Botswana: Township Rollers 0 - 0 Yanga SC! Yanga imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa matokeo ya awali

Botswana: Township Rollers 0 - 0 Yanga SC! Yanga imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa matokeo ya awali

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
yanga.jpg


roller.jpg


Township Rollers 0 - 0 Yanga SC
(Agg; 2 - 1)
01': Mpira umeanza hapa

02': Dakika ya pili ya mchezo, mpira unaendelea

03': Township wanamiliki mpira eneo la kati, unapigwa kwenda mbele lakini unatok nje

05: Mpira umeanza kwa kasi, kila timu inajaribu kutafuta bao la mapema
Kapteni wa Township anapoteza pasi kati mwa uwanja baada ya kutenegezewa na mwenzake, mpira unakwenda nje, Yanga wanarusha

17': Yusuph Mhilu anaenda na mpira sasa, anaukokota na anauota mwenyewe, unarushwa kuelekea Yanga

18': Gadiel Michael anatoka nje kugagangwa, ameumia

19': Faulo inapigwa kuelekea Yanga, kushoto kidogo mwa Uwanja, inapigwa, beki Andrew Vincent anaokoa kwa kichwa.

21': 0-0 mpaka sasa, kila timu inapambana kupata bao la mapema, Rollers wanakwenda, pigwa moja ndefuuu, inatoka, free kiki kuelekea Rollers.

22': Youthe Rostand ameumia, anapeana tano na Mwamuzi, tayari ashainuka

24':Nyavu bado ni ngumu kutikisika kwa pande zote mbele, kila timu inafanya mashambulizi ya kushtukiza

27': Mpira sasa anao Kamusoko katikati mwa Uwanja, anapasia kwake Mhilu, namna gani ananyang'anywa na wapinzani.

28': Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kucheza faulo, inapigwaaa, hatari, Mwamuzi anasema offside.

30': Yondani na mpira, anapasia huku pembeni lakini Rollers wanauchukua, unapigwa mbele huku, Vincent anakataa anautoa nje.

31': Mpira unarushwa kuelekea Yanga, Yanga wanauchukua, kwake Chirwa, faulo, inapigwa kuelekea Rollers.

32': Inapigwa unamkuta huku Mhilu, anapiga shuti lakini inakuwa goli kiki.

33'; Juma Abdul anautoa mpira nje, Rollers wanarusha, hatari katika eneo la Yanga ndani ya penati boksi, wanarudisha tena nyuma na kuanza upya.

34': Obrey Chirwa yupo chini, mpira umesimama, Lwandamina anajibizana na, Yondani anaingilia anapewa kadi ya njano.

35': Mpira anao Rostand, anapiga mbele huku, Rollers wanatoa nje, unarushwa huku, Yanga wanautoa, kwake Lemponye, wanagongeana hapa, faulo.

37: Rollers wanashambulia pembeni ya kulia mwa Uwanja, lakini mpira unatoka nje.

38': Mechi bado ngumu, nyavu bado hazijatikisika hata kwa nje.

39': Yondaaaaani, piga mashine moja inapaa juu ya lango la wapinzani.

41': Hatari katika lango la Yanga, namna gani mshambuliaji huyu anakosa bao la wazi kabisa, matokeo nado ni 0-0

42': Dakika 3 zimesalia mpira kwenda mapumziko

43': Papy amelala chini, yawezekana akawa ameumia, madaktari wanaingia kumpa huduma

44': Rollers wanakwenda sasa, wanashambulia kueleka lango la Yanga, wanapotezana hapa, Yondani anaokoa mpira na kupiga mbele.

45': Matokeo ni 0-0 bado

DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA, MPIRA NI MAPUMZIKO

45': Yanga wanaanzisha, matokeo ni 0-0

46': Mpira umesimama, mchezaji wa Township ameumia, unapigwa kuelekea Yanga

48': Rollers wanapandisha mashambulizi, Gadiel Michael anatoa mpira, unarushwa kuelekea Yanga, unamkuta lemponye, anapiga, Dante anaokoa.

49': Hatari langoni mwa Yanga ndani ya penati boksi, Rostand anaokoa.

51': Takribani dakika zote za kipindi cha kwanza Rollers wameliandama lango la Yanga

52': Inapigwa faulo kati ya uwanja kuelelea Yanga, pigwa kulee, Rostand anaidaka.

53': Hatariii, shuti kali linapigwa na mshambuliaji wa Rollers, Rostand anaupangua mpira na kutoka nje, kona.

54': Inapigwa huku, kipa anadaka

57': Yanga wanazidi kuruhusu lango kushambuliwa

59': Yanga wanapandisha mashambulizi sasa lakini Rollers wanaokoa, wanakwenda langoni mwa Yanga, linapigwa shuti kali, Rostand anaokoa kwa kupiga shuti kueleka kwa wapinzani

62': Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kamusoko, anaingia Ajibu

63': Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Rollers, ni karibu na eneo la hatari la wapinzani, unarushwa huku, kwake Chirwa, unakwenda nje.

65': Yanga wanarusha tena, Gadiel Michael, kwake Makapu, pigwa huku kwake Chirwa, wanaokoa huku Rollers

66': Mpira umeelemea kuelekea langoni mwa Yanga, Rollers wanashambulia vilivyo lango lao, matokeo bado ni 0-0

67': Kona nyingine inapigwa kuelekea Yanga

68': Inapigwa, Dante anaokoa kwa Kicgwa, Yanga wanafanya mabadiliko. Yusuph Mhilu anatoka na Mwashiuya anachukua nafasi yake

70': Bado Rollers wameliandama vilivyo lango la Yanga.
Chirwaaaaa, piga shuti moja engo ya kulia mwa Uwanja lakini linakuwa shuti mkaa.

72': Kinachoonekana hapa Rollers wanajaribu kupiga mashuti ya mbali kutafuta bao.

74': Tayari ameshainuka, mpira unaendelea. Kwake Said Makapu, pasia huku pembeni kwa Ibrahim Ajibu. Bado Yanga wanao.Dk 73, Rostand ameumia tena, mpira umesimama.

75': Faulo, Chirwa anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.

78': Mchezaji Seko amedondoka chini, mpira umesimama.

79': Chirwa anapata nafasi ya kupiga shuti, mpira unakwenda sentimita chache nje. Bado milango ni migumu.

82': Rostand anafanya kazi kubwa leo, anaokoa krosi hapa, kona nyingine.

83': Ajib anafanywa faulo, inapigwa sasa kuelekea Rollers, upande wa kulia mwa Uwanja

85': Dakika 5 zimesalia mpira kumalizika, milango bado ni migumu.

86': Nsanjigwa ametolewa nje baada ya kuanza kubishana na Mwamuzi, ameenda jukwaani

88': Rollers wanafanya mabadiliko, wanajaribu kupoteza muda.

89': Dakika moja imesalia mpira kumalizika.

DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, DAKIKA 4 ZIMEONGEZWA

91': Ajib na mpira, anapiga chenga mabeki wa Rollers, anadonoa shuti lakini mabeki wanaokoa

93': Mabadiliko mengine Rollers wanafanya.

Na mpira umekwisha, dakika 4 za kipindi cha pili zimemalizika, Yanga wanaondolewa kwenye mashindano baada ya mechi ya awali kukubali kipigo cha mabao 2-1
 
Hii mechi ajibu angepaswa kuanza badala ya buswita ingekuwa tamu sana ,hakuna natural winga wa amsha amsha,papy na kamusoko wanatembea vizuri kati ila winga zimelala haziwezi dribble.
 
Wao wanaongoza wale hawajapata kitu. emmyta mtani je, unaonaje matokeo haya?
 
Gooooooooooooooooooooooo! Dah umeme umekatika hapa sina uhakika inawezekana
kakosa.
 
mmeshaanza propaganda
Hapana mwl kafanya vizuri kumuanzisha kamusoko ,papy yupo free huku makapu akicheza ukabaji naona papy na kamusoko wanatembea na mpira fresh ila tatizo kule mbele hakuna ubunifu buswita yupo slow na sio mtu wa kudrible Ajibu angeanza angeleta changamoto kwa mabeki na purukushani za chirwa mabeki wa rollers wangepata shida sana..winga za yanga hazina madhara
 
Chirwa anapiga straight anonymous pass ambayo kitaalam tunaiita single acrobatic pass. Ni pass ambayo wachezaji wachache sana huwa wanamudu kuicheza.

Kwako Jesse.
 
Back
Top Bottom