Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,613
- 8,082
Inashangaza sana. Yaani kila kitu wanajua kuliko wengine. Corona imeanza china. Wenyewe wakasema tumejipanga vya kutosha wala hatuna wasiwasi,hata mipaka haikufungwa kama mataifa makubwa yalivyofanya. Cha cha ajabu hata vipimo tu vya airpot vya kubabaisha. Watu wanapita wanapimwa wanaingia na virus. Mwingine mmoja akasema hivyo virus vinaisha vyenyewe ndani ya siku 7. Yaani wanakijua zaidi ya kilikotokea. Huko juu wamesema pesa za noti yaani pamoja na dola na paund za noti zinachangia kueneza huu ugonjwa. Lakini hapa kwetu mtu anakuja anasema noti zetu zimejipanga kukabiriana na huu ugonjwa, hazienezi, zina dawa[emoji23][emoji23][emoji23] yaani sisi tuko juu. Tuko vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app