BRAZIL: Mtanzania, Felix Alphonce Simbu ashika nafasi ya 5 katika Marathon za Olimpiki

Wivuu wakibongoo ndioomaana mnapigana misumariii
 
Kunawatuu wakonje sikuzote wanaogopa hata kujenga kibanda kwao sababu ya misumari ya watanzania wakijenga wanaweza wasilale ndani
 
Hongera sana Simbu, japo hukupata medali lakini umeonesha nia ya kuitetea nchi yetu.
 
Unafiki wetu basi , kauli hapa kazi tu imepewa uzito zaidi ya tukio la Simbu kushinda nafasi ya tano. Nimeshangaa hadi Azam tv imeipa habari ya mtangazaji kusema hapa kazi uzito usiostahili. Mtangazaji Mkenya hivo kauli hapa kazi sio ngeni kwao ,ni majirani wetu.
 
Acha kubeza mbona wewe hukwenda mwakani nenda wewe km unadhani kufukuza upepo ni rahisi
 

..wanatakiwa wafanye mazoezi eneo ambalo lina muinuko (high altitude).

..hewa ktk maeneo hayo ni nyepesi hivyo mwanariadha hujenga stamina zaidi.

..kambi ya riadha kwa Tz inatakiwa iwe maeneo ya Mbulu, Kilimanjaro, au popote pale penye muinuko.

..baada ya kutoka huko kambini walitakiwa wa-simulate tena hiyo marathon ktk eneo ambalo kuna hali ya hewa kama ya Rio.
 
hatari
 
Anajua tu kusupport wa kina wema na vi app vyao uchwara badala ya kupanga mikakati ya vijana wetu kwenye michezo.
 
Sasa tumezidi. Fikiria kijana mdogo anayefuatilia mijadala kama hii...

Anafuatilia tunavyomshangilia na kumsifia mkimbiaji aliyeshindwa kupata medali Olimpiki kwa kisingizio kashika nafasi ya tano na hivyo kajitahidi!

Anafuatilia tunavyoshangilia na kuwasifu polisi wetu ambao badala ya kutulinda tukidai haki zetu wanatupiga risasi na kutuua kwa kisingizio cha kudumisha amani!

Anafuatilia tunavyomshangilia, kumsifia na kumtetea kiongozi wetu uchwara anayevunja katiba ya nchi kwa kisingizio cha hapa kazi tu!

Anafuatilia utumbuaji majipu huku EPA, IPTL, Richmond, Kagoda, ESCROW, majumba ya serikali, kivuko chakavu, Meremeta, Lugumi n.k. zikiwa pale pale!

Anafuatilia tunavyokuwa wepesi kuridhika na hali duni huku hazina tunazo, rasilimali tunazo, watu tunao, ardhi tunayo n.k. kwa kisingizio tu taifa changa!

Anafuatilia jinsi baada ya nusu Karne, watu wale wale, chama kile kile, Katiba ile ile n.k. lakini hapo hapo bado tunatumaini kupata matokeo tofauti!

To us Tanzanians good is enough even where better is possible. Naona wapo vijana hawajui tuliwahi kuvuma kwa riadha, wanashangilia failure!

Je huyu kijana mdogo atakuwa na malengo gani maishani? Kwamba hata usipofanikiwa kimaisha watakuwepo watakaokupa hongera?

Hakika tumelaaniwa...!
 
Hivi ninyi mnaomponda kijana Simbu mna akili timamu? Au kila sehemu mnaweka siasa? ....kabla ya kuilaumu serikali tukumbuke hivi vipaji tunaishi navyo majumbani mwetu. Jiulize ni lini ulifanya kitu hata kidogo kuendeleza kipaji hapo kwako? Mnajua Simbu alipoanzia hadi kufika hapo alipofika? Kwa taarifa yenu ni kuwa hao wanariadha hupitia maisha magumu sana wakati wakitafuta kufanikiwa kama ilivyo kwa vipaji vingine. Wengi wao hukatishwa tamaa na watu wao wa karibu kwasababu wanariadha ni nadra sana kufanya shughuli zingine ngumu maana hutumia muda mrefu kupumzika baada ya mazoezi makali. Kiufupi kijana Simbu kaanzia mbali hadi kufika hapo. Tumtie moyo apambane zaidi na kwasababu bado umri wake mdogo huenda akafanya makubwa zaidi. Mnaoponda MLAANIWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…