Ushawahi kuwaza Samia angekua Rais wa Zanzibar wazanzibari wasingeteseka hivi.
Samia angekua Rais wa Zanzibar, Wanzanzibar wasingeteseka hivi kwasababu mtu ni kwao
Kwa mfumo wetu wa sasa kinachotokea ni sawa na Kagame awe Rais wa Burundi tu kwa kipindi fulani huku akijuwa fika kabisa kuwa mwishoni burundi sio kwake pale anatimiza tu legacy ya kutawala lakini mwisho atamaliza hatamu yake na kurejea Rwanda, kwahiyo hawezi kuumiza kichwa au kujitoa kwa wananchi au nchi ambayo sio yake au upande usio wake.
Samia angekua Rais wa Zanzibar angehakikisha na kujitoa kwa kila namna wananchi wake wasipate tabu kabisa.
Kusingekua na matatizo kama haya, nahisi hata tozo, makato, kufutwa bima, makodi mizigo, ufisadi, wizi, mikataba ya hovyo kama bandari, mfumuko wa bei nk, asingeruhusu haya kwa raia wake, lakini huku Tanzania anaacha tuisome kwasababu moyo wa utaifa wa Mzanzibar yoyote yule ni Zanzibar na sio Tanganyika au Tanzania kwa ujumla!
Huo ndo ukweli ambao ni ngumu kuumeza! Hakuna mzanzibar anayeweza kuwa na uchungu na Tanganyika hata siku moja yanayofanyika ni "Bora liende au bora yeshe," tu siku ziende tu.
Katiba yetu ni mbovu sana yaani tuna bahati mbaya sana, CCM hawajawahi kuwa wema hata kwa chembe.