BoT: Pesa ya Tanzania haiwezi kusambaza Virusi vya Corona. Zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti

BoT: Pesa ya Tanzania haiwezi kusambaza Virusi vya Corona. Zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti

[emoji23][emoji23][emoji23] yaani sisi tuko juu. Tuko vizuri.
Inashangaza sana. Yaani kila kitu wanajua kuliko wengine. Corona imeanza china. Wenyewe wakasema tumejipanga vya kutosha wala hatuna wasiwasi,hata mipaka haikufungwa kama mataifa makubwa yalivyofanya. Cha cha ajabu hata vipimo tu vya airpot vya kubabaisha. Watu wanapita wanapimwa wanaingia na virus. Mwingine mmoja akasema hivyo virus vinaisha vyenyewe ndani ya siku 7. Yaani wanakijua zaidi ya kilikotokea. Huko juu wamesema pesa za noti yaani pamoja na dola na paund za noti zinachangia kueneza huu ugonjwa. Lakini hapa kwetu mtu anakuja anasema noti zetu zimejipanga kukabiriana na huu ugonjwa, hazienezi, zina dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu barua inasema simply tu "noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti " ambayo ni moja ya basic specification ya utengenezwaji wa noti. Hamna sehemu barua imesema pesa ya Tanzania haiwezi kusambaza Corona. Tafsiri yako sio sahihi mkuu
 
Kenya Benki kuu yao imetangaza kuweka karantini kwa siku 7 fedha taslimu ( cash) zitakazopokelewa na mabenki nchini humo!

Nadhani noti zetu ni za kisasa zaidi!

Kwa sasa wafuatiliaji wa mambo tunajua serikali serikali hii hutoa taarifa nyingi za uongo, hivyo hata hii ni uongo kama uongo mwingine.
 
Kweli Magufuli kiboko anaogopwa na kila mtu; adi mkuu wa mkoa wa Arusha alimwamuru mgonjwa kuwaomba msamaha watanzania kwa hofu ya kuogopa mh Rais.
Poleni watanzania
 
matamko tuuu, no action

Katika Kipindi hiki kigumu cha COVID-19, Serikali ulimwenguni zinasaidia wananchi wake. Tanzania kuna wananchi wanyonge na masikini wengi, hawana akiba ya fedha, kwa sababu ya udogo wa kipato.

Mfano, Sekta ya Utalii imepata pigo kubwa, wafanyakazi kupewa likizo bila malipo. Pia kukosekana mapato katika tourism, agriculture consumers imedrop mno, Kilimo kimeathirika, wakulima wameathirika kimapato.

Ni vigumu kugawa pesa kama USA, Serikali ifanye Subsdize katika huduma muhimu kama Unga, Mafuta kupikia, Gesi ya kupikia, Umeme. Serikali ipunguze kodi katika hizi bidhaa ili zipungue bei na wanyonge wasiteseke. Kuna PESA za Mwenge na pesa za maafa ..ziende huko.

Serikali iongee na Bakresa na Mo, na wazalishaji wengine, ili Wapunguze bei za unga na Mafuta, then Serikali ifidie. Na Wasambazaji wa gesi za majumbani, serikali iongee nao, gesi ipungue bei...Pili itaokoa mazingira na kufuta matumizi ya mkaa.

Wabunge wote, na wanaharakati, muishauri serikali.
 
View attachment 1392836
Benki Kuu ya Tanzania imesema noti za Tanzania zimetengenezwa kwa namna ambayo haziwezi kuhifadhi virusi.
Kama ina nguvu kiasi hicho cha kuzuia vimelea (Nadhani wanaongelea virus) wasikae kwenye noti basi ingekuwa vyema watumie hiyo materials ili itumike kama kinga ya kuzuia hao wadudu. Inaweza kuwa breakthrough kwenye kupata kinga na tiba kamili. Sasa wanatoa tahadhari ya nini tena? Kweli nalilia taifa langu....Limekosa maarifa au tupo kwenye hatua kubwa sana ya technology?
 
BOT wabadirike, kuna mifumo kama Paypal tunashindwa kuitumia kupokea pesa. Waende na wakati.
 
Aisee kuna uwezekano huo. Zile drama za jana za kumpigia simu live halafu akaanza blah blah za kuomba msamaha na kuishukuru serikali ya rais nani sijui...Nikajua hapa mh..maigizo mengine haya. Ikumbukwe ni kinyume cha maadili kuanika hadharani jina la mgonjwa na ugonjwa anaogua.
Haya yote ni maigizo..Anaomba msamaha wa nini? Anaishukuru serikali kwa kazi gani? hiyo ni purely staging.
 
Benki Kuu ya Tanzania imesema noti za Tanzania zimetengenezwa kwa namna ambayo haziwezi kuhifadhi virusi.
Moja kwa moja, hili lingetoa machapisho (papers) kadhaa kwa wenye taaluma katika eneo hilo.

Ni fursa ya kipekee kwa watafiti; kwa sababu hao hao Benki Kuu ndio wangeombwa fedha za kuendeshea utafiti huo.

Haitoshi kabisa kwa Benki Kuu kudai tu kuwa noti zao hazishiki vimelea.

Inatakiwa uthibitisho wa hilo kwa kufanya utafiti juu yake.

Coronavirus ni 'novel' (mpya), walijuaje kwamba noti zao haziwezi kumkamata. Kama hazikamati wengine, haina maana na yeye hakamatiki.

Hata hivyo wamefanya vizuri kutahadharisha zaidi juu ya jambo hilo.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mbavu zangu jamani sijawahi kuona serikali inayodanganya raia wake kama hii Hahahahahhahahahahhahahaaaaaiiiii Toba!
Mpaka unapata hasira. Hii nchi kila kitu inajua, mpaka aibu sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Aisee hiyo pesa yetu ina antivirus ehe!


BOT wanaamini kabisa kuwa watanzania ni mapopoma lakini kumbe na watanzania nao wanaziangalia data za BOT kwa kutumia Iceberg principles na wanakubaliana na data zao...sijui mshindi hapo ni nani though mie binafsi nafikiri BOT wameshinda kwa kuweka antivirus kwenye noti zao
 
Nadhani hao BOT wana akili fulani hivi za kiuwendawazimu. Wanaropoka tu.

Yaani wanasema Pesa za Tanzania zimetengenezwa kwa namna ambayo Corona haiwezi kukaa (Sijui walijua Corona itatokea duniani?) halafu hapo hapo wanasema wananchi tutumie njia ya mtandao kufanya manunuzi kuliko noti ili kuepuka kupata Corona kupitia kushika noti!!!
 
Ndio utajua hata idadi ya wagonjwa sio halisi ile idadi ya jana ukizidsha kwa 20 ndio utapata idadi halisi ya wagonjwa
Nchi hii wanakufa watu ovyo kila siku kwa mamia hakuna chochote kinachotokea. Leo hata wakifa elfu hawasemi....wanaficha ficha tu. Ndiyo maana tulipigwa stop ya kucheza hata green card. Serikali hii ya waongo na watesaji.
 
Back
Top Bottom