Sasa mtu aliyemaliza form 6 akija kuomba kazi kwenye kampuni yangu nimuajiri kwenye nini? labda mesenja wa kupeleka barua na vifurushi.
Wafanya kazi wangu wamesoma ufundi veta kuna welders 2 , Lather 2 na Mimi mwenyewe nina mechanical eng degree, kazi yangu ni quality control na logistic ya material and resources.
Wafanyakazi wangu wakubwa ni hao wanne, na welders siku hizi wanafundishwa CAD drawing application yani anaweza kumsikiliza mteja anataka nini, halafu anachora kwa CAD, ukikubalika, anaanza kazi, ya kuchomelea mwenyewe mpaka mzigo unakamilika, pia na wale wa lathe machine wanachonga vipuri.
Sasa wewe wa form 6 utafiti wapi wakati hata kutoa mchoro wa CAD huwezi, labda kidogo ingekusaidia kupata kazi.