Mirija iliyokatwa na kuumiza uchumi wa mabeberu:
1. Safari za viongozi nje ya nchi ambazo ziliwaingizia fedha nyingi.
2. Sheria mpya ya madini ambayo imepunguza faida kwa mabeberu
3. Udhibiti wa wanyamapori hai kwenda ulaya
4. Udhibiti wa madawa ya kulevya
5. Udhibiti wa utoroshaji madini
6. Udhibiti matumizi ya dola nchini
7. Umeme wa uhakika uliozuia mikataba ya umeme wa dharura
8. Udhibiti wa ufichaji pesa nje ya nchi
9. Ongezeko la makusanyo ya kodi hivyo kupunguza utegemezi
10. Kasi ya miradi ya maendeleo
11. Amani na utulivu nchini
Hayo ndiyo yamewachukiza wazungu na kuihofia serikali ya awamu ya tano. Tumuunge mkono JPM kwa maendeleo ya Taifa
Tatizo Magufuli anatunga mtihani mwenyewe na kusahihisha mwenyewe. Nitakupa hapa majibu sahihi hapa;
1. "Safari za viongozi nje ya nchi ambazo ziliwaingizia fedha nyingi."
Kweli amepunguza safari za nje lakini yeye mwenyewe ziara zake mikoani zinakuwa na magari hadi 70-100. Rejea ziara ya Mbeya mwanzoni mwa mwaka 2019. Gharama.ya posho na mafuta na ulinzi ni sawa tu na SAFARI za JK
2. "Sheria mpya ya madini ambayo imepunguza faida kwa mabeberu"
Sheria hii bado ni mapema kukubali kwamba itatupa faida. Tusubiri kwanza ripoti za Benki Kuu
3. "Udhibiti wa wanyamapori hai kwenda ulaya"
Halikuwa suala la kubwa ki-hivyo labda kama walikuwa wanapelekwa kinyume cha sheria . Maana hata kwenye awamu ya 5 wanasema tipunguze idadi ya mamba
4. "Udhibiti wa madawa ya kulevya"
Hapa kiini macho tu hakuna kilichofanyika. Juzi gazeti la The East African limesema Tanzania ni biggest transit hub ya drugs soma hapa
.https://www.theeastafrican.co.ke/news/ea/US-agency-labels-tanzania-east-africa-drugs-trafficking-hub/4552908-5482476-ssbpvl/index.html
Nilichokiona Makonda alipunguza ushindani kwa kukandamiza makundi hasimu ili kundi ambalo yeye ana masilahi lifanye biashara bila competition
5. "Udhibiti wa utoroshaji madini"
Aweza kuwa amefanikiwa kwa 30% maana baso kwenye mkataba ndilo tunainiwa zaidi na si kwa kujenga ukuta
6. "Udhibiti matumizi ya dola nchini"
Hii imekaa vizuri maybe amefanikiwa kwa 80%
7. "Umeme wa uhakika uliozuia mikataba ya umeme wa dharura"
Umeme bado unakatika tu, hakuna tofauti na awamu zilizopita kama kuna improvement basi ni kwa 10%
8. "Udhibiti wa ufichaji pesa nje ya nchi"
Hili halina uhakika na Tanzania haina uwezo kudhibiti.
9. "Ongezeko la makusanyo ya kodi hivyo kupunguza utegemezi"
Hapa ni ZERO kabisa. Uwongo ndiyo umetawala na uchakachuaji takwimu. Angalia deni la Serikali limekuwa kutoka TSH Trilion 38 mwaka 2016 hadi TSH Trilion
53. Kama tungekuwa tunakusanya sana tusingekuwa tunakopa HOVYO.
10. "Kasi ya miradi ya maendeleo"
Kila Rais wa Tanzania amewahi kufanya miradi ya Maendeleo kwa kiasi chake. Huyu anavyofanya ni kutimiza wajibu. Lakini kuna miradi ya HOVYO mingi tu kama Airport ya Chato, Mradi wa Umeme wa Stiglers. Kuna miradi ambayo siyo Kipaumbele cha Taifa na miradi mwingine haijafanyiwa feasibility study. Huwezi kuelewa leo ila tuombe uzima tuwepo hadi 2030
11. "Amani na utulivu nchini"
Nafuu wakati wa Mkoloni kuliko sasa, amani unayoiongelea imekuwa kiini macho. Awamu zilizopita POLISI walikuwa wanapambana na majambazi wanao hatarisha usalama wa maisha na mali za wananchi. Awamu hii POLISI wanaitwa WATU WASIOJULIKANA, wanaua watu Mkuranga, Kibiti na Ruffini. Wanataka akina Roma na Mdude na Mo Dewji. Wanajeruhi Tundu Lissu, wanaua Ben Saa8 na Azory Gwanda.
Watanzania hawawezi kuongea kwa uhuru kwenye nchi yao halafu unasema kuna amani?