Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Tarehe 11 Agosti 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Broadhurst, nchini Botswana, ilitoa hukumu dhidi ya raia wa Tanzania, Emma Sezary Beda (42), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la umiliki wa dawa za kulevya aina ya “dagga” (bhangi).
Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi la Botswana, tukio lilianzia mnamo 14 Aprili 2025 wakati askari walipofanya upekuzi wa ghafla kwenye gari alilokuwa akisafiria, karibu na eneo la Tsolamosese. Ndani ya gari hilo walibaini zaidi ya kilo 5 za mmea unaosadikiwa kuwa bangi.
Uchunguzi uliendelea hadi kwenye nyumba aliyokuwa ameikodisha Mogoditshane-Nkoyaphiri, ambapo askari walipata kiasi kingine cha vitu vinavyodhaniwa kuwa bangi.
Baada ya kusikiliza ushahidi, mahakama ilimhukumu Emma kulipa faini ya P40,000 (takriban Tsh. milioni 7.5) ndani ya miezi mitatu, au kutumikia kifungo cha miaka 2 iwapo hatalipa.