BOX BODY vs SCANIA MENDE

BOX BODY vs SCANIA MENDE

Ni suala la kufanya modifications tu mkuu kama ilivyo kwa Tandam (Fuso) hata hiyo scania mende unaifanyia. Scania na pilikapilika za mchanga labda barabara iwe ya kueleweka otherwise utalichukia. Migodini peleka Faw,Shaqman,Howo ukinunua jipya mpaka lianze kuleta migogoro faida ushaingiza. Unauza au unakatakata skrepa Unanunua nyingine mpya
 
Naomba mchango wenu , ushauri, mapendekezo, kuhusu biashara ya lori( Truck),

Mimi nina gari langu SCANIA MENDE, nimefanya nalo biashara ya mchanga kwa miaka 3 , lakini biashara imekuwa ngumu kutokana na kuingia hizi tipa za kichina,
Nimeonelea niibadili iwe box body ya kubeba mizigo kwenda mikoani,

Naomba mwenye ujuzi na biashara hiyo ya box body anifahamishe kabla sijafanya uamuzi wa kulivua tipa.

Naomba vilevile kama ninaweza kujua gharama za kutengeneza box body, na lipi ni zuri kati ya box body na body lililo wazi , ambalo unaweza kubeba mifugo toka mikoani,

Gari langu ni SCANIA 114 340

Ahsanteni Waungwana
Habari yako mkuu. Hongera kwa kujaribu kuwaza nje ya box baada ya mambo kuyumba, pole kwa changamoto hiyo.
Kwa hiyo gaari yako ni jambo zuri ambalo kimsingi nimekua nikiwashauri baadhi ya watu wenye tipa scania kwani mazingira ya uendeshaji yamekua ni magumu. Gari zinzpitia shurba ambazo hazikuumbwa nazo, inapigika, inakula hela nyingi ya matengenezo na mwisho wa siku zinakufa mapema ama kinachopatikana sio kile kilichotarajiwa.
Kwa upande wa mende, mi nashauri funga box body, irefushe kidogo na ikikaa sawa ikawa na uwezo wa kubeba tai 20 basi ni kiasi rafiki kabisa.
Kwa gari nyingi, by one huwa ndio kazi zake na katika hilo ninashauri beba mizigo inayoenda kupita kwenye barabara ya lami tu, maana ukiipeleka huko Ifakara ndanindani basi huwa sio rafiki sana kwa scania na utakua unaiumiza gari sana. Chagua route yako ya Mwanza japo mzigo wa return huwa ni mchache lakini ukiweka sawa mipango huwezi kukosa 4 hadi 6 kwa mwezi. Na wendi wale wanaotoa kwa malengo huwa ni kama 4M hadi 5 kwa wiki kwa gari mpya. Unampa dereva gari na machine ya EFD unasubiri hela yako mwisho wa mwezi
Kwa sasa hapa Dar gharama za kuweza kujenga box body, kuongeza chasis na ufundi pamoja na vifaa kazi vyote kwa wengi ni kati ya 18M hadi 21. So utajua wewe unafanyaje. Ushauri ni kuwa usiwashushe sana bei mafundi maana hata wakikubali basi uchue kuna ubora utapungua kwenye kazi yako. Ukimpata fundi mzoefu itakua vema zaidi.
Kila la kheri, kwa mende box body ninakuhakikishia huwezi kukosa kazi eti gari ilale hapa Dar kwa siku 3 kisa imekosa mzigo, kikubwa uzingatie route ambazo utakua ukienda ili kuwepo na mzigo wa kurudi.

Kila la kheri.​
 
Kama una mpango wa kuja kuvuta trela baadae jenga box body.. ila kwa kazi mchanganyiko jenga open body. Karibu KIMATARE GARAGE moshi kwa kazi nzuri na ya wakati. Bei ni m19 body rangi na kuirefusha kidogo ili iwe na urefu sahihi na uwezo wa kubeba mzigo mkubwa(volume)
Mkuu weka mawasiliano yenu kama hutajali
 
Pia mchina mafuta inatumia kidogo na vipuri bei ndogo ,kwenye upakiaji wa mchanga inaingia mtoni na sehemu ngumu ,mende haiwezi shughuli ngumu
Yeah, upo sawa kabisa,
Ndio maana sisi tunakimbia hilo game
 
Changamoto kubwa ni simu za usiku
Kivipi mkuu, hizo simu nimeshazizoe hata ilipokuwa kwemye game la mchanga,

Sasa wewe unaona nafuu ni wapi , kwenye mchanga au mkoa kwa mkoa,

Maana kwenye mchanga kwa sababu ya uzito wa mzigo na barabara mbaya , ina ut cost sana kimatengezo,

Matairi kupasuka, kuvunja spring,, kukata hengar, kubamomoa Diff, driving mambar, cross joint, french yale maskio yake, yaani mambo ni mengi huko,

Sasa kama natoa body , yaani tiper maana yake naondoa mfumo wote mpaka pump ya kuinulia tiper,

Sasa hapo naomba ushauri wako , je kwenye lami hayo matatizo yataendelea kuwapo,

Maana target yangu nipate angalau sh mil 2.5 kwa mwezi , ambayo ni kama faida nyingine yote iende kwenye matengenezo na Driver,

Turn boy mimi mwenyewe na driver ni fundi vilevile
 
Asante mkuu.
Nakuongezea, utembee na maeneo itakapofanya Kazi, kama chanika tembea migodi yote ya mchanga then jua gharama za tairi maana kupasuka Kwa mpya Ni kawaida hasa kwenye kukata Kona Kali. Katika hesabu zako uweke na posho za matrafiki hiyo ni given kupata go ahead to smooth Mambo.
Ukipata dereva mzuri na Kazi zipo utasema nilikuwa wapi, ila ugumu upo pia na ujue hiyo 500000 au 400000 kuna muda gari hailali anapanda mtu anashuka mtu, ukipishana.

Ukiona chuma kaishika deiwaka usiwe mkali maana zinachosha Sana Sana mkuu hata uwe tingo 🤣🤣
 
Mchanga unapaswa uwe na roho ngumu Sana asee...changamoto Ni nyingi na presha juu. Sometime route ndefu gari ikikosa Kazi inapumumua kidogo
Kivipi mkuu, hizo simu nimeshazizoe hata ilipokuwa kwemye game la mchanga,

Sasa wewe unaona nafuu ni wapi , kwenye mchanga au mkoa kwa mkoa,

Maana kwenye mchanga kwa sababu ya uzito wa mzigo na barabara mbaya , ina ut cost sana kimatengezo,

Matairi kupasuka, kuvunja spring,, kukata hengar, kubamomoa Diff, driving mambar, cross joint, french yale maskio yake, yaani mambo ni mengi huko,

Sasa kama natoa body , yaani tiper maana yake naondoa mfumo wote mpaka pump ya kuinulia tiper,

Sasa hapo naomba ushauri wako , je kwenye lami hayo matatizo yataendelea kuwapo,

Maana target yangu nipate angalau sh mil 2.5 kwa mwezi , ambayo ni kama faida nyingine yote iende kwenye matengenezo na Driver,

Turn boy mimi mwenyewe na driver ni fund
 
Habari yako mkuu. Hongera kwa kujaribu kuwaza nje ya box baada ya mambo kuyumba, pole kwa changamoto hiyo.
Kwa hiyo gaari yako ni jambo zuri ambalo kimsingi nimekua nikiwashauri baadhi ya watu wenye tipa scania kwani mazingira ya uendeshaji yamekua ni magumu. Gari zinzpitia shurba ambazo hazikuumbwa nazo, inapigika, inakula hela nyingi ya matengenezo na mwisho wa siku zinakufa mapema ama kinachopatikana sio kile kilichotarajiwa.
Kwa upande wa mende, mi nashauri funga box body, irefushe kidogo na ikikaa sawa ikawa na uwezo wa kubeba tai 20 basi ni kiasi rafiki kabisa.
Kwa gari nyingi, by one huwa ndio kazi zake na katika hilo ninashauri beba mizigo inayoenda kupita kwenye barabara ya lami tu, maana ukiipeleka huko Ifakara ndanindani basi huwa sio rafiki sana kwa scania na utakua unaiumiza gari sana. Chagua route yako ya Mwanza japo mzigo wa return huwa ni mchache lakini ukiweka sawa mipango huwezi kukosa 4 hadi 6 kwa mwezi. Na wendi wale wanaotoa kwa malengo huwa ni kama 4M hadi 5 kwa wiki kwa gari mpya. Unampa dereva gari na machine ya EFD unasubiri hela yako mwisho wa mwezi
Kwa sasa hapa Dar gharama za kuweza kujenga box body, kuongeza chasis na ufundi pamoja na vifaa kazi vyote kwa wengi ni kati ya 18M hadi 21. So utajua wewe unafanyaje. Ushauri ni kuwa usiwashushe sana bei mafundi maana hata wakikubali basi uchue kuna ubora utapungua kwenye kazi yako. Ukimpata fundi mzoefu itakua vema zaidi.
Kila la kheri, kwa mende box body ninakuhakikishia huwezi kukosa kazi eti gari ilale hapa Dar kwa siku 3 kisa imekosa mzigo, kikubwa uzingatie route ambazo utakua ukienda ili kuwepo na mzigo wa kurudi.

Kila la kheri.​
Da , Ahsante sana ndugu kwa mawazo yako na kunipa moyo na matumaini, sasa nimepata nguvu, najuta sana Mende yangu kuipeleka kwenye mchanga, ni shida kubwa sana , maana pesa yote ilikuwa inaenda kwenye matengenezo na vipuri,

Barabara tunazoenda huko kwenye mchanga shida kubwa sana , huwezi kumaliza trip moja bora ugonjwa,, kama sio kukata spring basi ni tairi kupasuka,

Ila SCANIA 114 nimeivulia kofia upande Engine,

Nimeshavunja diff ( meno) mala mbili, bei ya diff mil3,
Nimeshavunja jeck ya tiper, bei yake mil 3, yote hayo mwaka mmoja tu,

Kuna tatizo la trafic, hapo ndio usiseme , maana haya magari bora hata daladala,
Hata hivyo tunawashukuru , maana ukisema ugombane nao , gari lenyewe halikosi matatizo.

Mimi target yangu wala sio milioni 4 au tano,
Nikipata milioni 2 tu nitamshukuru Mungu.

Je unaweza kuniamvia kama kwenye rami naweza kupata matatizo kama hayo niliyoorodhesha hapo juu?
Au matatizo yake makubwa ni yaoi hasa.
 
Hizo gari msikae nazo mjini nendeni mikoani ambapo ndio miji inachangamka kazi ni nyingi trips za mchanga unapiga tu za kutosha.

Kwa sasa ni Bora kununua gari za kubebea mchanga na kokoto kuliko gari za abiria ni vile watu bado hawajajua. Mchanga ni Mali sana hasa ukipata gari nzima
 
Da , Ahsante sana ndugu kwa mawazo yako na kunipa moyo na matumaini, sasa nimepata nguvu, najuta sana Mende yangu kuipeleka kwenye mchanga, ni shida kubwa sana , maana pesa yote ilikuwa inaenda kwenye matengenezo na vipuri,

Barabara tunazoenda huko kwenye mchanga shida kubwa sana , huwezi kumaliza trip moja bora ugonjwa,, kama sio kukata spring basi ni tairi kupasuka,

Ila SCANIA 114 nimeivulia kofia upande Engine,

Nimeshavunja diff ( meno) mala mbili, bei ya diff mil3,
Nimeshavunja jeck ya tiper, bei yake mil 3, yote hayo mwaka mmoja tu,

Kuna tatizo la trafic, hapo ndio usiseme , maana haya magari bora hata daladala,
Hata hivyo tunawashukuru , maana ukisema ugombane nao , gari lenyewe halikosi matatizo.

Mimi target yangu wala sio milioni 4 au tano,
Nikipata milioni 2 tu nitamshukuru Mungu.

Je unaweza kuniamvia kama kwenye rami naweza kupata matatizo kama hayo niliyoorodhesha hapo juu?
Au matatizo yake makubwa ni yaoi hasa.
Shukran kwa appreciation mkuu. Gari ni kama binadamu tulivyo, kwenye lami gari inaweza kuharibika pia lakini ni uharibifu wenye nafuu na frequency ndogo sana ukilinganisha na huko kwenye mashimo. Huku ni yale matatizo ya kawaida ambayo eidha yanatokana na kuchoka kwa gari ama zile service za lazima. Lakini kwa sehemu kubwa kuna unafuu, kuna gari ilipokamilika tulianza na trip za huko Ifakara hadi Mlimba na Malinyi. Ni kweli pesa ipo lakini tatizo ni ubovu wa barabara unakula sana gari unakuta gari mpya lakini imechomwa sana. Ila ukipeleka kwenye lami kunakua na nafuu kiasi na angalau hela inaonekana.
Kikubwa hakikisha unapata fundi mzuri na mzoefu wa kuibadili kuwa box body hasa kwenye kuongeza chasis na kuvuta nyuma miguu ya diff la sivyo huwa zinakula sana tairi.
 
Back
Top Bottom