Botswana imefanyaje kufikia hatua hii?

Uzalendo hauletwi na nyie magenge ya majizi
Nyie si ndio miccm isiyoshiba, mnakula bila kubakisha, hamjui kuna watu wengi wanahitaji kupata huduma muhimu za kiuchumi na kijamii.

Siku ccm itupiliwe mbali kabisa, lije kundi maalumu la kuleta uzalendo katoka nchi ili tuanze upya.

CCM ni kundi dogo sana lina watu wachache sana ila ni walafi na wanaimaliza nchi.

Nitolee uchawa wako hapa.
 
Wenzetu wamejipanga na wanadhamiria kufanya mambo ya maendeleo,wana mikakati
Botswana,Namibia nchi moja safi sana
Zimbabwe yenyewe miaka ile tunaenda ya 90s huko ilikuwa safi sana ukifika huko wenyewe tunashangashanga,tunaenda huko ili kuwaletea wabongo maziwa wanywe ya super milk
Leo hii humu tunabishana na watoto wadogo tena wanangu wakina Tlaatlaah
😄

Ova
 
Population ya 2.5mill yaani 1/3 ya Dar a lot of natural resources, Diamond 💎 na gold za kutosha plus utawala Bora Kila kitu kimewezekana.
 
Population ya 2.5mill yaani 1/3 ya Dar a lot of natural resources, Diamond 💎 na gold za kutosha plus utawala Bora Kila kitu kimewezekana.
Hivi tz utawala bora,uongozi bora
Haliwezekani

Ova
 
miaka ya 90 dah
Zimbabwe hata kama pangekua hakuna tatizo wasingetufikoa kwa chochote, hilo la kwanza....

lakini pia huko pengine ulikopataja sijui ati Namibia, sijui Botswana n.k, ati wamejipanga

labda wamejipanga kua na maisha magumu.
ndio maana wanafunzi wakija kusoma Tz, wakimaloza hawatamani tena na wala hawataki kurudi kwao, huko ukilopataja kwa kwasababu wana maisha mazuri, na wamejipanga, right?

nchi ulizozitaja sijui nisemaje,
ila itoshe tu kusema ni maskini sana, wana hali ngumu mno ukilinganisha na nchi nyingine barani Africa. Inatia huruma, inaskitisha sana.
kiufupi hakuna cha kujifunza katika nchi hizo...


kwan, hakuna namna nyingine ya kupotosha ndugu yangu mrangi ?

au njala yaavire
 
Mwanangu we mmbishi sana
Unataka kusema tz watu hawaishi
Kwenye hali ngumu

Ova
 
1. Naweza kusema population density yao ni ndogo sana, watu 4.6 kwa kilometa ya mraba ukilinganisha na Tanzania ina watu 72 kwa kilometa ya mraba. Kimantiki ukiwa na rasilimali nyingi na mpo wachache maana yake ni matajiri lakini pia kwa upande mwingine uwezo wao wa uzalishaji upo chini. Fikiria unahitaji hospitali na mashule mangapi kwa watu 2m vs watu 62m.

2. Kutokuwa na umaskini - ukiwa hauna umaskini unakuwa huna haja ya kufanya ubadhirifu kujilimbikizia mali sababu mahitaji muhimu yote unapata hivyo huna ule woga uliopo Tanzania kwamba mtu anahakikisha anajilimbikizia yeye na ndugu zake kwa kuogopa umaskini.

3. Elimu bora na maadili - elimu bora inaleta viongozi bora na pia maadili ya jamii yanatengeneza watu waadilifu. Nchi kama yetu watu ni wezi kwa ngazi zote kuanzia mfagizi mpaka wale wa juu na jamii imekubali.

4. Uzalendo, Katiba bora, mfumo wa demokrasia na siasa - hivi vitu visipokaa sawa ni ngumu kupiga hatua kama taifa. Botswana iko mbele kwenye hivi vitu.
 
Mwanangu we mmbishi sana
Unataka kusema tz watu hawaishi
Kwenye hali ngumu

Ova
sasa kama ni Tz, si tuzungumze ya Tz kuliko kule ilikopataja mwanzo

hali ngumu mara nyungi huwakumba baadhi ya watu wavivu wachache, dhidi ya wachapakazi wengi ambao hawana tatizo na mtu, wala kulalamika lalamika na kulaumu bila kikomo huku wakiwa na gubu dhidi ya wanaofanya bidii
 
Total population is not more than 3 million. Sawa na population ya mkoa wa Mwanza
Population ikiwa kubwa ni faida kwa nchi kwani ni sources of 1. Productions labour 2. Market ndo maana nchi kama China , India, USA, Brazil zina watu wengi na zimeendelea sana.
 
Mpaka watu washtuke na kuvunja laana iliyo kwenye ardhi ya Tanzania 🇹🇿 toka mwaka 1967.
 
...Na Jeshi liko busy Kuliñda Mipaka ya Nchi TU, kinachoendelea Ndani ya Nchi halina Habari! Sad. [emoji35][emoji35]
 
Good Governance, that is all..!! Sijasema kingine, mie CCM, ila sijasema chochote msije niwekea maneno mdomoni..!!
 
Nchi yetu ingekuwa hapo kama ilivyo Botswana ila mikataba mibovu iliyosainiwa na viongozi hasa miaka ya nyuma imetukwamisha sana. Inashangaza sana kuona nchi hii ambayo ina rasilimali nyingi ikihangaika kwenda kukopa huku ikishindwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa ajili ya wananchi wake kuondokana na utegemezi.
 
Wanakula na makaburu, hawajimwambafai.
 
Wacha sisi tuhangaike na siasa za kijinga
Sio siasa za kijinga, Botswsna wanategemea madini na hakuna rukhsa kuuwepo na wachimbaji wadogo.

Mchimbaji mdojo ukinusa tu sehemu za almasi unauliwa.

Mnataka Tanzania ifanye hivyo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…