Boyz II Men hili kundi limekufa Tanzania au limeongezwa wanachama?

Boyz II Men hili kundi limekufa Tanzania au limeongezwa wanachama?

Nadhani bado lipo, mzee wa msoga bado analiendesha undercover!

Lowasa alishafeli, kijiti anashikili mbayumbayu kwasasa, naona anamuongoza saa100 kama roboti kwa remote control. Amemsogeza Nchimbi nae awakabidhi mwanae mzee ngada china!

January Yusufu Makamba na Nnape Moses Nnauye walijaribu kuanzisha kundi lao la Boyz II Men wakawahiwa na kusambaratishwa mapema sana!

Adios Amigo!
 
Hili kundi baada ya kutengana na kufariki yule mzee wa kimasai na mmoja kujitoa Je, hili kundi bado lipo au limekufa nalo?
Amebakia Kikwete peke yake na amehakikisha akiwa bado hai anaacha mrithi wake mwingine baada ya Samia kuachia ofisi mwaka 2030, Emmanuel Nchimbi ni muendelezaji wa kundi hilo baada ya Samia kuondoka.

Kikwete anatamani hata akiwa na miaka 100 aendelee kuwa na ukaribu na awamu itakayokuwa ikulu, ni mzee mmoja hapendi kustaafu siasa na kuishi mazima ya mzee anayekula pensheni.

Ni kweli kwamba marais wanamtegemea kwa uzoefu wake lakini na yeye anapenda mno kuhusika na uongozi wa nchi, kuwa sehemu ya walaji wa keki nyingi ya TZ.
 
Nadhani bado lipo, mzee wa msoga bado analiendesha undercover!

Lowasa alishafeli, kijiti anashikili mbayumbayu kwasasa, naona anamuongoza saa100 kama roboti kwa remote control. Amemsogeza Nchimbi nae awakabidhi mwanae mzee ngada china!

January Yusufu Makamba na Nnape Moses Nnauye walijaribu kuanzisha kundi lao la Boyz II Men wakawahiwa na kusambaratishwa mapema sana!

Adios Amigo!
Nape ni mtupu tu kwenye masuala ya uongozi. Makamba uchekibobu umemjaa na anajisahau kwa kudhani anajua kuliko hata hao wanaomuapisha pale ikulu.

Bosi wake alimpigia simu mkurugenzi wa zamani wa TCAA akishangazwa na uamuzi wa Makamba kuliingilia mazima suala ambalo kiutaratibu wahusika wakuu ni wakurugenzi wa mamlaka za anga za Kenya na Tanzania, lengo lake aonekane kwa mheshimiwa kwamba yupo kazini kumbe kwa kufanya hivyo akawa amemkera bosi.

Amerudishwa mwaka huu kwa lengo la kuipigania CCM iweze kushinda uchaguzi lakini haimaanishi kwamba moja kwa moja atakuwepo kwenye baraza lijalo la mawaziri.
 
Back
Top Bottom