BoT, toeni matangazo kupitia vyombo vya habari kukumbusha kuwa kufanya biashara ya kukopesha mitaani bila leseni ni kosa la jinai

BoT, toeni matangazo kupitia vyombo vya habari kukumbusha kuwa kufanya biashara ya kukopesha mitaani bila leseni ni kosa la jinai

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Nchi hii kuna sheria ambazo hutungwa halafu huwa zipo tu kwenye makaratasi na mojawapo inaweza kuwa ni Microfinanc ACT ya Mwaka 2018 na kanuni zake.

Sheria hii, pamoja na mambo mengine, inapiga marufuku watu kufanya biashara ya kukopesha bila kusajaliwa na kuwa na leseni na inatoa adhabu kali kwa wanaovunja hii sheria.

Hata hivyo, kinachoendelea mitaani ni kama vile hii sheria haipo, na watu wanafanya hii biashara kiholela baadhi kwa kutoza riba kubwa tena kwa kunyanyasa wakopojaji wakati wao hata kodi hawalpi na hata leseni hawana.

Hata kwa walio na leseni na ni tatizo kwanini mtu akikwama, basi mkopaji hutamani hata kukimbia nyumbani au eneo lake la biashara kuogopa fedheha ya kudhalilishwa au kudaiwa mbele za watu.

Ni kweli wakopojaji wanapaswa kulipa, ila mtu anapokwama, sheria inamlinda dhidi ya unyanyasaji au uzalilishaji na hata mikataba wanayotoa inapaswa kuzingatia sheria na kanuni zake.

Hivyo, nashauri BoT watoe matangazo kwenye vyombo vya habar kukumbusha kuwa ni kosa la jinai kufanya hii biashaara kama hujasajiliwa na huna leseni.

Pia, wenye leseni wazingatie mashariti ya leseni zao ikiwa ni pamoja na kutoa mikataba na kutonyanyasa wateja wao.

Halikadhalika, wakopojaji nao wakumbushwe kuwa wana wajibu wa kulipa madeni yao kukingana wa mikataba yao.

Kilichonisukuma kuandika haya ni hii mikopo ambayo marejesho yake ni ya kila siku bila kujali mtu siku hiyo umeuza au hujauza na umepata faida au hujapata ila rejesho ni lazima.

Wahanga wakubwa huku mitaani ni kina Mama ambao unaweza hata kuwaonea huruma wanapohangaika na haya marejesho ya kila siku.

Mwisho, nashauri serikali kupitia BOT, ikiwezekana wapige marufuku marejesho ya kila siku na iwe ni option ya mteja kutaka kurejesha kila siku.

Siamini kama kuna biashaara ya kutengeneza faida kila siku ya Mungu na hata kama ipo, Siamini kama kila siku hutopata dharau ukashindwa kufanya biashaara mfano kuugua au kuguliwa, n.k.

BoT chukueni hatua kunusura watu hasa kina Mama ambao wengi wao mitaji yao ni midogo. Ikiwezekana, pia mje na utaratibu sheria au kanuni kudhibiti riba kwenye hii biashaara ambayo kwa kiasi kikubwa inafanywa kiholela na wahusika hata kodi hawalipi.
 
Na pia iwakumbushe wananchi wasome mikataba kabla ya kukopa. Mkataba umeandikwa marejesho ni kila siku, umesaini, umechukua pesa za watu, umezitumia kwa namna iliyokupendeza halafu unataka Serikali ije isadie kuzuia kupeleka marejesho kila siku. UPUUZI.
 
Na pia iwakumbushe wananchi wasome mikataba kabla ya kukopa. Mkataba umeandikwa marejesho ni kila siku, umesaini, umechukua pesa za watu, umezitumia kwa namna iliyokupendeza halafu unataka serikali ije isadie kuzui kupeleka marejesho kila siku. UPUUZI.
Msitumie shida za watu kujinufaisha.
 
hutamani hata kukimbia nyumbani au eneo lake la biashaara kuogopa fedheha ya kuzalilishwa au kudaiwa mbele za watu.
Pamoja na yote mazuri uliyoeleza ila hakuna mkopo usiokuwa na vigezo na masharti yake.

Ukikopa ina maana umekubaliana na vurumai zake. Dawa ya deni ni kulipa. Kama hutaki hizi aibu basi lipa kwa wakati au usikope.
 
Pamoja na yote mazuri uliyoeleza ila hakuna mkopo usiokuwa na taratibu na sheria zake.
Ukikopa ina maana umekubaliana na vurumai zake.
Dawa ya deni ni kulipa.
Kama hutaki hizi aibu basi usikope.
Hawa ambao hawana leseni hawatoa mikataba kwasababu wanajua itakula kwao.
 
Namtetea Shangai yako na Mama yako kule kijijini Namtumbo na dada yako aleko mjini
Wakopaji wengine matapeli tu. Hivi unajua sekta ya microfinance inapopita? Bila ujanja na kuwa aggresive mfanyabiashara anafilisika, Kanuni zinataka usikopeshe juu ya riba 3.5% pm reducing method. Yaaani ukimkopesha mtu laki, arudishe laki na elfu tatu mia tano. Hiyo faida hata ukinyanyua simu kukumbusha imeishia kwenye vocha, bado marejesho hawapati kwa wakati, bado kodi, bado mishahara, bado mikopo chefuchefu. Waoneeni huruma.
 
Sasa mkuu unataka wanaokopesha ndo waache kukopesha kwa kuwa hawana leseni au wanaokopa wasikope kwa wasio na leseni, maana hapo ni sawa na mtu anaetaka kuzuia biashara ya kuuza mwili aende akawadhibiti wauzaji badala ya wanunuzi, Mwenye shida siku zote ndo wa kuzuiliwa na sio mtatuzi... kwani hao wamama hawazioni bank, kwanini wasiende kukopa huko kama wanataka sheria za kuwalinda?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Msitumie shida za watu kujinufaisha.
Hakuna mtu atakusaidia tu sababu wewe ni mtu, ukipata shida ni fursa kwa mwingine.

Daktari anataka uumwe ndo anufaike, mwanasheria anataka upate kesi anufaike, muuza majeneza anataka mfe kwa wingi, wanaotengeneza ARV wanataka mpate hiv, wenye mabaa wanataka muwe walevi, mwalimu anatamani usielewe haraka ili akufundishe masomo ya ziada kwa gharama za ziada n.k.
 
Back
Top Bottom