Habari yako mkuu. Hongera kwa kujaribu kuwaza nje ya box baada ya mambo kuyumba, pole kwa changamoto hiyo.
Kwa hiyo gaari yako ni jambo zuri ambalo kimsingi nimekua nikiwashauri baadhi ya watu wenye tipa scania kwani mazingira ya uendeshaji yamekua ni magumu. Gari zinzpitia shurba ambazo hazikuumbwa nazo, inapigika, inakula hela nyingi ya matengenezo na mwisho wa siku zinakufa mapema ama kinachopatikana sio kile kilichotarajiwa.
Kwa upande wa mende, mi nashauri funga box body, irefushe kidogo na ikikaa sawa ikawa na uwezo wa kubeba tai 20 basi ni kiasi rafiki kabisa.
Kwa gari nyingi, by one huwa ndio kazi zake na katika hilo ninashauri beba mizigo inayoenda kupita kwenye barabara ya lami tu, maana ukiipeleka huko Ifakara ndanindani basi huwa sio rafiki sana kwa scania na utakua unaiumiza gari sana. Chagua route yako ya Mwanza japo mzigo wa return huwa ni mchache lakini ukiweka sawa mipango huwezi kukosa 4 hadi 6 kwa mwezi. Na wendi wale wanaotoa kwa malengo huwa ni kama 4M hadi 5 kwa wiki kwa gari mpya. Unampa dereva gari na machine ya EFD unasubiri hela yako mwisho wa mwezi
Kwa sasa hapa Dar gharama za kuweza kujenga box body, kuongeza chasis na ufundi pamoja na vifaa kazi vyote kwa wengi ni kati ya 18M hadi 21. So utajua wewe unafanyaje. Ushauri ni kuwa usiwashushe sana bei mafundi maana hata wakikubali basi uchue kuna ubora utapungua kwenye kazi yako. Ukimpata fundi mzoefu itakua vema zaidi.
Kila la kheri, kwa mende box body ninakuhakikishia huwezi kukosa kazi eti gari ilale hapa Dar kwa siku 3 kisa imekosa mzigo, kikubwa uzingatie route ambazo utakua ukienda ili kuwepo na mzigo wa kurudi.
Kila la kheri.
Da , Ahsante sana ndugu kwa mawazo yako na kunipa moyo na matumaini, sasa nimepata nguvu, najuta sana Mende yangu kuipeleka kwenye mchanga, ni shida kubwa sana , maana pesa yote ilikuwa inaenda kwenye matengenezo na vipuri,
Barabara tunazoenda huko kwenye mchanga shida kubwa sana , huwezi kumaliza trip moja bora ugonjwa,, kama sio kukata spring basi ni tairi kupasuka,
Ila SCANIA 114 nimeivulia kofia upande Engine,
Nimeshavunja diff ( meno) mala mbili, bei ya diff mil3,
Nimeshavunja jeck ya tiper, bei yake mil 3, yote hayo mwaka mmoja tu,
Kuna tatizo la trafic, hapo ndio usiseme , maana haya magari bora hata daladala,
Hata hivyo tunawashukuru , maana ukisema ugombane nao , gari lenyewe halikosi matatizo.
Mimi target yangu wala sio milioni 4 au tano,
Nikipata milioni 2 tu nitamshukuru Mungu.
Je unaweza kuniamvia kama kwenye rami naweza kupata matatizo kama hayo niliyoorodhesha hapo juu?
Au matatizo yake makubwa ni yaoi hasa.