natanguliza:kwa maoni yangu.
wajameni inaniuma sana nikifikiria kuwa wapo ndugu zangu kule kijijini hawana maji, umeme, madawa na hata vifaa vya shule ila serikali inadiliki kugharamia ujio wa timu ya brazil kwa tsh 3 bilion,pia inauma kuona hata malimbikizo yetu ya mishahara hatulipi ili tuwasidie hao ndugu zetu.mbaya zaidi kiingilio cha mchezo huo ni tsh 200,000 hadi tsh 50,000 ambacho ni zaidi ya kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi au hata akitoa hio tsh 50,000 mwezi huu atakula matembele mpaka yaote tumboni.kwa hio ni mechi ya walionazo tu, sisi walala puu tulie, kweli
kwa upande wangu sijaona faidi ya ujio wa timu hii kiuchumi kwani wabrazili hawajagi kutalii kwetu, watalii wengi wanatoka europe na si hivyo tu bali tunatakiwa kujitangaza kimataifa kwa kutumia tuvuti(website) na maonyesho kwenye balozi zetu wala sio kwa mpira ambao hata dstv inayoonekana dunia nzima hawaonyeshi hii maechi.
Haya ni matumizi mabaya ya hela za serikali kwa kupenda misifa ya kijinga, hata hao wanaotupa misaada watashangaa na kutuona mapopopo.
Tumechoka na udhalimu huu,mwaka huu lazima tuing'oe serikali ya ccm jamani
mfurukutwa