Kwanini kutoa Pesa kwenye Mabenki kutachochea Kuanguka kwa Serikali ya CCM. Katika jicho la Kiuchumi na Sayansi ya Siasa

Kwanini kutoa Pesa kwenye Mabenki kutachochea Kuanguka kwa Serikali ya CCM. Katika jicho la Kiuchumi na Sayansi ya Siasa

MlimaSayuni

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
7,285
Reaction score
13,703
Mimi ni mmoja ya watu ninaounga mkono Maandamano yoyote yatakayotangazwa nchini hadi CCM ianguke na nchi ipate katiba mpya, hakuna shaka kabisa utawala uliopo umefitinika na hauna uhalali mbele ya watu na Mungu.

Leo nitaelezea njia mojawapo ya kuchochea kuanguka kwa Serikali ya CCM, njia hii ni moja ya njia za amani kabisa za kutangaza kutokuwa na Imani na huu utawala pamoja na mifumo yake wezeshi. Moja ya mfumo unaowezesha maovu yote nchini ni mfumo wa Kifedha nchini ambao uti wa mgongo wake ni Sekta ya Mabenki.

Ukitaka kumshinda adui yako vitani unashambulia maeneo makuu ya aina mbili, 1. Maeneo/Mifumo ya Uchumi, 2. Dhana za Kijeshi, hivi ndio Marekani hufanya kwa kila mtu anayepigana nae vita au mpinzani wake, sasa sisi Watanzania adui yetu ni CCM na utawala wake tumshambulie kwenye Mifumo ya uchumi ndio tufate maeneo ya kijeshi ikibidi.

Nianze na Utangulizi.
Mabenki mengi ya aina zote Duniani hufanya kazi kwa mfumo unaoitwa "fractional reserve banking", maana yake mabenki yanaruhusiwa kwa sheria kukaa na kiasi fulani cha pesa ya mteja na kukopesha au kuwekeza kiasi kingine.

1. Kwa sasa BoT inasimamia fractional reserve vipi?
Statutory Minimum Reserves (SMR), BoT ilipunguza SMR kutoka 7% hadi 6% ya amana za wateja mwaka 2020, na kiwango hiki cha 6% bado kinatajwa kama kiwango cha sasa kwenye maelezo ya sera na uchambuzi wa sheria.

Pia BoT inaweza kupunguza kiwango SMR kwa benki zinazokopesha sekta ya kilimo kwa riba nafuu, Report ya BoT ya mwaka 2024.

Hii ina maana gani?, Ukiwa na shilling 100, Benki uliyotunza hela inachukua shiling 94 yako inaenda kumkopesha Mwalimu alisimamia Uchaguzi, Inaenda kumkopesha Askari aliyeua mtu, Inaenda kuisaidia CCM kwenye kampeni na siasa zao za ovyo, inaenda Kuikopesha serikali kwa njia ya Hati fungani, hiyo ela inaenda kuwalipa Mishahara Askari wauaji, kununua silaha na risasi zilizoua watu, inaenda kuibwa na mafisadi na kutumiwa vibaya kadri iwizekavyo.

2. Serikali inakopa kiasi gani kutoka kwetu kuptia mabenki ya Ndani?

Kulingana na Taarifa za BoT Mwezi wa nane huu ndio ulikuwa mgawanyo wa deni la Ndani,
Taarifa ya Uchumi Mwezi wa Tisa, 2025
MkopeshajiKiasi (bilioni TZS)Sehemu ya deni la ndani
Mabenki ya biashara10,558.328.4%
Benki Kuu (BoT)7,052.219.0%
Mifuko ya pensheni10,116.527.2%
Makampuni ya bima1,821.84.9%
Mfuko maalum BoT799.32.2%
Wengine6,781.719.2%
Jumla37,129.8100%




Borrowing Instruments/Njia za Kukopa
Aina ya deniKiasi (bilioni TZS)Sehemu ya deni la ndani
Government securities (jumla)31,868.085.8%
↳Treasury bills ↳2,075.7 ↳5.6%
↳Government stocks ↳135.7 ↳0.4%
↳Government bonds ↳29,656.5 ↳79.9%
↳Tax certificates ↳0.1 ↳0.0%
Non-securitized debt (jumla)5,261.814.2%
Overdraft ↳5,243.4 ↳14.1%
Other liabilities ↳18.4 ↳0.0%
Jumla ya deni la ndani37,129.8100%




3. Mali za Benki, Amana za Wateja wa mabenki, Mikopo Halisi kwa Wateja Kwa Mabenki ya Tanzania

Hapa nitatumia mifano ya benki kubwa mbili na zingine mbili ndogo, Benki ndogo ndio rahisi kuanguka

Vyanzo
Financial Statement - CRDB
Financial Statement - NMB
Financial Statement - Maendeleo Bank
Financial Statement - MUCOBA Bank
Benki (2024)Mali za Benki (≈ TZS T)Amana (≈ TZS T)Mikopo Halisi (≈ TZS T)
CRDB16.610.810.4
NMB13.79.38.5
Maendeleo Bank0.150.100.09
MUCOBA0.020.010.01



Mgawanyo wa Mali za CRDB
Kipengele cha Mali za BenkiKiasi (≈ TZS bilioni)Maelezo kwa kifupi
Cash≈ 554Pesa taslimu kwenye tawi/ATM
Balances with Bank of Tanzania≈ 1,632Akiba na miamala kwa BoT (pamoja na reserve)
Investment in Government Securities≈ 2,063Uwekezaji kwenye T-bills na bonds za Serikali
Balances with Other Banks & FIs≈ 845Amana/miamala na mabenki na taasisi nyingine
Interbank Loans Receivables≈ 187Mikopo ya muda mfupi kwa mabenki mengine
Investment in Other Securities≈ 27Uwekezaji mwingine wa karatasi za fedha (zisizo za serikali)
Loans, Advances & Overdrafts (Net)≈ 10,369Mikopo halisi kwa wateja (baada ya makadirio ya mikopo mibovu)
Other Assets≈ 443Mali zingine (prepayments n.k.)
Equity Investments≈ 14Uwekezaji kwenye hisa/ubia wa makampuni mengine
Property, Plant & Equipment≈ 456Majengo, matawi, vifaa, mifumo n.k.
Jumla ya Mali za Benki≈ 16,591Jumla ya mali zote za benki


Mgawanyo wa Mali za NMB
Kipengele cha Mali za BenkiKiasi (≈ TZS bilioni)Maelezo
Cash≈ 629Pesa taslimu kwenye matawi na ATM za benki.
Balances with Bank of Tanzania≈ 863Akiba na miamala iliyopo kwenye Benki Kuu (pamoja na statutory reserve).
Investments in Government securities≈ 2,256Uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali (T-Bills na Bonds).
Balances with other banks and financial institutions≈ 171Amana/miamala ya muda mfupi na mabenki mengine na taasisi za kifedha.
Cheques and items for clearing≈ 2Hundi/cheque zilizo kwenye mchakato wa kulipwa/ku-clear.
Interbranch float items≈ 0.1Tofauti za muda wa uhamishaji kati ya matawi ya benki.
Bills negotiated≈ 16Bills za biashara ambazo benki imezifadhili (trade finance).
Interbank loans receivables≈ 718Mikopo ya muda mfupi ambayo NMB imekopesha mabenki mengine.
Investments in other securities≈ 13Uwekezaji mwingine kwenye karatasi za fedha zisizo za serikali.
Loans, advances and overdrafts (net)≈ 8,499Mikopo halisi kwa wateja (baada ya kutoa makadirio ya mikopo mibovu).
Other assets≈ 366Mali zingine za uendeshaji: prepayments, piu, n.k.
Equity investments≈ 4Uwekezaji wa NMB kwenye hisa/ubia wa makampuni mengine.
Property, plant and equipment≈ 193Majengo, samani, vifaa, mifumo ya IT, magari, n.k.
Jumla ya Mali za Benki≈ 13,731



Mgawanyo wa Mali wa Maendeleo Bank
Kipengele cha Mali za BenkiKiasi (≈ TZS bilioni)Maelezo kwa kifupi
Cash and balances with Bank of Tanzania≈ 10.4Pesa taslimu na mizania iliyo BoT (pamoja na reserve).
Placements and balances with other banks≈ 14.1Amana/mizania ya muda mfupi na mabenki mengine.
Government securities≈ 29.5Uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali (T-Bills & Bonds).
Loans and advances to customers≈ 88.6Mikopo kwa wateja (kabla ya makato ya ECL).
Inventories0
Other assets≈ 2.5Mali nyingine za uendeshaji (prepayments, piu, n.k.).
Intangible assets≈ 0.2Mali zisizogusika – software, licences, n.k.
Property and equipment≈ 2.3Majengo, samani, vifaa, mifumo ya IT, n.k.
Leasehold improvements≈ 0.6Uboreshaji wa maeneo ya pango (leasehold).
Tax receivable (payable)≈ 0.8Kodi inayodaiwa na/au kulipwa (net).
Deferred tax≈ 2.2Kodi ya kuahirishwa (deferred tax asset).
Jumla ya Mali za Benki≈ 151.2

[td>Hakuna stock/inventory mwishoni mwa mwaka.[/td]


Mgawanyo wa Mali za Bank ya MUCOBA
Kipengele cha Mali za BenkiKiasi (≈ TZS bilioni)Maelezo
Cash≈ 0.28Pesa taslimu kwenye tawi/kaunta/ATM za MUCOBA.
Balance with Bank of Tanzania≈ 0.14Akiba na mizania iliyohifadhiwa kwenye Benki Kuu (pamoja na reserve).
Investments in Government securities0
Balance with other banks and financial institutions≈ 0.75Amana/mizania ya muda mfupi kwenye mabenki na taasisi nyingine za kifedha.
Cheques and items for clearing0Hakuna hundi zilizokuwa kwenye mchakato wa "clearing" tarehe hiyo.
Inter branch float items0Hakuna tofauti za muda kati ya matawi zilizobaki kwenye vitabu.
Bills negotiated0Hakuna bills za biashara zilizofadhiliwa (negotiated bills) mwishoni mwa mwaka.
Customers' liabilities for acceptances0Hakuna dhamana za "acceptances" za wateja zilizosimamiwa na benki.
Interbank loans receivables0Hakuna mikopo ya muda mfupi ambayo MUCOBA imekopesha mabenki mengine.
Investments in other securities0Hakuna uwekezaji mwingine wa karatasi za fedha.
Loans, advances and overdrafts (net of allowances)≈ 13.36Mikopo halisi kwa wateja baada ya kutoa makadirio ya mikopo mibovu.
Other assets≈ 3.70Mali zingine (prepayments, piu, n.k.) zinazotokana na uendeshaji wa benki.
Equity Investments0Hakuna uwekezaji kwenye hisa/ubia wa makampuni mengine.
Property and Equipment and Right of Use Assets≈ 0.29Majengo, samani, vifaa, mifumo ya IT, pamoja na haki za kutumia mali za upangishaji (ROU assets).
Jumla ya Mali za Benki≈ 18.51Ndiyo ukubwa wote wa balance sheet ya MUCOBA (≈ TZS 18.5 bilioni).

[td>Hakuna uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali mwishoni mwa 2024.[/td]



4. Bank run: Watu wakienda Kuchukua kati ya 10-30% ya amana kwenye benki nne nilizozitolea Mfano
BenkiAmana (T)30% ya amana (T) – watu wanataka kuchukua
CRDB10.83.24
NMB9.32.79
Maendeleo0.100.03
MUCOBA0.0120.0036
Jumla20.2≈ 6.06



Jumla ya Pesa Taslimu TZS 6..06 zitakuwa mikononi nje ya taarifa za Serikali ndani ya muda mfupi, hii itakuwa hatua nzuri ya awali kuifanya Serikali ipate msukosuko wa Kifedha, hapa tunaingia kwenye kitu kinaitwa Liquidation

Hatua ya Kwanza kukabiliana na hii Changamoto itakuwa ni bank kutumia cash walizonazo hapa tunazungumzia karibu 1.19T Fedha taslim.

Hatua ya pili Benki lazima wachukue akiba zao B.o.T, Akiba kwenye Benki Kuu ≈ TZS 2.50 trilioni, Baada ya hapa itabidi benki kuu itoe msaada wa Takribani shilingi trilioni 2.4 kama itachelewa au kutopatikana sekta ya benki itaingia kwenye Mgogoro mkubwa, Hazitaweza kutoa mikopo mipya, riba itaongezeka kama upepo, bank ndogo kabisa Kama MUCOBA zitakuwa kwenye hatari ya kuwa Insolvent.

Pia Bank kubwa itabidi ivute fedha zako kwenye mabenki mengine madogo (chain reaction) itatokea kwenye mfumo wa bank wote.

Tanzania tuna bank kama MUCOBA ambayo imekopesha akiba yote ya Watu, this is very interesting, hakuna protection ya mteja kabisa.

5. Athari kwa Serikali kufanya kazi​

Hapa ndio lengo letu la msingi Serikali inapoteza urahisi wa kukopa ndani​

  • Benki Ndio wanunuzi wakuu wa hati fungani za serikali (hazina za muda mfupi na muda mrefu).
  • Benki Pia ndizo zinazosimamia akaunti nyingi za serikali (mapato, mishahara, miradi).
Kwa Mabenki
  1. Benki zinajikita zaidi kwenye kuokoa ukwasi kuliko kununua hati mpya za serikali.
    • Inakuta riba zinapanda sana,
    • Au zabuni za hati za serikali hazijajazwa vya kutosha.
Matokeo:
  • Serikali inaweza kulazimika kuchelewesha malipo (kwa wakandarasi, mishahara, miradi).
  • Au kutafuta mkopo wa haraka kutoka nje kwa masharti magumu.
6. kupanda kwa bei na kuyumba kwa sarafu

Benki Kuu ikitoa Takribani TZS 2.4 trilioni za ziada kuokoa benki, fedha kwenye mzunguko zitaongezeka, matokeo ya hili ni mfumko wa bei, kushuka kwa Shilingi, hapa ndio narudia ushauri wa msingi hakikisha unanunua foreign currency, hii pia ni mbinu ya kuidhoofisha serikali kifedha.

7. Bima ya amana
Kama benki ndogo zikianguka kabisa, Tanzania bima ya amana ni million 7.5:
  • Mfuko wa bima ya amana utalazimika kuwalipa wateja ndani ya kiwango kinacholindwa.
  • Kama haitoshi,
    • Serikali au BoT wanaweza kulazimika kuingiza mtaji mpya katika benki fulani,
    • Hii inaweza kuongeza mzigo kwenye bajeti ya serikali au kuilazimu serikali ikope zaidi (kumbuka Serikali haiwezi kukopa nje, hii kwetu ni shinikizo muhimu sana).

8. Mifano ya Bank runs za Hivi karibuni

1. Cyprus – mgogoro wa benki na “haircut” ya amana (2013)


Benki za Cyprus zilikuwa zimewekeza sana kwenye deni la Ugiriki, Athari za deni la Ugiriki zilipofumuka, Benki zikawa dhaifu sana, Ikabidi watafute msaada wa dharura kutoka umoja wa Ulaya na IMF.

Tuchukue somo kutoka Cyprus, asilimia 28 ya deni la ndani la Tanzania linatokana na Bank za Tanzania, tofauti na wao EAC, SADC au AU hawezi kutupa msaada wa dharura, pia tumepoteza sifa za kupata mkopo kutoka IMF.

Nini Serikali inaweza kufanya kwenye mgogoro huu. Vikwazo vya kutoa fedha na kuhamisha fedha nje ya nchi, Kwa baadhi ya akaunti kubwa, sehemu ya amana ilichukuliwa moja kwa moja kuokoa benki (hasa amana kubwa zisizolindwa).

Hii ni muhimu kwenu ninyi wenye Mapesa mengi bank mnaolinga kuzitoa na hata kuziweka nje ya nchi. Kwenye mgogoro kama huu ukiwa na hela nyingi zaidi ya milion 7.5 unaweza kutakiwa kugawana Hasara na Benki

2. Ugiriki – kufungwa kwa benki na ukomo wa kutoa fedha (2015)


Chanzo hapa ni deni la Serikali, Nyie msiotaka kutoa pesa zenu, mnadhani Serikali ya Samia bila mikopo na fedha za kigeni kwenye utalii na wawekezaji wa nje itaweza kulipa deni kwa wakati? Ni muda wa kuiwahi serikali kabla haijawahai.

Serikali ilichukua hatua kama ya Cyprus.

3. Lebanon – watu kushindwa kabisa kufikia amana zao (tangu 2019)

Madeni makubwa ya serikali, ufisadi, uchumi dhaifu, na kupungua kwa fedha za kigeni. Mfumo wa benki ulishindwa kuendelea kulipa amana kikamilifu

Serikali yao ilichukua njia zilezile wengine walizofanya, Ugiriki na Cyprus, Lebanon watu walienda mbali sana wakaamua kuvunja benki na kuchukua fedha zao.

Ndugu zangu Watanzania, kuwahi kuushinikiza huu utawala ni jambo bora kuliko kusubiri utawala uanguke kifedha kabisa uanguke na fedha zetu, Tuanze kampeni ya kutoa fedha zetu benki na mifumo ya fedha za simu (Hela zao pia zinakaa kwenye Mabenki), kununua sarafu za kigeni (hii pia ni njia ya kuangusha sarafu na yale mahela wanayolipwa wasiojulikana, hii ni collateral), pia kama unaaccount nje anza kuhamisha nje.

Watanzania kwa pamoja tunaweza kudhoofisha nguvu za CCM kwa kutumia kila njia, hii ni moja wapo.
 
Screenshot_20251119-103538~2.png
 
Ni wazo zuri. Inahitaji staying power Martin Luther King Junior, Malcolm X, Gadhi walitumia hii mbinu.

Ilichukukua miezi lakini haki zilipatikana. Napendeza itumike pamoja na mbinu nyingine.
 
Jambo lingine kwa Watumishi wa umma kwa nini Serikali hii ilikosa maarifa inawalazimisha msichukue fedha zenu za pensheni mnapostaafu au mkiacha kazi kwa sababu asilimia 27 ya deni la ndani inatokea hapo (pesa wanazochukua kwa nguvu), inaona mkichukua haraka au mkipewa zote itasabisha Serikali isifanye kazi.

Unganeni na sisi wadai haki turekebishe hili jambo, pesa zenu msipoweza kuzisimamia Mafisadi hawataacha kuzitumia ovyo.
 
Nimetumia muda wangu kufanya research ya documents za B.o.T, CRDB, NMB na benki zingine kwenye hili.

Tukijitoa wote tutaisaidia nchi haraka sana

Kabisa, nakupongeza sana, umeeleweka sana sana
 
Sidhani kama unaelewa madhara mapana ya ku-fail kwa mfumo wa kibenki katika nchi.

Watakao athirika ni raia zaidi kushinda serikali, sumu aionjwi. Samia kujaribu kwa kufanya mauaji hawezi pendwa na watanzania tena hata afanye nini, asafishiki ata kwa dodoki.

Same kufail kwa bank madhara yake story ni ndefu sana kwenye uchumi. Kwa ufupi bank inakopeshea hela za wateja na sehemu kubwa ya asset ni mikopo ukishaua bank umepoteza hela za wateja.

That’s just a start, hili ni wazo la mtu ambae hajui madhara ya ku-fail kwa bank otherwise downside spiral effect sikia tu kuna hyperinflation, kupotea kwa pensions, kukosekana kwa huduma za jamii kama, kusimama kwa shughuli za uchumi.

Hakuna nchi duniani inayoombea ‘bank failure’ sio kwa madhara ya serikali ni kwa kulinda raia kwanza.
 
Sidhani kama unaelewa madhara mapana ya ku-fail kwa mfumo wa kibenki katika nchi.

Watakao athirika ni raia zaidi kushinda serikali, sumu aionjwi. Samia kujaribu kwa kufanya mauaji hawezi pendwa na watanzania tena hata afanye nini, asafishiki ata kwa dodoki.

Same kufail kwa bank madhara yake story ni ndefu sana kwenye uchumi. Kwa ufupi bank inakopeshea hela za wateja na sehemu kubwa ya asset ni mikopo ukishaua bank umepoteza hela za wateja.

That’s just a start, hili ni wazo la mtu ambae hajui madhara ya ku-fail kwa bank otherwise downside spiral effect sikia tu kuna hyperinflation, kupotea kwa pensions, kukosekana kwa huduma za jamii kama, kusimama kwa shughuli za uchumi.

Hakuna nchi duniani inayoombea ‘bank failure’ sio kwa madhara ya serikali ni kwa kulinda raia kwanza.
Kwenye andiko langu nimeandika collateral, pia nimesema ni we need to "fail fast", nchi inatafunguka haraka kama kutakuwa na uwajibikaji wa haraka, kadri tunavochelewa ndio tunaenda njia ya Zimbabwe, na kibaya zaidi huu utawala unaanza kufanya uchochezi wa Kidini
 
Ni kuendelea kuminy pumbu tu mpaka mjomb achuchumae chini 😂
 
Sidhani kama unaelewa madhara mapana ya ku-fail kwa mfumo wa kibenki katika nchi.

Watakao athirika ni raia zaidi kushinda serikali, sumu aionjwi. Samia kujaribu kwa kufanya mauaji hawezi pendwa na watanzania tena hata afanye nini, asafishiki ata kwa dodoki.

Same kufail kwa bank madhara yake story ni ndefu sana kwenye uchumi. Kwa ufupi bank inakopeshea hela za wateja na sehemu kubwa ya asset ni mikopo ukishaua bank umepoteza hela za wateja.

That’s just a start, hili ni wazo la mtu ambae hajui madhara ya ku-fail kwa bank otherwise downside spiral effect sikia tu kuna hyperinflation, kupotea kwa pensions, kukosekana kwa huduma za jamii kama, kusimama kwa shughuli za uchumi.

Hakuna nchi duniani inayoombea ‘bank failure’ sio kwa madhara ya serikali ni kwa kulinda raia kwanza.
Tusipoitoa CCM nchi hii itakuwa failed state, na tutairejesha kwa damu nyingi
 
Kuna watu mmeumbwa kuandika,
AI Mkuu wala usidanganyike anachofanya ni copy and paste halafu anaediti baadhi ya maeneo. All in all miaka 5 siyo mingi tuvumilieni tu maana CCM wameshaona wapi wamekosea..
 


Watanzania
 
Back
Top Bottom