McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni zinazoeleza kuwa benki za biashara nchini zimepata au zinatarajiwa kupata shambulio la kimtandao litakalosababisha upotevu wa fedha za wateja na kusababisha hitilafu katika mifumo ya kibenki.
Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa na Gavana Emmanuel Tutuba siku ya Jumamosi Novemba 22, 2025, BoT imesema taarifa hizo ni za upotoshaji na zimekusudiwa kuwatia hofu wananchi ili kuwahamasisha kutoa fedha kutoka kwenye akaunti zao.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, mifumo ya malipo ya Taifa inaendelea kufanya kazi kwa usalama na ufanisi, na amana za wateja katika benki zote za biashara zipo katika uangalizi wa karibu na wa kitaalamu. Benki Kuu imewahakikishia wananchi kuwa hakuna shambulio lolote la kimtandao lililotokea katika benki nchini, na kwamba taarifa hizo zinazosambazwa hazina ukweli wowote.