"Nakuonea huruma sana! Watoto wa siku hizi mnapenda kuparamia mambo makubwa nikushauri tu kama mdogo wangu hapa umeingia choo cha kiume"

Akachukua simu akapiga akaanza kuongea na mtu niliuejua ni mzee akamwambia "Mbona una dhambi wewe! Haya mtoto mdogo hivi unataka kumuharibia maisha yake? Una laana wewe nakuambia" aliongea sana alipomaliza akaniambia siku akirudi asinikute mule ndani kisha akaondoka.
Hii episode nimeisoma huku nasikiliza wimbo wa Alikiba ~ Macmuga najikuta kusikitika sana aseeh
 
SEHEMU YA 5
Kiukweli nilichukia sana!
Nilianza kumtumia Mzee msg za matusi kwasababu simu zangu alikua hapokei
"Hivi wewe unanichukuliaje, mabaya yote uliyonisababishia nilidhani utatulia ikibidi unioe lakini hufungi zipu unaruhusu malaya wako ananifata hadi nyumbani
Kaa ukijua mwanaume haupo peke yako na mimi sijajikatia tamaa kiasi hicho ms3nge wewe" nilimtumia hii msg lakini hakujibu.

Nilishinda ninalia nikijua mzee atarudi muda wowote, nia yangu ni arudi nyumbani anikute ninalia lakini nilishinda mpaka saa 4 usiku ndio akarudi na muda huo machozi yashanikauka.

BABA EMMY: Umeshindaje?
Ghafla nikaanza kulia upya huku namwambia "nataka kwenda kwetu umeniharibia maisha yangu, hunipendi una wanawake chungu nzima"

BABA EMMY: Nikupe nauli ya kwenu kiasi gani? Ukiondoka utakua umenipunguzia matatizo, kukaa na mtoto wa mtu huku wazazi wake hawajui ni mtihani.

TINA: Kumbe kweli hunipendi! Wanaume wengi wananitaka ila nawakataa kisa wewe angalia usije kujutia kunipoteza.

BABA EMMY: Ebu nipe namba za hao wanaume.

TINA: Wewe za nini mpaka nikupatie?
Niliongea huku nimefurahi nikijua hili biti limemtikisa.

BABA EMMY: Niwapigie waje kukuchukua wao siwanakutaka!

Niliishiwa pozi, nikatoka kama nilivyokua na kipensi changu juu ya magoti nikaanza kutembea njiani, nilitembea mpaka akili zikanirudi kuangalia saa ni 6 usiku.

Nikapata wazo niende kwenye Bar X ambapo mara nyingi naendaga na Mzee haipo mbali sana na kwetu ni kama vituo viwili tu.
........................................
BARMAID: Dada nikuhudumie nini?
Nikaganda kwa dakika kadhaa lakini Barmaid akarudia swali lake lile lile.
Nikaanza kuangua kilio, ilibidi mdada wa watu akae akaniangalia kwa makini kisha akaniuliza "Leo umekuja mwenyewe? inaonekana haupo sawa, bwana ako yupo wapi?"

Wahudumu wa hii Bar wananifahamu na mzee, sababu huwa tunakuja sana.

Kilio changu hapa Bar kimebeba mengi, nakumbuka mzee anayonifanyia pia nipo hapa sina hata shillingi 50.
Mzee huwa hanipatii pesa zaidi ya chakula kuhusu kusuka ananipa inayotoshea bila ya nyongeza.

TINA: Sijui niagize nini sababu sins hata pesa na bwana angu unayemuulizia nimegombana nae ndo nalia hapa.

BARMAID: Eeeh! Shoga unakaa unamlilia mzee kama yule kwa kipi? Mbona wewe ni mzuri!

TINA: Tatizo tumetoka mbali, nimefeli mpaka chuo kwa sababu yake.

BARMAID: Nipe namba yako tutazidi kuwasiliana siwezi kuendelea kukaa, hapa nipo kazini.

TINA: 07....
BARMAID: Wewe tulia hapohapo huwezi kukosa wa kukununulia pombe mimi nitakua napita kukuangalia ila usiondoke bila kuniaga.

Nilifurahi nimepata shoga mpya nimemuelezea shida yangu na kanielewa haraka.

Haukupita muda mrefu shoga yangu akanirudia.

BARMAID: Sikia! Twende ukakae Mesa ile pale, unamuona yule kaka aliyekaa peke yake.

TINA: Ndio! Nimemuona
BARMAID: Naomba nikuitie, twende ukakae unywe pombe zake ila akitaka kwenda kulala na wewe usikubali hata namba usimpe. Yule ni chawa ila Boss wake atakuja muda sio mrefu Hugo ndiye wa kudeal nae.

Nikatii amri! "Nawezaje kukaa kwenye Bar ya watu bila kuagiza chochote? Acha nikamwage mboga kama mzee alivyomwaga ugali" nikajisemea.

Na kweli yule chawa alianza kunipa maneno lakini nilimpuuzia huku nikiangaza macho kumsubiri huyo Boss na alifika.

Shoga yangu akaja haraka kwenye Meza yetu akamwambia Boss "Kila siku ananiambia mimi mchoyo Sasa leo mtoto huyo hapo"

Nilishtuka na ile kauli ilibidi nimkate jicho barmaid na yeye akaniangalia akanikonyeza.

Boss akamuuliza "Nilidhani ni shemeji yangu kwa Y"
Y akimaanisha mkaka ambae nimeambiwa ni chawa.
Barmaid akamjibu "Huyu wa kwako, mtoto anataka hela"

Boss akanigeukia akaniuliza "kweli?"
Nikamjibu "Ndio"

Akatuambia wote tuagize tunachotaka nikaagiza kitimoto na bia.

Simu yangu ikatoa mlio wa msg nikaifungua nikaona namba ngeni imeniambia CHANGAMKA SHOGA MSAADA WANGU NDIO HUO.

"Ukinifurahisha na mimi nitakufurahisha, usipige simu mpaka nikupigie, tuma msg whatsApp mimi ni mume wa mtu nina familia" Haya ni maelekezo napewa na Boss tukiwa gesti baada ya kuvunja amri ya 6.
Akanipa laki moja kisha akaondoka, Tina mimi sio mchoyo nikaenda kumuaga shoga yangu mpya na kumuachia elfu 20. Sasa naianza safari kwenda kupambana na mzee.

......................
TINA: Naomba tutumie kondomu
BOSS: Kwani huniamini? Nina mke nawezaje kua na ukimwi?
TINA: Hamna sio hivyo
BOSS: Ila? Au wewe unao?
TINA: Hapana sina ila kondomu inazuia hata mimba.
BOSS: Mimi nataka kavukavu, kuhusu mimba P2 zipo.

Mimi ni nani nimkatalie Boss wakati nishaambiwa ana hela?
Muda huo simu nimeweka Do not disturb ili nisisikie simu na msg za Mzee anayeniuliza nipo wapi.
 
Gridi ya taifa

Back
Top Bottom