Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Township Rollers 0 - 0 Yanga SC
(Agg; 2 - 1)
01': Mpira umeanza hapa(Agg; 2 - 1)
02': Dakika ya pili ya mchezo, mpira unaendelea
03': Township wanamiliki mpira eneo la kati, unapigwa kwenda mbele lakini unatok nje
05: Mpira umeanza kwa kasi, kila timu inajaribu kutafuta bao la mapema
Kapteni wa Township anapoteza pasi kati mwa uwanja baada ya kutenegezewa na mwenzake, mpira unakwenda nje, Yanga wanarusha
17': Yusuph Mhilu anaenda na mpira sasa, anaukokota na anauota mwenyewe, unarushwa kuelekea Yanga
18': Gadiel Michael anatoka nje kugagangwa, ameumia
19': Faulo inapigwa kuelekea Yanga, kushoto kidogo mwa Uwanja, inapigwa, beki Andrew Vincent anaokoa kwa kichwa.
21': 0-0 mpaka sasa, kila timu inapambana kupata bao la mapema, Rollers wanakwenda, pigwa moja ndefuuu, inatoka, free kiki kuelekea Rollers.
22': Youthe Rostand ameumia, anapeana tano na Mwamuzi, tayari ashainuka
24':Nyavu bado ni ngumu kutikisika kwa pande zote mbele, kila timu inafanya mashambulizi ya kushtukiza
27': Mpira sasa anao Kamusoko katikati mwa Uwanja, anapasia kwake Mhilu, namna gani ananyang'anywa na wapinzani.
28': Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kucheza faulo, inapigwaaa, hatari, Mwamuzi anasema offside.
30': Yondani na mpira, anapasia huku pembeni lakini Rollers wanauchukua, unapigwa mbele huku, Vincent anakataa anautoa nje.
31': Mpira unarushwa kuelekea Yanga, Yanga wanauchukua, kwake Chirwa, faulo, inapigwa kuelekea Rollers.
32': Inapigwa unamkuta huku Mhilu, anapiga shuti lakini inakuwa goli kiki.
33'; Juma Abdul anautoa mpira nje, Rollers wanarusha, hatari katika eneo la Yanga ndani ya penati boksi, wanarudisha tena nyuma na kuanza upya.
34': Obrey Chirwa yupo chini, mpira umesimama, Lwandamina anajibizana na, Yondani anaingilia anapewa kadi ya njano.
35': Mpira anao Rostand, anapiga mbele huku, Rollers wanatoa nje, unarushwa huku, Yanga wanautoa, kwake Lemponye, wanagongeana hapa, faulo.
37: Rollers wanashambulia pembeni ya kulia mwa Uwanja, lakini mpira unatoka nje.
38': Mechi bado ngumu, nyavu bado hazijatikisika hata kwa nje.
39': Yondaaaaani, piga mashine moja inapaa juu ya lango la wapinzani.
41': Hatari katika lango la Yanga, namna gani mshambuliaji huyu anakosa bao la wazi kabisa, matokeo nado ni 0-0
42': Dakika 3 zimesalia mpira kwenda mapumziko
43': Papy amelala chini, yawezekana akawa ameumia, madaktari wanaingia kumpa huduma
44': Rollers wanakwenda sasa, wanashambulia kueleka lango la Yanga, wanapotezana hapa, Yondani anaokoa mpira na kupiga mbele.
45': Matokeo ni 0-0 bado
DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA, MPIRA NI MAPUMZIKO
45': Yanga wanaanzisha, matokeo ni 0-0
46': Mpira umesimama, mchezaji wa Township ameumia, unapigwa kuelekea Yanga
48': Rollers wanapandisha mashambulizi, Gadiel Michael anatoa mpira, unarushwa kuelekea Yanga, unamkuta lemponye, anapiga, Dante anaokoa.
49': Hatari langoni mwa Yanga ndani ya penati boksi, Rostand anaokoa.
51': Takribani dakika zote za kipindi cha kwanza Rollers wameliandama lango la Yanga
52': Inapigwa faulo kati ya uwanja kuelelea Yanga, pigwa kulee, Rostand anaidaka.
53': Hatariii, shuti kali linapigwa na mshambuliaji wa Rollers, Rostand anaupangua mpira na kutoka nje, kona.
54': Inapigwa huku, kipa anadaka
57': Yanga wanazidi kuruhusu lango kushambuliwa
59': Yanga wanapandisha mashambulizi sasa lakini Rollers wanaokoa, wanakwenda langoni mwa Yanga, linapigwa shuti kali, Rostand anaokoa kwa kupiga shuti kueleka kwa wapinzani
62': Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kamusoko, anaingia Ajibu
63': Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Rollers, ni karibu na eneo la hatari la wapinzani, unarushwa huku, kwake Chirwa, unakwenda nje.
65': Yanga wanarusha tena, Gadiel Michael, kwake Makapu, pigwa huku kwake Chirwa, wanaokoa huku Rollers
66': Mpira umeelemea kuelekea langoni mwa Yanga, Rollers wanashambulia vilivyo lango lao, matokeo bado ni 0-0
67': Kona nyingine inapigwa kuelekea Yanga
68': Inapigwa, Dante anaokoa kwa Kicgwa, Yanga wanafanya mabadiliko. Yusuph Mhilu anatoka na Mwashiuya anachukua nafasi yake
70': Bado Rollers wameliandama vilivyo lango la Yanga.
Chirwaaaaa, piga shuti moja engo ya kulia mwa Uwanja lakini linakuwa shuti mkaa.
72': Kinachoonekana hapa Rollers wanajaribu kupiga mashuti ya mbali kutafuta bao.
74': Tayari ameshainuka, mpira unaendelea. Kwake Said Makapu, pasia huku pembeni kwa Ibrahim Ajibu. Bado Yanga wanao.Dk 73, Rostand ameumia tena, mpira umesimama.
75': Faulo, Chirwa anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.
78': Mchezaji Seko amedondoka chini, mpira umesimama.
79': Chirwa anapata nafasi ya kupiga shuti, mpira unakwenda sentimita chache nje. Bado milango ni migumu.
82': Rostand anafanya kazi kubwa leo, anaokoa krosi hapa, kona nyingine.
83': Ajib anafanywa faulo, inapigwa sasa kuelekea Rollers, upande wa kulia mwa Uwanja
85': Dakika 5 zimesalia mpira kumalizika, milango bado ni migumu.
86': Nsanjigwa ametolewa nje baada ya kuanza kubishana na Mwamuzi, ameenda jukwaani
88': Rollers wanafanya mabadiliko, wanajaribu kupoteza muda.
89': Dakika moja imesalia mpira kumalizika.
DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, DAKIKA 4 ZIMEONGEZWA
91': Ajib na mpira, anapiga chenga mabeki wa Rollers, anadonoa shuti lakini mabeki wanaokoa
93': Mabadiliko mengine Rollers wanafanya.
Na mpira umekwisha, dakika 4 za kipindi cha pili zimemalizika, Yanga wanaondolewa kwenye mashindano baada ya mechi ya awali kukubali kipigo cha mabao 2-1