Bosi TRA anavyoitafuna nchi

Bosi TRA anavyoitafuna nchi

Sheria zetu ni mbovu sana mtu kama huyu ningekuwa Raisi angenyongwa na kufulisiwa mali zake zote na washirika wake wote
 
Kama umemficha bora usingeleta hapa hayo ni majungu sasa..kama una uhakika sema mana kama anaiba hata wewe anakuumiza hela zinapotea na wewe unakosa huduma bora zaidi za afya..barabara na mengineyo mengi..Mtaje hapa hapa tujue....

Na wewe unaeiba hao unaoona wanakuletea hela ujue wanakusema na ujue ukistaafu hizo hela zitaisha hawatapokea simu zako hao sio watu mnashirikiana kuibia nchi kwa muda huu tu..Badaae wanakutupa kama takataka
 
Yaan niwe na Bill 35 mtoto asome st mathew kongowe ??? Shule ambayo ada haifiki 2m kwa mwaka??? Yaan nilijua mtoto wake labda yupo feza huko au shule kubwa kubwa zenye ada milion 15 huko... kingine mtu huwez kuwa na B 35 ukaenda kununua kakiwanja ka m 150 hv unawajua wale wanaowavua watu magorofa hapo kkoo kwa B kadhaa?.. mleta mada hii ni chuki unaleta
 
Walishaambiwa wale kwa urefu wa kamba zao! Sasa huyu bwana kwa vile kamba yake ni ndefu mwache ale bwana!
mtarudi kumkumbuka makufuli kwa upumbavu wenu mnawasikiliza sana chadema sera zao za kumsema makufuli lakini mda sio mrefu mtaimba nyimbo moja woote, kodi zitazidi na bei ya bidhaa zitazidi mtakuwa kama libya lakini nyinyi bila vita
Nani alikuambia wapigaji waliisha nchi hii hata wakati wake kuna baadhi yao walikuwa watandikaaa
Na wee ukipata line pigaaaa

Ova
 
Kwa kweli ila tafuta njia zingine tu za riziki kumbuka kuna wafanya biashara wengi wana hio hela na zaidi ila hawajulikani usitegemee ajira mkuuuu 😎
dah hapo ndio kipengele sasa mkuu
 
Kuna watu wanaitafuna Nchi, Serikali ni sikivu, watu kama hawa hawatufai kwenye jamii yetu

BOSI TRA ANAVYOITAFUNA NCHI
Wakati kashfa ya baadhi ya watumishi wa umma kutajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) haijapoa, Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), (jina naliweka kapuni kwa sasa) 'anaitafuna' nchini!

Taarifa za uhakika zinaeleza Bwana Huyo (nitatumia jina hilo kwa sasa kabla ya kulitaja jina lake kamili hapo baadaye) ambaye ni bosi wa TRA upande wa bandarini, anaitafuna nchi vile anavyojisikia.

"Bwana Huyo anajiandaa kustaafu, kama sio mwaka huu basi mwakani. So (kwahiyo) anachokifanya sasa ni kufuru kaka. Anaiibia nchi bila woga," anasema mtoa taarifa.

Anasema Bwana Huyo ambaye ni baba wa watoto watano, amekuwa akishirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta kuihujumu Serikali katika ukwepaji wa kodi.

"Bwana Huyo anaishi Msasani hizi siku za wikiendi ni jambo la kawaida kuwaona Wafanyabiashara wakija nyumbani kwake na bahasha kubwa kubwa na wakati mwingine wanakuja na maboksi makubwa yenye pesa."

Kwa mujibu wa vyanzo vingine vya habari, vinasema Aprili 17, 2023 Mamlaka za Serikali ambazo bado hazijafahamika zilivamia nyumba yake usiku wa manane na kukuta kiasi kikubwa cha pesa kwenye maboksi.

"Kinachonishangaza na kunistajaabisha baada ya kumkamata usiku uleule aliachiwa na asubuhi akaingia kazini! Waliomvamia waliondoka na boksi 19 za pesa!

"Taarifa ambazo ninazo zinadai wale jamaa waliovamia usiku sina hakika ni TAKUKURU au Polisi, nasikia walikuta pesa nyingi sana. Maana inasemekana alikuwa na Dolla ambazo ukizileta kwenye pesa za Kitanzania inafika bilioni 35," anasema.

Taarifa zaidi zinasema, mtumishi huyo wa umma katika siku za hivi karibuni alinunua nyumba na kiwanja huku pesa ya mali hizo akizitoa nyumbani kwake Msasani.

"Bwana Huyo anaitafuna nchi nielewe. Hivi unaweza kununua nyumba zaidi ya milioni 150 halafu ukaenda ndani kuchukuwa 'cash' na kulipia? Sasa Bwana Huyo, amenunua nyumba Mwananyamala na kiwanja Bagamoyo kwa ajili ya kuweka sheli na pesa zote amelipia cash akitoa ndani kwake!" Anasema mtoa taarifa.

Anasema pamoja na kutoa taarifa kwa Mamlaka za Serikali (TAKUKURU Upanga) lakini anashangaa kuona hakuna hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo nyeti ya Serikali.

"Unajua nchi hii wakati mwingine watumishi walioaminiwa na serikali wanakatisha watu tamaa sana maana nishatoa taarifa Takukuru lakini hadi sasa hakuna lolote limefanyika," anasema.

Bwana Huyo, mwaka jana alimhamisha mtoto wake wa kiume aitwaye (jina kapuni kwa sasa) kutoka katika Shule ya Sekondari Bwawani kwenda St. Methew kwa kile kinachoelezwa "kuficha upigaji wa baba".

Taarifa zinasema mtoto wa Bwana Huyo alikamatwa na uongozi wa Shule ya Sekondari Bwawani akiwa na simu ya gharama aina ya 'iphone' maarufu kama macho matatu.

Taarifa zinasema Nelkoni alipohojiwa na uongozi wa shule alikiri kumwibia pesa baba yake na kununua simu hiyo ambayo gharama yake dukani si chini ya milioni 2. Baada ya taarifa hizo kufika kwa wazazi wa Nelkoni ndio wazo la kumwamisha likaja ili mengi zaidi yasijulikane.

Zipo taarifa zisizo na shaka kwamba baada ya uvamizi wa Aprili 17, Bwana Huyo aliwafuta kazi wafanyakazi wake wawili wa nyumbani.

Maswali ambayo hayajapatiwa majibu ni kuwa kwa nini mamlaka hazijachukua hatua za kumkamata Bwana Huyo? Boksi zilizokamatwa zipo wapi? Kwa nani? Nani yupo nyuma ya Bwana Huyo?

Nitarudi na ushahidi kamili ikiwemo wa nyaraka za ununuzi wa mashamba na nyuma ikiwa ni katika moja ya harakati zake za kutakatisha fedha.
Mbona hiyo ni pesa ya mboga na ni vijsenti tu, huo ni wivu wa kike, nchi hii kuna wapigaji wakuu ndio maana hawa wadogo nao wanafuata nyayo tu, ningekuona wa maana kama ungewafuatilia wale wa ripoti ya Mkaguzi mkuu wa serikali CAG na genge la wahuni aka walamba asali na Don wao!
 
Torra umeandika wivu uliojaa ghilba mtaje huyo kigogo kwa majina kwani unaogopa nini mwehu wewe
 
Taarifa imekaa kimbea mbea. Weka jina na kapicha wazi wazi.
 
Nimeamua kuongeza nyama baada ya kuona hakuna hatua zilizochukuliwa na mamlaka

Afisa huyo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anaitwa Jumbe Donald Magoti,

Magoti ambaye ni baba wa watoto watano wanaojulikana, amekuwa akishirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta kuihujumu serikali katika ukwepaji wa kodi.

Wafanyakazi waliofukuzwa kazi ili bwana huyo alinde siri ya kilichotokea nyumbani ni Kuluthumu na John.

Jumatatu Mei 08, 2023 majira ya saa 5:37 asubuhi kuna wanahabari walimfuata Magoti ofisini kwa nia ya kupata ufafanuzi kuhusu tuhuma zake akaomba mazungumzo hayo yafanyike nje ya ofisi, wakapanga wakutane Jack's Pub iliyopo Masaki jijini Dar saa 12 jioni.

Magoti hakutokea sehemu husika! Baada ya kupigiwa simu akawasili saa 1:42 usiku eneo la Masaki katika Bar nyingine na si ile aliyopendekeza awali!

Kabla ya kuanza mazungumzo Magoti akawataka Waaandishi kutaja jina la mtu aliyeleta habari ndio atoe majibu ya maswali atakayoulizwa, akajulishwa kuwa hilo halitawezekana, hivyo mazungumzo yakafa hapohapo.

Afisa mmoja wa mamlaka ya rushwa wa Ilala alisema analijua sakata hilo licha ya kuwa si eneo lake la kazi na kudai kuwa "Sasa suala likishafika Makao Makuu sisi huku wa ngazi ya Mkoa hatuna Mamlaka ya kulizingunzia.”

Upande wa mamlaka ya Kinondoni walisema hawana taarifa juu ya suala hilo

NAIBU DCI HUYU HAPA
Baada ya kukosa majibu ya uhakika Takukuru Ilala na Kinondoni, tulimtafuta DCP (Naibu DCI), Salehe Ambika, ambaye hakuwa na taarifa zozote kuhusu jambo hili.

Alikazimika kuwasiliana kwa njia ya simu ZCO Dar es Salaam ili kujua kama anataarifa zozote. Baada ya mazungumzo yao yaliyochukuwa takribani dakika 7 alisema suala hilo liliripotiwa Takukuru na si polisi.

"Hata hivyo mtu huyo mnaesema (Magoti) hakuwa na kiasi kikubwa mlichoambiwa. Alikuwa na milioni 40 pesa za kitanzania na Dolla 2. Pesa hizo inadaiwa alitumiwa na dada yake anaeishi nchi Ufaransa," alisema.

Akaongeza, "Kwahiyo kama mnataka kujua zaidi nendeni Takukuru ambako suala hili ndipo liliripotiwa kwa mara ya kwanza."

TAKUKURU MAKAO MAKUU
Tulikazimika kurudi tena Takukuru lakini safari hii Makao Makuu, Dodoma.

Msemaji wa taasisi hiyo nyeti ya serikali, Doreen Kapwani, alipoulizwa kama kuna taarifa kama hizo kama tulivyoelezwa na Mkuu wa Takukuru Ilala, kwa kifupi alisema, "Hatuna taarifa hii."
 
Imagine kila mtu aingie alaf apambanie uzao wake waibe mpaka wasaze naamini zitakua ni familia chache Tu swali ni vipi hizi familia zaidi ya million 40 ambazo familia zao hazijapata nafasi hio ya kuiba ziendelee kuishi kwenye Lindi la umasikini kwasababu ya hizo familia chache ??
Daaah alaf ukishaiba ww na uzao wako wote then what next vipi ukienda kuulizwa na mungu kuhusu familia zaidi ya millioni 40 ulizoziibia utajibu nn
Kwann tunahamisishana maovu kwann tunahamisishana wizi daah unajua hii ndio itakua Tabia yetu tusipoangalia
Wabongo wengi sio kwamba wanachukia ufisadi. Kinachowakera ni wao kuwa nje ya mfumo wa upigaji. Soma comments nyingi hapa utagundua kitu.
 
mtarudi kumkumbuka makufuli kwa upumbavu wenu mnawasikiliza sana chadema sera zao za kumsema makufuli lakini mda sio mrefu mtaimba nyimbo moja woote, kodi zitazidi na bei ya bidhaa zitazidi mtakuwa kama libya lakini nyinyi bila vita
Chadema wanataka kwenda kuhiji chato…. Agenda zao ni kama lawalawa
 
Hata hivyo mtu huyo mnaesema (Magoti) hakuwa na kiasi kikubwa mlichoambiwa. Alikuwa na milioni 40 pesa za kitanzania na Dolla 2. Pesa hizo inadaiwa alitumiwa na dada yake anaeishi nchi Ufaransa," alisema.
 
Nchi inafunwa harafu wanatokea wajanja wachache wanaongeza Tozo kwenye Umeme badala ya kudhibiti wizi na matumizi mabovu wao wanaongeza mapato ili waited zaidi...
 
Bro mwisho wa siku what matters ni ww na uzao wako mkuuu

Kuna mtu x mwaka y alikuwa kitengo z

Kwa miaka A alichota bil E akastaafu mwaka q yuko canada na wanae ana five star hotel 3 humo nchini right now

Hivyo kila mtu apambanie uzao wake mkuuuuu
Find the value of X
 
Kwa mantiki hiyo, Mtanzania anakuwa hana tofauti na wanyama au hayawani wa porini. Pona ya digidigi ni kushiba kwa Simba. Na watoto wa Chui wanaweza uwa mtoto wa swala kwa kujifunzia kuwinda. Tumia muda kidogo tu kuangalia Tv channel za wanyama na uone maisha ya mwituni.
Ndivyo unavyotaka binaadamu wa miongo ya leo aishi!!!?
Sisi ni Binaadamu. Ni bora kuliko hayawani na wengine wote.
Kaa chini ufikirie vizuri.

Wakatabahu
Infopaedia

Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanaitafuna Nchi, Serikali ni sikivu, watu kama hawa hawatufai kwenye jamii yetu

BOSI TRA ANAVYOITAFUNA NCHI
Wakati kashfa ya baadhi ya watumishi wa umma kutajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) haijapoa, Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), (jina naliweka kapuni kwa sasa) 'anaitafuna' nchini!

Taarifa za uhakika zinaeleza Bwana Huyo (nitatumia jina hilo kwa sasa kabla ya kulitaja jina lake kamili hapo baadaye) ambaye ni bosi wa TRA upande wa bandarini, anaitafuna nchi vile anavyojisikia.

"Bwana Huyo anajiandaa kustaafu, kama sio mwaka huu basi mwakani. So (kwahiyo) anachokifanya sasa ni kufuru kaka. Anaiibia nchi bila woga," anasema mtoa taarifa.

Anasema Bwana Huyo ambaye ni baba wa watoto watano, amekuwa akishirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta kuihujumu Serikali katika ukwepaji wa kodi.

"Bwana Huyo anaishi Msasani hizi siku za wikiendi ni jambo la kawaida kuwaona Wafanyabiashara wakija nyumbani kwake na bahasha kubwa kubwa na wakati mwingine wanakuja na maboksi makubwa yenye pesa."

Kwa mujibu wa vyanzo vingine vya habari, vinasema Aprili 17, 2023 Mamlaka za Serikali ambazo bado hazijafahamika zilivamia nyumba yake usiku wa manane na kukuta kiasi kikubwa cha pesa kwenye maboksi.

"Kinachonishangaza na kunistajaabisha baada ya kumkamata usiku uleule aliachiwa na asubuhi akaingia kazini! Waliomvamia waliondoka na boksi 19 za pesa!

"Taarifa ambazo ninazo zinadai wale jamaa waliovamia usiku sina hakika ni TAKUKURU au Polisi, nasikia walikuta pesa nyingi sana. Maana inasemekana alikuwa na Dolla ambazo ukizileta kwenye pesa za Kitanzania inafika bilioni 35," anasema.

Taarifa zaidi zinasema, mtumishi huyo wa umma katika siku za hivi karibuni alinunua nyumba na kiwanja huku pesa ya mali hizo akizitoa nyumbani kwake Msasani.

"Bwana Huyo anaitafuna nchi nielewe. Hivi unaweza kununua nyumba zaidi ya milioni 150 halafu ukaenda ndani kuchukuwa 'cash' na kulipia? Sasa Bwana Huyo, amenunua nyumba Mwananyamala na kiwanja Bagamoyo kwa ajili ya kuweka sheli na pesa zote amelipia cash akitoa ndani kwake!" Anasema mtoa taarifa.

Anasema pamoja na kutoa taarifa kwa Mamlaka za Serikali (TAKUKURU Upanga) lakini anashangaa kuona hakuna hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo nyeti ya Serikali.

"Unajua nchi hii wakati mwingine watumishi walioaminiwa na serikali wanakatisha watu tamaa sana maana nishatoa taarifa Takukuru lakini hadi sasa hakuna lolote limefanyika," anasema.

Bwana Huyo, mwaka jana alimhamisha mtoto wake wa kiume aitwaye (jina kapuni kwa sasa) kutoka katika Shule ya Sekondari Bwawani kwenda St. Methew kwa kile kinachoelezwa "kuficha upigaji wa baba".

Taarifa zinasema mtoto wa Bwana Huyo alikamatwa na uongozi wa Shule ya Sekondari Bwawani akiwa na simu ya gharama aina ya 'iphone' maarufu kama macho matatu.

Taarifa zinasema Nelkoni alipohojiwa na uongozi wa shule alikiri kumwibia pesa baba yake na kununua simu hiyo ambayo gharama yake dukani si chini ya milioni 2. Baada ya taarifa hizo kufika kwa wazazi wa Nelkoni ndio wazo la kumwamisha likaja ili mengi zaidi yasijulikane.

Zipo taarifa zisizo na shaka kwamba baada ya uvamizi wa Aprili 17, Bwana Huyo aliwafuta kazi wafanyakazi wake wawili wa nyumbani ili wasije wakavujisha kile ambacho kimefanyika.

UTATA UKO WAPI?
1. Idara gani ya serikali ilimkamata Bwana huyo usiku wa April 17, 2023?
2. Kwanini kulikuwa na uchelewi tangu taarifa ziripotiwe Takukuru?
3. Kwanini alikamatwa usiku na kuachiwa usiku huohuo?
4. Kwanini Takukuru na Polisi hawajui lolote kuhusu sakata hili?
5. Nani yupo nyuma ya Bwana huyo ambaye jina lake la kwanza linaanza na J huku jina lake la mwisho likianza na M?

Nitarudi na ushahidi kamili ikiwemo wa nyaraka za ununuzi wa mashamba na nyuma ikiwa ni katika moja ya harakati zake za kutakatisha fedha.
Mama, mama , mama. Mara mpeni maua yake.
Nchi inaisha tukiiabudu CCM!!
 
Back
Top Bottom