Bora uitwe bahili kuliko kuitwa masikini

Bora uitwe bahili kuliko kuitwa masikini

Mwanaume ambae una mamlaka na hela yako utakua na mamlaka na maisha yako pia. Wanawake watakuita mbahili kwa sababu umekataa kuwamwagia hela lakini nakuambia ukweli, wanawake hao hao wanawaheshimu wanaume ambao wamejipata kupitia nidhamu ya hela.

Mwanaume ambae unatapanya pesa ukifikiria iyo ndio njia ya kupendwa utaishia kutumika na kuwa masikini. Ilinde hela yako, hela yako ndio ndugu, jamaa, mpenzi na rafiki wa kweli hapa duniani

Wanawake watakuweka majaribuni, watakuita mbahili, watakuona mtu cheap, watakuambia "tafuta hela". Usikubali kuingia kwenye mtego wao, they are trying to bully you because you are smart enough not to fall for their tricks.

Sikilizeni vijana, ngono haina maajabu kama ambavyo mnaitukuza. Sex is not worth striving for, quiting your plans for, go broke for or making your life miserable for. Stop competing against other men over this sex thing, start competing with yourself not to remain in the same level every year.

Thamani yako haiwezi kupatikana kwa kutapanya hela kwa mwanamke mjinga anaefikiri ana haki ya kupewa hela za bure kwa sababu tu yeye ni mwanamke, thamani yako itapatikana kwa kuwa na nidhamu ya hela na kuzifanya hela zako zikutumikie wewe mwenyewe.

Acha kuwapa hela wanawake wakati wewe mwenyewe bado hauna uhuru wa kifedha. Familia yako pia inahitaji hela, ni bora izo hela zikazunguke kwenye familia yako. Mwanamke ana nguvu na akili timamu, ana miguu miwili, mikono miwili na masaa 24 ya siku kama wewe. Hakuna ambacho kinamzuia kufanya kazi apate hela yake mwenyewe.

Wanawake sio wenzako. Mwanamke anaweza asiwe msomi, asiwe na ujuzi, awe masikini, asiwe na chochote cha kumpa mafanikio na bado akatoka kimaisha kupitia njia mbili tu. Moja ni kukutana na mwanaume ambae ameshajipata, mbili ni kutumia mwili wake kupata anachokitaka.

Lakini wewe mwanaume hauwezi kwenda na kanuni iyo. Mafanikio yako mwanaume ni mchakato wa nidhamu, muda, vikwazo na juhudi.

Uyo mwanamke ambae unaamini anahitaji msaada wako, anahitaji kuhudumiwa na wewe tambua kwamba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kimaisha kuliko wewe unaempa hela na

Mwanamke uyo atakapokutana na mwanaume atakaemwekea mezani dau kubwa kuliko analolipata kutoka kwako atakuacha bila kujiuliza hata mara moja. Ukipoteza muda wako kuwekeza kwake hela ambazo ulitakiwa kuwekeza kwa ajiri yako mwenyewe utaishia kuangamiza mustakabali wako.

Nipo hapa kufungua code ili uitoe akili nje ya matrix na kuuona ukweli. Ukiamua kuelewa au kukaza shingo huo ni uamuzi wako.
WEll said
 
Tatizo Ni Kutaka Kumpandisha Mtu Kili Mountain
20241012_143143.jpg
20241012_091721.jpg
20241012_091736.jpg
 
Yap kuna masuala mengine kama kubet, ulevi n.k.. lakini hili ni jukwaa la mahusiano ndio maana tuna-concentrate zaidi kwenye angle ya mahusiano
Nilimaanisha ujinga binafsi ndo unaweza kukufanya maskini coz pesa wanazohitaji wanawake kwetu ni kidogo sana ambazo wala hazifai kua kisingizio cha mtu kuishiwa.
 
Umetoka nje ya mada. Mwanaume hata asipokua malaya bado anaweza kuangukia mikononi na mwanamke chuma ulete.

Vile vile mwanaume anaweza kuwa malaya na akafanikiwa kufanya vetting katika kuchagua wanawake wa ku-date nao kwa kuangalia kigezo cha mwanamke anaejimudu kiuchumi, hii itamuwesha kutoingia gharama za ku-maintain mahusiano

Katika dunia ya sasa almost wanawake wote mapenzi kwao ni biashara. Wanachotofautiana ni mbinu tu.

Kuna ambao wanafanya biashara direct(mtandaoni, kumbi za starehe, kujipanga barabarani n.k) na kuna wanaofanya biashara indirect(kwa kujificha kwenye kichaka cha kuhudumiwa au kuwa masponsor wengi)

Kwa mwanaume bila kujali mwanamke yupi ambae utakutana nae maishani mwako, unawajibika kujipa kipaumbele wewe mwenyewe.
Umepangua hoja kwa ustadi mkubwa
 
Mh embu fafanua.
90% ya wafanya biashara wanahudumia rundo la wanawake bt daily mambo yanaenda.

Nadhani kinachoweza kufilisi kirahisi ni mikopo, kamari na ulevi wa sifa bt wanawake tunawasingizia bure.
 
Ila wanawake Mungu anawaona ,kuna jiran yetu mmoja enzi hizo wakati tunaishi oysterbay,alihama kwake oysterbay na kwenda kuishi msasani na kuacha familia

Omba tu usikamatwe na mwanamke
Ni ujinga tu, wala sio suala la kuomba
 
90% ya wafanya biashara wanahudumia rundo la wanawake bt daily mambo yanaenda.

Nadhani kinachoweza kufilisi kirahisi ni mikopo, kamari na ulevi wa sifa bt wanawake tunawasingizia bure.
Hao wafanyabiashara walianza walijijenga kwanza kupitia nidhamu ya hela ndio wakaanza kuhudumia wanawake. Sasa wewe na bela yako ya papatu papatu jaribu kuwageza.
 
Nilimaanisha ujinga binafsi ndo unaweza kukufanya maskini coz pesa wanazohitaji wanawake kwetu ni kidogo sana ambazo wala hazifai kua kisingizio cha mtu kuishiwa.
KWanini anahitaji pesa yako? Ni mtoto yatima au mlemavu asieweza kufanya kazi?
 
Hao wafanyabiashara walianza walijijenga kwanza kupitia nidhamu ya hela ndio wakaanza kuhudumia wanawake. Sasa wewe na bela yako ya papatu papatu jaribu kuwageza.
Ndio maana nikasena ujinga binafsi ndo unaweza kukufilisi na sio wanawake coz watu smart hufanya yaliyo ndani ya uwezo wao.
 
Linapokuja suala la mahusiano wanaume ni provider, hivo unapowahitaji wanawake pia ujue unajukum la kuprovide.
Kwanini uwe provider kwa mwanamke ambae ana access zote za kutafuta hela kama wewe?, jukumu la baba ake ni lipi?
 
Back
Top Bottom