Bora tukose umeme na Maji kuliko watu kupotea na kuokotwa kwenye Viroba baharini Coco Beach

Bora tukose umeme na Maji kuliko watu kupotea na kuokotwa kwenye Viroba baharini Coco Beach

Salaam Wakuu,

Nape Nnauye aliwahi kusema "Bahari imetulia, Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi".

Kuna utawala uligubikwa na Sintofahamu ya Watu kupotea, kufa, kubambikiziwa kesi.

Utawala uliteneza kundi la watu wasiojulikana ambao kazi yao ilikuwa kumshughulikia yoyote atakayekuwa na Mawazo mbadala au kuhoji matumizi ya fedha za Serikali.

Tukamuomba Mungu na kusoma albadiri ili atuepushie na kikombe kile, Mungu akasikia maombi yetu

Sasa leo kuna watu wamekosa maji na umeme kwa siku kadhaa wanatamani kurudi utumwani Mungu alikotutoa na wanamlaumu Mungu kwanini katutoa kule ambapo mtu alikuwa hajui kesho yake kama ataamka salama. Mbona vijijini watu hawana Umeme na Wanaishi? Itakuwa huu umeme wa kukosa mwezi mmoja ndo utamani kurudi Misri? Jipe moyo Utashinda

Hata Wana wa Israel walipookolewa Misri utumwani walitamani kurudi huko. Ndo hawa wanaotamani kurudi tulikotoka.

Nawatia Moyo, tulieni tuiunge Mkono Serikali na Mamlaka yake kwani Mamlaka ya Serikali yanatoka kwa Mungu. Giza likiwa nene kunakalibia kupambazuka

KUTOKA 14:11

11 Wakamwambia Mose, “Je, hapakuwa na makaburi ya kutosha nchini Misri hata ukatuleta tufie huku jangwani? Mbona umetutendea haya, kwa tututoa katika nchi ya Misri?

12Je, hatukukuambia mambo haya tulipokuwa bado Misri? Tulikuambia utuache tuendelee kuwatumikia Wamisri. Ingalikuwa afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufia huku jangwani.”

13Mose akawaambia Waisraeli, “Msiogope! Kaeni imara! Leo mtaona jinsi Mwenyezi-Mungu atakavyowaokoa. Maana, hawa Wamisri mnaowaona leo, hamtawaona tena.

14Mwenyezi-Mungu atawapigania; nyinyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu.”

15Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kwa nini mnanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele.

16Inua fimbo yako na kuinyosha juu ya bahari. Maji yatagawanyika na Waisraeli wataweza kuvuka katikati ya bahari mahali pakavu.

Viongozi wetu washainua Fimbo juu, tutavuka salama
Wadanganye hao hao,

Bahari Bado haijatulia, hapajakucha Bado.

KITI Bado hakikaliki.

Machungu juu ya wananchi yakupe ALARM!!!!

Angalizo: Kutumia vifungu vya BIBLIA, kitabu KITAKATIFU Kwa HILA, unajitafutia LAANA.

Acha mara moja, UTAPIGWA, Mungu hadhihakiwi.
 
Salaam Wakuu,

Nape Nnauye aliwahi kusema "Bahari imetulia, Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi".

Kuna utawala uligubikwa na Sintofahamu ya Watu kupotea, kufa, kubambikiziwa kesi.

Utawala uliteneza kundi la watu wasiojulikana ambao kazi yao ilikuwa kumshughulikia yoyote atakayekuwa na Mawazo mbadala au kuhoji matumizi ya fedha za Serikali.

Tukamuomba Mungu na kusoma albadiri ili atuepushie na kikombe kile, Mungu akasikia maombi yetu

Sasa leo kuna watu wamekosa maji na umeme kwa siku kadhaa wanatamani kurudi utumwani Mungu alikotutoa na wanamlaumu Mungu kwanini katutoa kule ambapo mtu alikuwa hajui kesho yake kama ataamka salama. Mbona vijijini watu hawana Umeme na Wanaishi? Itakuwa huu umeme wa kukosa mwezi mmoja ndo utamani kurudi Misri? Jipe moyo Utashinda

Hata Wana wa Israel walipookolewa Misri utumwani walitamani kurudi huko. Ndo hawa wanaotamani kurudi tulikotoka.

Nawatia Moyo, tulieni tuiunge Mkono Serikali na Mamlaka yake kwani Mamlaka ya Serikali yanatoka kwa Mungu. Giza likiwa nene kunakalibia kupambazuka

KUTOKA 14:11

11 Wakamwambia Mose, “Je, hapakuwa na makaburi ya kutosha nchini Misri hata ukatuleta tufie huku jangwani? Mbona umetutendea haya, kwa tututoa katika nchi ya Misri?

12Je, hatukukuambia mambo haya tulipokuwa bado Misri? Tulikuambia utuache tuendelee kuwatumikia Wamisri. Ingalikuwa afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufia huku jangwani.”

13Mose akawaambia Waisraeli, “Msiogope! Kaeni imara! Leo mtaona jinsi Mwenyezi-Mungu atakavyowaokoa. Maana, hawa Wamisri mnaowaona leo, hamtawaona tena.

14Mwenyezi-Mungu atawapigania; nyinyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu.”

15Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kwa nini mnanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele.

16Inua fimbo yako na kuinyosha juu ya bahari. Maji yatagawanyika na Waisraeli wataweza kuvuka katikati ya bahari mahali pakavu.

Viongozi wetu washainua Fimbo juu, tutavuka salama
Ujinga ujinga tu, utavumiliaje kukosa maji katikati ya Jiji!!

Una HAKIKA pale MAGOGO I hakuna maji pia?

Au unataka tuje kuhakikisha.!!!!!
 
Sasa msihalalishe huu udhaifu wa kukosa umeme na maji kwa kukumbusha mambo yaliyopita, ni kweli kwamba jamaa alifanya uhalifu na mambo yasiyofaa, ila isiwe kichaka, tunataka maji na umeme wa uhakika.

Kukubali tu kwamba jamaa ni kweli alifanya uhalifu tayari umeshawekwa,kaa hapo hapo kwa mleta mada.
 
Wanasema raisi kama malaika

Nadhani haujaipitia katiba yako vizuri kwa sababu ndio inayo mpa nguvu raisi kutekeleza ayatakayo.

Ila sisi watanzania ni wepesi sana wa kusahau tulipo toka

Lau kama Kiongoz wa awam ya 6 angegombea 2015 sizan kama angetoboa.

Hii nchi lile jembe kaichukua ikiwa imeoza
Kuisafisha kwake kulihitaji maamuzi magumu

Jakaya mwenyewe alishawai sema kuwa si mnataka raisi mkali? Basi nimewaletea JPM

Mwinyi mwenyew akasema wao walipambana na rushwa ila JPM kaisambaratisha kabisa.

Mauwaji (maono yangu)
1.Ni mchezo Mchafu wa kisiasa
2.wewe ukiujua wa iv mm naujua wa iv
3.ujambazi/uhuni wa aina yoyote ule ulipotea
Amani ilikuwepo kwa asilimia kubwa sana

Na nukuu ya aliye tangulia kusema
Tulia sindano/chanjo ya mtu aliyekufa ikuingie

Swali: Hivi awamu ya 6 imeingiaje bila kampeni?

Kwa sababu sijapiga kura kwa awamu ya sita kura yangu ilikuwa awamu ya tano muhula wa pili.
 
Mnalalamika maji wakati upo jirani na bahari?Uzembe huo.Na kama umeme wa Tanesco wa kukupa mwanga hakuna,tumia solar power.Nayo huna?Basi tumia kijinga cha moto kumulika palipo giza.😂😂😂😂
 
Bora mama kuliko yule muuwaji na hata wakati wa muuwaji njaa ilikuwepo ila wakuu wa wilaya walitishwa wakaambiwa ole wako utangaze wilaya yako ina njaa! Wakaufyata! Tukija kwenye umeme pia ulikuwa unakatika kama kawaida na tanesco wakaacha kufanya matengenezo ili tu kulazimisha umeme uwake kiufupi lile dubwana bora Mungu kalitowesha!
Nja inatangazwa?
 
Hebu tuulizane kitu kimoja, hao watu waliyokuwa wanauliwa katika utawala uliyopita walikuwa ni kundi gani la watu kwa maana ni wananchi tu wa kawaida? Waaandishi wa habari? Wanasiasa? Wafanya biashara au ni kundi gani hasa?

Hapa napoandika Tanesco washafanya yao muda huu huu.
waliokuwa wakiokotwa kwenye viroba hawakuwa hata na ndugu. Sijui alikuwa anawaua kutoka nje ya nchi?
 
Niukweli mwingi sana mpaka hapa Leo tunaenda mwaka wa 2 wasiojulikana hawapo.
 
Back
Top Bottom