figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Nape Nnauye aliwahi kusema "Bahari imetulia, Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi".
Kuna utawala uligubikwa na Sintofahamu ya Watu kupotea, kufa, kubambikiziwa kesi.
Utawala uliteneza kundi la watu wasiojulikana ambao kazi yao ilikuwa kumshughulikia yoyote atakayekuwa na Mawazo mbadala au kuhoji matumizi ya fedha za Serikali.
Tukamuomba Mungu na kusoma albadiri ili atuepushie na kikombe kile, Mungu akasikia maombi yetu
Sasa leo kuna watu wamekosa maji na umeme kwa siku kadhaa wanatamani kurudi utumwani Mungu alikotutoa na wanamlaumu Mungu kwanini katutoa kule ambapo mtu alikuwa hajui kesho yake kama ataamka salama. Mbona vijijini watu hawana Umeme na Wanaishi? Itakuwa huu umeme wa kukosa mwezi mmoja ndo utamani kurudi Misri? Jipe moyo Utashinda
Hata Wana wa Israel walipookolewa Misri utumwani walitamani kurudi huko. Ndo hawa wanaotamani kurudi tulikotoka.
Nawatia Moyo, tulieni tuiunge Mkono Serikali na Mamlaka yake kwani Mamlaka ya Serikali yanatoka kwa Mungu. Giza likiwa nene kunakalibia kupambazuka
KUTOKA 14:11
11 Wakamwambia Mose, “Je, hapakuwa na makaburi ya kutosha nchini Misri hata ukatuleta tufie huku jangwani? Mbona umetutendea haya, kwa tututoa katika nchi ya Misri?
12Je, hatukukuambia mambo haya tulipokuwa bado Misri? Tulikuambia utuache tuendelee kuwatumikia Wamisri. Ingalikuwa afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufia huku jangwani.”
13Mose akawaambia Waisraeli, “Msiogope! Kaeni imara! Leo mtaona jinsi Mwenyezi-Mungu atakavyowaokoa. Maana, hawa Wamisri mnaowaona leo, hamtawaona tena.
14Mwenyezi-Mungu atawapigania; nyinyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu.”
15Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kwa nini mnanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele.
16Inua fimbo yako na kuinyosha juu ya bahari. Maji yatagawanyika na Waisraeli wataweza kuvuka katikati ya bahari mahali pakavu.
Viongozi wetu washainua Fimbo juu, tutavuka salama