Brazil to play Tanzania in a friendly

Brazil to play Tanzania in a friendly

Mbona viti vingi ni vitupu? Nilisikia kuwa ticket zaidi ya 60,000 zilikuwa zinategema kuuzwa. Je uwanja ule unachukua watu zaidi yo 60,000?
 
Taifa Star leo watabugia magoli kwa Uchahe wa Magoli Watafungwa Taifa Stars 0 - 5 Brazil Taifa Star Wanafundishwa Mpira leo na Baba zao Wa Brazil.
 
Kumbe walifungwa na Rwanda sasa ndo watawafunga Brazil?
 
TBC1 wanaonyesha mpira naona mkuru kawaambia wa Chalinze nao wanataka kuona mechi
 
Mie naangalia kupitia chanel moja ya waraabu,naona mtangazaji unauita uwanja wa ben mkapa,kwani tayari mmeubadilisha jina uwanja wetu.
 
Nafikiri TV za kulipia nyingi wanaonyesha huu mchezo. Kuna mshikaji wangu aliniambia ataangalia kwenye EUROSPORT 2. Wanafaidi wenye madishi yao na hii ina maana kuwa nchi nyingi wanaangalia ila sidhani kama TV za taifa/Za bure wataonyesha hii mechi.

Wananchi wamefanya safi sana kugomea mechi. Hamna hata tangazo la Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, ovyoooo.

Hilo Tangazo la SERENGETI utafikiri limeandikwa kwa kutumia KISAMVU, chafu kabisa na halionekani. Sijui Idiot gani alitengeneza.

Ngasa naona anajiuza safi sana na anacheza na wenzake. Yule mwenye nwele ndefu (kasuka) anacheza kama kalazimishwa. Anajiona MATAWI sana wakati hapo ndani kuna akina KAKA wapo simple na friendly kabisa.

Naona poa tu sikupoteza hela zangu kununua ticket kwenda Dar na kununua ticket ya mpira. Hela ya ticket ntawapa masikini.

Sikonge this game is very interesting though vijana wetu wanajitahidi though finishing yao ndiyo ipo very poor...Ila wasipoangalia HADI DAKIKA 90 SINAISHA NI 4-0....

AlAFU uwanja upo empty kabisa naona watu wamenunia game....lakini come to think about this...hii mechi ingekuwa investment nzuri sana...maana hapa naangalia live na matangazo kibao tuu online kumbuka lazima kwenye haya matangazo lazima tanzania tuna commision yetu na kila tv itakayoonyesha lazima tanzania tulipwe tunaweza make so much money kuliko hata tuliyolipia hii mechi ya Brazil kuja kucheza na Tanzania....Sema tuu one thing ni kwamba Mafisadi watajigawia....Na umasikini bado unaendelea....
 
Nafikiri tunawatangaza marefa wetu ,yaani wanavyoenda mbio na mbia kuutangaza uwanja ili tuweze kuchezesha kombe la dunia kwa miaka ijayo ,uwanja una nyasi kibao ,tatizo refa anazungumza na waburazili kiswaili ,hongera kocha maxima kwa kuileta burazili apo bongo.
Nasubili jamaa watakavyonyang'anyia jezi.
 
he heeeeeeeeee Mkwere hapo anajisikiaje jamani? Mashimo oops sorry Max nani tena naye anakereka kiaina ka vile amewanoa sana hawa dogo. Hawa walitakiwa wawe kama wale watoto wetu kule Kopa Coca Cola! Chapa mtu 15, 11 yaani ni raha tu lol
 
nashukuru sana mkuu ninaungalia live hapa kwenye ESPN VIVO. Ubarikiwe duu
 
Mhh goolkeeper naona bora wangemtoa tu kabisa maana sioni anachofanya
 
naomba Cv ya huyu kipa wetu mharami mohamed please na maximo alimuonaje huko nje ya nchi au alitumia kuambiwa?


tukiacha kucheza kama mchangani kwamba kila mtu anataka kufunga yeye tunaweza kupata goli la kufuta jasho la walipa kodi lakini tukiendelea kila mtu anataka kupata sifa ya kupata goli lake zidi ya Brazil ni noma.
 
Alafu huyu namba 14 ni mnene sana alafu mzito
 
Mbona viti vingi ni vitupu? Nilisikia kuwa ticket zaidi ya 60,000 zilikuwa zinategema kuuzwa. Je uwanja ule unachukua watu zaidi yo 60,000?

mwalimu uwanja is only half full (or empty) na kama Brazil imeshindwa kuujaza huo uwanja sijui timu gani duniani inaweza kuujaza!!
 
Back
Top Bottom