Boti iliyookotwa Zanzibar hii hapa, Wanajeshi waifanyia uchunguzi baada ya hofu ya mabomu

Boti iliyookotwa Zanzibar hii hapa, Wanajeshi waifanyia uchunguzi baada ya hofu ya mabomu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, Rashid Hadid Rashid amesema hakuna mabomu yaliyokutwa katika boti iliyookotwa kando kando mwa fukwe ya bahari ya Bwejuu kama ilivyodhaniwa na baadhi ya wavuvi walioisogeza boti hiyo ufukweni

RC Rashid amebainisha hayo siku ya pili baada ya boti hiyo kusogezwa katika fukwe ya bahari ya Bwejuu mnamo April 23, 2022, katika juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama juu ya kuibinuwa boti hiyo ambayo zoezi lake ilichukua siku mbili kufanikiwa.

Rashid amesema boti hiyo ambayo ina usajili wa Mauritius inadhaniwa kuibiwa kutoka nchi hiyo.



Source: Wasafi FM
 
Sasa mbona hawajavaa PPE [emoji3064]
 
Maajabu, boti inaokotwa, ina maana kuna mtu kaidondosha au kaitupa ikaokotwa
 
Hiyo boat naona jamaa wali i iba huko kwao na kuitumia kusafirishia drugs naona baadae waka enda kuitelekezea mbali huko naona imekuja kwa mawimbi ya bahari mpaka Zanzibar sijui ilipata dhoruba gani jingine maana naiona ipo juu chini.
 
Sasa kuinuia Boti tuu ndo imechukua siku 2, kwani Zanzibar hakuna zile All Terrain Crane
 
Yani Imeptaje Madagascar ikiwa ina elea elea ivyoo bila kuonekana au ilizama ikaja kuibukia zenji
 
Back
Top Bottom