Kwa habari nilizozipata toka kwenye chanzo cha kuaminika ni kwamba tiketi za laki 2 zimeisha, za elfu hamsini zimeisha pamoja na elfu thelathini pia nazo zimeisha.
Nasikia baadhi ya watu wamezinunua kwa wingi, e.g. Yusuf Manji (for Yanga fans), Azim Dewji (for his staff at Simba Plastics), NMB (main sponsor), Serengeti (Sponsor), na makampuni mengine mengi. Wengi wa hawa watu wameshalipia tayari, hii ni kwa mujibu wa chanzo changu kilichopo pale TFF!!
Binafsi nimeanza kuingiwa na woga wa kuikosa mechi hii!!
Hivi kuna haja gani ya TFF kutangaza kuanza kuuza tiketi kesho mchana huku tayari wameshaziuza tayari baadhi ya tiketi kupitia mlango wa nyuma? Hii ni sawa kweli????