BoT wakanusha taarifa za upotoshaji kuhusu usalama wa mifumo ya malipo na akaunti za amana. Mifumo ipo salama

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni zinazoeleza kuwa benki za biashara nchini zimepata au zinatarajiwa kupata shambulio la kimtandao litakalosababisha upotevu wa fedha za wateja na kusababisha hitilafu katika mifumo ya kibenki.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa na Gavana Emmanuel Tutuba siku ya Jumamosi Novemba 22, 2025, BoT imesema taarifa hizo ni za upotoshaji na zimekusudiwa kuwatia hofu wananchi ili kuwahamasisha kutoa fedha kutoka kwenye akaunti zao.

Kwa mujibu wa Benki Kuu, mifumo ya malipo ya Taifa inaendelea kufanya kazi kwa usalama na ufanisi, na amana za wateja katika benki zote za biashara zipo katika uangalizi wa karibu na wa kitaalamu. Benki Kuu imewahakikishia wananchi kuwa hakuna shambulio lolote la kimtandao lililotokea katika benki nchini, na kwamba taarifa hizo zinazosambazwa hazina ukweli wowote.

​
 
Mbona ukituma pesa zinaganda hewani, kuna miamala kwa sasa ukituma pesa haifiki inapoenda na hairudi ilipotoka mpaka hakuna maana ya huduma, .
 
Naweza waamini BOT. Japo sio kwamba haiwezekani wao kuingiliwa mifumo yao
 

Watanzania Katoeni pesa Bank
 
Uzuri nikwamba wametuthibitishia wenyewe kuwa wapo salama ,wacha tushike hiyo ,japo ukweli haupo hivyo na soon watakuja hadharani kivingine ,tujipe muda tena siyo muda mrefu .
 
Serikali imekuwa ya kipuuzi kila kitu inajibu...
'Mama Samia hajanya siku ya sita leo'.
Nasubiri serikali ije kukanusha!
 
Serikali imekuwa ya kipuuzi kila kitu inajibu...
'Mama Samia hajanya siku ya sita leo'.
Nasubiri serikali ije kukanusha!
kwa sababu wasipojibu watu wanaamini uongo na wameshazoeshwa na mange kimambi kupenda uongo na udaku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…