Bosi mpya TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga asema: Tunatarajia changamoto ya upungufu wa umeme imalizike Machi 2024

Bosi mpya TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga asema: Tunatarajia changamoto ya upungufu wa umeme imalizike Machi 2024

Wahuni sana toka nipo darasa la kwanza umeme wanakatakata sana
 
All the best!
Progress inaonekana kuanzia kwenye maneno.
Maneno yake yanaonesha kutakuwa na measurable result in a specified time period.
 
Mama yupo kazini,mama Anaendelea kulipa Taifa Tabasamu,Mama Anaendelea kufanya mapinduzi katika kila Eneo,Mama Anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania,Mama Anaendelea kusonga mbele kwa mafanikio makubwa,mama Anaendelea kuonyesha uwezo wake mkubwa wa kiuongozi,mama Anaendelea kuonyesha nakuwaumiza wale waliotaka na kutamani kuona akishindwa kuliongoza Taifa letu.mama Anaendelea kuwalaza na viatu wenye chuki binafsi na uongozi wake,mama Anaendelea kujizolea uungwaji mkono kutoka kwa watanzania wazalendo ,wenye akili Timamu na wenye mapenzi mema na Taifa letu,mama Anaendelea kutekeleza kwa kishindo mipango yenye kuleta matokeo chanya kwa watanzania,mama Anaendelea kulipaisha Taifa letu kiuchumi.
 
Amesema Shirika linaendelea kukamilisha utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere litakalokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2115 ambao mpaka sasa umefikia 92%
92% less leakages kwenye expansion joints
 
Huwezi tegemea maji kama umeme wa uhakika
 
Hv Hawa watu wanatuonaje watanzania? Kwan kauli ya kuwa ikifika kipindi Fulani kukatika umeme kutakuwa historia kumeanza kusemwa leo? C tokea kipindi cha JK. Tatizo viongozi wetu Huwa hawawajibiki kwa kauli zao.
 
Kwa wanaojenga au wenye nyumba tayari, hakikisheni mnawekeza kwenye solar kama mnavyowekeza kwenye milango na madirisha, Tanzania Kuna jua kuliko mahitaji,Kuna una pesa kidogo achana na hawa matapeli wa TANESCO wekeza kwenye solar, hakuna sababu ya kukosa u meme sasa
 
Ukiangalia ratiba ya TANESCO ni kuwa, tatizo la upungufu wa umeme yaani ratiba nzima ya mgao ingemalizikia juzi Dec 4 kwa Dar na mikoa kadhaa, lakini hamna kitu, kama matatizo ndio haya hiyo miezi 6 waliyopewa si ndio itakua ni bure kabisa?

Hivi Rais Samia una uchungu na hii nchi kweli? Unajua yaliyo kifuani kwako ni tofauti na uyatoayo majukwaani? Vipi nikisema kuna fikra ya "Bora liende tu?" Fikra ya kuamini Bara ni kama nchi ya kigeni ambayo utatumikia tu ila mwishoni unarejea zako Zanzibar na kwamba huwezi kuumiza kichwa kwa ajili ya Tanzania bara ambapo hata hivyo sio nchi yako kimuungano?

Ni sawa na mtu atoke Rwanda akawe Rais wa Burundi tu kwa muda akili yake itajua yupo pale tu lakini at the end atarudi zake Rwanda tu, so moyo wa kujitoa atakua hana maana pale kisaikolojia atapachukulia kama ugenini tu?
 
Ushawahi kuwaza Samia angekua Rais wa Zanzibar wazanzibari wasingeteseka hivi.

Samia angekua Rais wa Zanzibar, Wanzanzibar wasingeteseka hivi kwasababu mtu ni kwao

Kwa mfumo wetu wa sasa kinachotokea ni sawa na Kagame awe Rais wa Burundi tu kwa kipindi fulani huku akijuwa fika kabisa kuwa mwishoni burundi sio kwake pale anatimiza tu legacy ya kutawala lakini mwisho atamaliza hatamu yake na kurejea Rwanda, kwahiyo hawezi kuumiza kichwa au kujitoa kwa wananchi au nchi ambayo sio yake au upande usio wake.

Samia angekua Rais wa Zanzibar angehakikisha na kujitoa kwa kila namna wananchi wake wasipate tabu kabisa.

Kusingekua na matatizo kama haya, nahisi hata tozo, makato, kufutwa bima, makodi mizigo, ufisadi, wizi, mikataba ya hovyo kama bandari, mfumuko wa bei nk, asingeruhusu haya kwa raia wake, lakini huku Tanzania anaacha tuisome kwasababu moyo wa utaifa wa Mzanzibar yoyote yule ni Zanzibar na sio Tanganyika au Tanzania kwa ujumla!

Huo ndo ukweli ambao ni ngumu kuumeza! Hakuna mzanzibar anayeweza kuwa na uchungu na Tanganyika hata siku moja yanayofanyika ni "Bora liende au bora yeshe," tu siku ziende tu.

Katiba yetu ni mbovu sana yaani tuna bahati mbaya sana, CCM hawajawahi kuwa wema hata kwa chembe.
 
Tanzania na watanzania ni wamoja ACHA UBAGUZI MKUU!

Urais ni Taasisi na sio Mtu! MUACHE RAIS AFANYE KAZI YAKE.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Tanzania na watanzania ni wamoja ACHA UBAGUZI MKUU!

Urais ni Taasisi na sio Mtu! MUACHE RAIS AFANYE KAZI YAKE.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Ukweli unauma sana wacha muumie tu
 
Back
Top Bottom