Tanzania yaiua Zimbabwe 15-0 'Sauzi'
Na Somoe Ng`itu
7th June 2010
[FONT=ArialMT, sans-serif]Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania iliendeleza kutoa 'dozi ya vipigo katika mashindano ya kimataifa ya Copa Coca Cola baada kuisambaratisha timu ya vijana ya Zimbabwe kwa 'mvua' ya magoli 15-0 katika mechi iliyofanyika kwenye jiji la Johannesburg jana jioni.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mshambuliaji Thomas Ulimwengu alifunga magoli matano katika dakika za 6, 9, 12, 21 na 22, na magoli mengine yakaongezwa na Omega Seme (dk.10), Ali Thabit (dk. 27, 31, 63), Jerome Lambele (dk.44, 51, 57), Ibrahim Rajab (dk. 49), Hamisi Mroki (dk59)na Himid Mao aliyefunga katika dakika ya 61. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kipigo hicho kilikuwa ni cha nne kwa Zimbabwe katika mechi zao nne baada ya kuchapwa 5-0 na Nigeria, 5-0 dhidi ya Malawi na 15-0 kutoka kwa wenyeji Afrika Kusini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kabla ya ushindi wa jana jioni wa 15-0, Tanzania iliwashangaza mabingwa watetezi Nigeria, kwa kuwashushia kipigo cha magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika asubuhi jana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tanzania ilianza kampeni zake kwa kuichakaza timu ya vijana ya Malawi kwa magoli 11-0 juzi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Magoli yaliyoipa ushindi timu hiyo ya Tanzania katika mechi yao dhidi ya Nigeria jana asubuhi, yalifungwa na Lambele Gerome katika dakika za 27 na 47.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na matokeo hayo, timu ya Tanzania imekuwa gumzo katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu 12. Tanzania itamaliza mechi zake za hatua hiyo ya makundi leo asubuhi dhidi ya wenyeji Afrika Kusini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kiongozi wa timu hiyo, Ahmed Mgoyi na makocha wa timu, Rodrigo Stockler na msaidizi wake, Sylvester Marsh, wameliambia gazeti hili kuwa wachezaji wamefanya juhudi kuhakikisha wanashinda mechi zote.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE