BoT: Kukopesha fedha bila leseni faini Tsh. Milioni 20, jela miaka 2

BoT: Kukopesha fedha bila leseni faini Tsh. Milioni 20, jela miaka 2

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa onyo kwa wananchi kuepuka kukopa au kufanya Biashara na Taasisi, Kampuni, Mtu au Watu Binafsi ambao hawana leseni.

Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 imezuia na kukataza biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na vibali maalumu.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (2) (a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, adhabu ya ukiukaji wa Sheria hii ni faini isiyopungua Tsh. Milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka miwili.

====================

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu/watu binafsi ambao hawana leseni.

Hiyo ni baada ya kubaini kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

"Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa leo Alhamisi, Novemba 24, 2022 na Gavana wa BoT.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili.

Kufuatia hilo, BoT imewaasa wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni. "Orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz,” imeeleza

MWANANCHI
 
Kwa hiyo huyu Jirani yangu aliyekuwa kuniomba nimkopeshe 100,000 ili asafiri kwenda mbaya kumzika baba yake, nisimpe tena?
Uyo Ni Kama unamuazima tu,ingekua unamwambia hiyo laki akirudisha iwe laki na 30 ndio sio ruhusa Kama hauna leseni
 
Loan sharks wa Tanzania wapo hatua mia mbili zaidi ya Sheria zenu BOT kuanzia kushikiria kadi za benki za wakopaji hadi kuandikishana kuwa wameuziana mpunga au mbuzi na wakopaji! Ila jamani nguvu mnazotumia kuweka Sheria kwanini nguvu hizo hizo zisitumike kutafuta chanzo hasa cha kuibika utitili wa wakopeshaji bubu?...ngoja niwape mfano hai wa jinsi benki zetu hapa nchini wanavyofanya kazi kwa mazoea!

Kuna benki moja kubwa tu hapa nchini kijana wangu alienda kukopa mkopo wa kununua pikipiki ya miguu mitatu ya kubeba abiria maarufu kama Bajaj. Wakamwambia una leseni ya biashara, uzoefu, nk kijana ni mzoefu pia leseni anayo na anayo bajaji nyingine ila imezeeka. Akaambiwa aweke kiasi cha pesa nadhani alimbiwa milioni mbili na nusu, yote kijana akafanya...likaja suala la mdhamini akaambiwa mdhamini awe baba yake au mama na awe na nyumba yenye hati au mdhamini awe ni mtumishi wa serikali ila eneo lake la kazi yaani mwajiri wake awe ndani ya eneo inapohudumia benki. Kijana akafanikiwa kumpata mdhamini ambaye ni mtumishi wa serikali. Benki waksema pia ni lazima mshahara wa huyo mtumishi upitie hapo benki.

Yaani pamoja na kadi za chombo kubaki benki, mkopaji kutanguliza milioni mbili na nusu, kukatiwa bima kubwa chombo atakachokopa, mdhamini kupotisha mshahara wake benki hiyo, bado afisa mikopo yupo alionekana kumzungusha huyo kijana na mwisho kijana akakata tamaa na kwenda kwa wakopeshaji feki ambao BOT inawawekea Sheria Kali!
 
Tutakopeshana sana huku huku mitaani!! Japo hawa loan sharks wanapiga riba kubwa sana na pia wanahatarisha Mali za wakopaji,sababu ni kuwa hizo taasisi rasmi kama Bank si rafiki kabisa na watu ambao ndiyo hasa wenye sifa za kukopa,wao wame base kuwakopesha waalimu na manesi na mapolisi ambao tayari wana ajira zenye mishahara ya uhakika,ila mimi muuza mchele sokoni nikiwaomba wanipe mkopo wa 1m ninunue gunia kadhaa nirushe hapo nchi jirani wanaleta urasimu wa ajabu kabisa,yaani hadi upate mkopo wa 1m utajikuta umetumia ½ ya mkopo tayari
 
Loan sharks wa Tanzania wapo hatua mia mbili zaidi ya Sheria zenu BOT kuanzia kushikiria kadi za benki za wakopaji hadi kuandikishana kuwa wameuziana mpunga au mbuzi na wakopaji! Ila jamani nguvu mnazotumia kuweka Sheria kwanini nguvu hizo hizo zisitumike kutafuta chanzo hasa cha kuibika utitili wa wakopeshaji bubu?...ngoja niwape mfano hai wa jinsi benki zetu hapa nchini wanavyofanya kazi kwa mazoea!

Kuna benki moja kubwa tu hapa nchini kijana wangu alienda kukopa mkopo wa kununua pikipiki ya miguu mitatu ya kubeba abiria maarufu kama Bajaj. Wakamwambia una leseni ya biashara, uzoefu, nk kijana ni mzoefu pia leseni anayo na anayo bajaji nyingine ila imezeeka. Akaambiwa aweke kiasi cha pesa nadhani alimbiwa milioni mbili na nusu, yote kijana akafanya...likaja suala la mdhamini akaambiwa mdhamini awe baba yake au mama na awe na nyumba yenye hati au mdhamini awe ni mtumishi wa serikali ila eneo lake la kazi yaani mwajiri wake awe ndani ya eneo inapohudumia benki. Kijana akafanikiwa kumpata mdhamini ambaye ni mtumishi wa serikali. Benki waksema pia ni lazima mshahara wa huyo mtumishi upitie hapo benki.

Yaani pamoja na kadi za chombo kubaki benki, mkopaji kutanguliza milioni mbili na nusu, kukatiwa bima kubwa chombo atakachokopa, mdhamini kupotisha mshahara wake benki hiyo, bado afisa mikopo yupo alionekana kumzungusha huyo kijana na mwisho kijana akakata tamaa na kwenda kwa wakopeshaji feki ambao BOT inawawekea Sheria Kali!
Hawa hawakuwa na lengo la kumkopesha
 
Hiyo adhabu ilikuwepo ama ndio imeanza mwaka huu, maana kama ni watu kukopesha bila leseni mtaani wapo kibao.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo huyu Jirani yangu aliyekuwa kuniomba nimkopeshe 100,000 ili asafiri kwenda mbaya kumzika baba yake, nisimpe tena?
Kukopesha kunakozungumziwa ni ile kukopesha kibiashara ambayo ina mpaka riba.
 
Hii mikopo ilitutesa sana kipind tuko chuo jamaa walikua hawana huruma ana card yako ya bank boom likiingia ni vita
 
Back
Top Bottom