BoT: Kipato cha kila mkazi wa Dar chaongezeka kwa shilingi Laki 5, wa mikoani kwa Laki 1

Hii ndio Taarifa Mpya kutoka BOT , kwamba watu wa Dar wameongeza utajiri wao kwa 12% kutoka mil 4.8 mwaka uliopita hadi mil 5 mwaka huu .

View attachment 2778872

Toa maoni yako .
Zangu nadhani zitakuwa zimeibiwa au wamenisahau kunipa. Au pengine kuna mtu atakuwa amenichukulia! Ngoja niweke kwenye Status kuuliza aliyenichukulia mil 5 zangu aniletee tafadhali
 
Zangu nadhani zitakuwa zimeibiwa au wamenisahau kunipa. Au pengine kuna mtuatakuwa amenichukulia! Ngoja niweke kwenye Sytus kuuliza aliyenichukulia mil 5 zangu aniletee tafadhali
😆😆😆😆
 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na BoT kwenye ripoti yake ya Consolidated Report ya mwaka 2022 inaonesha Pato la Kila Mkazi wa Dar limeongezeka Kwa Shilingi Laki 5 wakati wastani wa Pato la Kila Mtanzania likiongezeka kutoka sh.2.7 mln Hadi sh 2.8 mln (Laki Moja) Kwa mwaka 2022.

My Take: Kila mtu aangalie account yake na mapato yake kama yameongezeka au hapana 😁😁

=====

Kipato cha kila mkazi wa Dar chaongezeka kwa laki 5 - SwahiliTimes​

Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha ongezeko la asilimia 5 katika wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka ambao umechagiwa na na kukua kwa uchumi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa.

Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa kipato cha Mtanzania (GDP per Capita) cha mmoja mmoja kimeongezeka zaidi kutoka wastani wa TZS milioni 2.7 hadi Shilingi milioni 2.8.

Wastani wa kipato cha wakazi wa Dar es Salaam kimeongezeka zaidi kuliko maeneo megine nchini kutoka Shilingi milioni 4.81 hadi shilingi milioni 5.39 kwa mwaka 2022 sawa na ukuaji wa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo kila mkazi wa Dar es Salaam aliongeza TZS 500,000 katika mapato yake ya mwaka .

Hata hivyo, hesabu ya pato la mtu mmoja mmoja inapatikana kwa kugawa pato la Taifa au eneo fulani (GDP) kwa idadi ya watu waishio humo.

Shirikia la Fedha Duniani (IMF) linasema GDP hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa katika kipindi husika na pia si zote ambazo zinajumuishwa.
Yule mtu Cuba alishawahi waambia. Ninyi ni wahuni
 
Kama kwako hakijaongezeka usilazimishe na Kwa wengine.Mfano mdogo maelfu ya Ajira zilizotolewa ni sehemu ya figures ya hiyo ripoti.
Kutoka na kichwa Cha Uzi unajumuisha watanzania wote mkuu

Alafu ukisema maelfu ya ajira je ni watanziq wote tumepata hizo ajira..!?

Labda ungesemq "kipato Cha walioajiriwa chaongezeka kwa kiasi Fulani"
 
Kwani kwako maelfu yanaanzia ngapi? Maelfu ni sawa na wote? Unaweza nitajia Nchi ambayo wote Wana Ajira?
 
Wanangu wa mikoani mmegundua Nini kuhusu daslam kutokana na Uzi huu...!?
Sasa kama Serikali inawekeza Kila kitu Dar unategemea nini? Kiufupi maisha Yako Dar.

Nimewahi Shusha Uzi kulaumu hii tabia ya serikali kuwekeza Kila kitu Dar.

Unakuta mambo ya Kilimo miundombinu Iko Dar wakati tunatia jasho sie ,nimeandika nyuzi nyingi sana kupinga hii tabia ya kuchukua pesa zetu mikoani na kujenga Dar.
 
Mimi binafsi kipato kimeongezeka baada ya Kumaliza Bodi ya Mikopo na kulipwa arears Sasa hapo Kwa nini nisiseme figures ziko sahihi? Japo kimeongezeka Kwa figures za mkoani.sio za Dar.
 
Attachments

  • E6CC552B-BF58-488F-9E89-12065CC0AA34.jpeg
    E6CC552B-BF58-488F-9E89-12065CC0AA34.jpeg
    68.7 KB · Views: 1
Sasa kama Serikali inawekeza Kila kitu Dar unategemea nini? Kiufupi maisha Yako Dar.

Nimewahi Shusha Uzi kulaumu hii tabia ya serikali kuwekeza Kila kitu Dar.

Unakuta mambo ya Kilimo miundombinu Iko Dar wakati tunatia jasho sie ,nimeandika nyuzi nyingi sana kupinga hii tabia ya kuchukua pesa zetu mikoani na kujenga Dar.
Au wanataka wote twende dar...

Sawa Kama wameamua kuwekeza dar Kila kitu Ila kwann watujumlishe na sisi kwenye ujinga wao...!?

Yaani hii nchi ni ngumu mkuu imagine pamoja na serikali kuhamia dodoma Ila bado Kila kitu ni dar as if sisi wa mkoani ni mifugo.
 
Mbaya sana hiyo ,soma huu Uzi
 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na BoT kwenye ripoti yake ya Consolidated Report ya mwaka 2022 inaonesha Pato la Kila Mkazi wa Dar limeongezeka Kwa Shilingi Laki 5 wakati wastani wa Pato la Kila Mtanzania likiongezeka kutoka sh.2.7 mln Hadi sh 2.8 mln (Laki Moja) Kwa mwaka 2022.

My Take: Kila mtu aangalie account yake na mapato yake kama yameongezeka au hapana 😁😁

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1712122817989185938?t=tqREV3t-EiJZXfFQV3k8xg&s=19

=====

Kipato cha kila mkazi wa Dar chaongezeka kwa laki 5 - SwahiliTimes​

Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha ongezeko la asilimia 5 katika wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka ambao umechagiwa na na kukua kwa uchumi wa Kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa.

Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa kipato cha Mtanzania (GDP per Capita) cha mmoja mmoja kimeongezeka zaidi kutoka wastani wa TZS milioni 2.7 hadi Shilingi milioni 2.8.

Wastani wa kipato cha wakazi wa Dar es Salaam kimeongezeka zaidi kuliko maeneo megine nchini kutoka Shilingi milioni 4.81 hadi shilingi milioni 5.39 kwa mwaka 2022 sawa na ukuaji wa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo kila mkazi wa Dar es Salaam aliongeza TZS 500,000 katika mapato yake ya mwaka .

Hata hivyo, hesabu ya pato la mtu mmoja mmoja inapatikana kwa kugawa pato la Taifa au eneo fulani (GDP) kwa idadi ya watu waishio humo.

Shirikia la Fedha Duniani (IMF) linasema GDP hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa katika kipindi husika na pia si zote ambazo zinajumuishwa.

BOT ni Kenge..walete dola kwanza
 
Back
Top Bottom