Brazil to play Tanzania in a friendly

Brazil to play Tanzania in a friendly

Mechi muhimu sana hii kwa taifa letu! Tumeandika historia...asante TFF na CCM
 
Jehovah tusaidie tupate watumishi wataolitumikia taifa kwa uwazi na moyo wa kuleta mabadiliko mazuri na sio usanii na ubabaishaji
watu wasio wezi na kutuibia watanzania kiasi cha kushtusha mioyo,watumishi wataoonyesha moyo wa kizalendo na kuilinda nchi
watumishi wataochukua mawazo ya watanzania walio wengi ambayo yana akili na ushauri mzuri tu na kuyafanyia kazi (kama hili game la leo nani kawashauri?)
watumishi watao.....maneno yananiishia nikiwaza hivi!!!
puuuuh!
 
Nasubiri mapato manake uwanja ulikuwa empty sana leo
 
Jamani si maanishi kipigo cha 5 kwa 1; la hasha bali mambo yaliyojitokeza humo ndani. kipigo tulikitarajia

1) wakati wimbo wa Brazil inapigwa - jamaa wa ile screen kubwa alikuwa bize kutuonesha ngoma za kwao na ujumbe wa kilimo kwanza.

2)wimbo wa Tz CD yake kukwama kwa seconds kadhaa mpaka wakabadilisha - si bora wangeita brass band

3)jamaa wa ile big screen kutufundisha ms exce & power point na jinsi ya kuzungusha cursor kwenye screen muda wote, utafikili (kwa kweli nilihisi kukereketwa na kitu moyoni muda wote)

nashindwa kujua kama hawa jamaa ndio walikuwa wanajifunza jinsi ya ku-operate ile screen aibu tupu. Nguvu kubwa walitumia kuitangaza hii match bila kufanya maandalizi ya vitu vidogo kama hivi ambavyo ni vya muhimu sana.

NB: nahisi lengo halikutimia , na isingekuwa Manji hali ya mambo ingekuwa mbaya sana kwa Tff, idadi ya waliouzulia ilikuwa ni ndogo sana kama 1/3 ya uwezo wa uwanja.
 
Level of income in mislead planning nyingi sana, nadhani itakuwa fundisho wakati mwingine they want everything but they just miss out hizo tiketi zilizoisha ni zile alizonunua manji kwa pesa yetu
 
wachezaji wetu hawana stamina kabisa.Tanzania hakuna Gym?trainers kazi yao ni nini?

Wamecheza mechi mbili back to back, jumlisha na uchovu wa safari. Hakuna planing kabisa Bongo!
 
duh wakuu ndo kwanza naingia nyumbani toka mihangaikoni,jinsi nilivyokuwa nimechoka háta kuwasha laptop sikuwa na hamu.haya niangalie tv natafuta programu itayonivutia mara eurosport hiyo,khe nashangaa naona friend match report TANZANIA 1-BRAZIL- 5.mweeeh!nilishtuka kama nimeskia bomu la mbagaraaa,hivi tumewalipa bei gani vile waje watutie madole??na hii itakua idea ya MAXIMO hii maana si mumempigia debe hafai?kaamua kutulipizia na timu ya kwao,aargh mi sikubali bana kuanzia leo nashabikia BURAZIL HOYEEEEEEE,TENGA HOYEEEEEEE,UTALII HOYEEEEEEEE,:target:ngoja nikalale sasa maana naona wazimu unataka kunishika kwa hasira.
 
VIDEO - Tanzania Yabugizwa 5-1 na Brazil, Maximo Apigwa Chini
4595390.jpg

Mwarami Mohamed kipa wa Tanzania akiwa amekaa chini baada ya kutunguliwa na Wabrazili Monday, June 07, 2010 8:10 PM
Mpira umeisha na matokeo ni ya kusikitisha, Tanzania ambayo jana ilifungwa 1-0 na Rwanda leo imepokea kipigo kingine cha nguvu toka kwa Brazili kwa kubamizwa 5-1. Wakati huo huo kibarua cha Maximo kimeota mbawa na sasa nafasi yake itachukuliwa na kocha toka Denmark. Tanzania imeshindwa kutamba mbele ya Brazili na kukubali kubamizwa mabao 5-1 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kutokana na viingilio vikubwa, uwanja haukujaa kama ulivyotarajiwa na bila shaka TFF itakuwa kwenye mahesabu makali ya kurudisha pesa zao walizotumia kuwaleta Brazili.

Kocha wa Brazili, Dunga aliingiza kikosi chake kamili cha wachezaji 11 akikosekana kipa wake namba moja Julio Cesar ambaye aliumia mgongo katika mechi na Zimbabwe ambayo Zimbabwe ilifungwa 3-0.

Tanzania ikicheza mbele ya rais Jakaya Kikwete ilionyesha mchezo mzuri na kujaribu kuwamudu Wabrazili lakini makosa madogo madogo na udhaifu wa kipa Mwarami Mohamed ndiyo yaliyopelekea Tanzania kubugizwa magoli mengi.

Mshambuliaji hatari wa Brazili, Robinho aliifungia Brazili magoli mawili wakati Kaka naye baada ya takribani mwaka mzima akiwa na ukame wa magoli katika timu ya taifa, alifanikiwa kuzingisha nyavu za Tanzania.

Kiungo wa Brazili, Ramires aliyeingia uwanjani kipindi cha pili, aliifungia Brazili magoli kuhitimisha karamu ya magoli ya Brazili.

Goli la Tanzania lilifungwa na Jabir Aziz kwenye dakika ya 87. Jabir alienda hewani na kuunganisha kwa kicha mpira wa kona na kumuacha kipa wa Brazili, Gomes akigaragara huku mpira ukitinga nyavuni.

Pamoja na kufungwa na Brazili, Tanzania imekuwa ndio nchi ya kwanza kuchafua rekodi ya Brazili ya mechi sita bila nyavu zake kutingishwa. Timu ya mwisho kuzamisha mpira kwenye nyavu za Brazili ilikuwa ni Bolivia mnamo oktoba mwaka 2009.

Wakati huo huo TFF imemtema kocha wa Tanzania, Marcio Maximo ambaye nafasi yake sasa itachukuliwa na kocha toka Denmark, Jan Borge Poulsen mwenye umri wa miaka 64.

Poulsen ameingia mkataba wa miaka miwili na ataanza kuinoa rasmi Taifa Stars kuanzia mwezi wa nane.

Kama ungependa kujikumbusha matukio muhimu ya mechi na magoli yote sita katika mechi hii, basi angalia VIDEO hii chini.


VIDEO - Tanzania 1-5 Brazili Bonyeza hapa kuiona Video NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.






 
jamani mimi nahisi wa tz walicheza vizuri tu lakini goakeeper na central defenders wametuangusha .ninasema haya kwa ushahidi wa match stats
TZ
shoot on goals - 18
corner -7
ball possession-39%

BRAZIL
shoot on goals-20
corner kicks-6
ball possession-61%

najua tumefungwa lakini wachezaji walijitahidi sana especially ngasa.vile vile tuzingatie kwamba brazil kiwango chao ni kikubwa mno .vile vile brazil hawajaruhusu goli tokea october mwaka jana.
kuhusu TFF kuilipa brazil 2.5 dollar hiyo vile vile si tatizo kwasababu inaonekana tff nao wameuza right ya kuuza game kwa vituo vya television .kwa hesabu za haraka naona wamepata faida more than $2 million .kumbukeni kwamba hii game imeonyeshwa karibu nchi nyingi za ulaya na arabuni pamoja na america .
jambo lililonitia uchungu ni uwekaji wa matangazo ni mbovu kabisa.watu wanaoshughulikia utalii inaonekana wamelala kabisa .
 
duh wakuu ndo kwanza naingia nyumbani toka mihangaikoni,jinsi nilivyokuwa nimechoka hбta kuwasha laptop sikuwa na hamu.haya niangalie tv natafuta programu itayonivutia mara eurosport hiyo,khe nashangaa naona friend match report tanzania 1-brazil- 5.mweeeh!nilishtuka kama nimeskia bomu la mbagaraaa,hivi tumewalipa bei gani vile waje watutie madole??na hii itakua idea ya maximo hii maana si mumempigia debe hafai?kaamua kutulipizia na timu ya kwao,aargh mi sikubali bana kuanzia leo nashabikia burazil hoyeeeeeee,tenga hoyeeeeeee,utalii hoyeeeeeeee,:target:ngoja nikalale sasa maana naona wazimu unataka kunishika kwa hasira.

omba msamaha ..au tumia umoja hapo na sio plural
 
jamani mimi nahisi wa tz walicheza vizuri tu lakini goakeeper na central defenders wametuangusha .ninasema haya kwa ushahidi wa match stats
tz
shoot on goals - 18
corner -7
ball possession-39%

brazil
shoot on goals-20
corner kicks-6
ball possession-61%

najua tumefungwa lakini wachezaji walijitahidi sana especially ngasa.vile vile tuzingatie kwamba brazil kiwango chao ni kikubwa mno .vile vile brazil hawajaruhusu goli tokea october mwaka jana.
Kuhusu tff kuilipa brazil 2.5 dollar hiyo vile vile si tatizo kwasababu inaonekana tff nao wameuza right ya kuuza game kwa vituo vya television .kwa hesabu za haraka naona wamepata faida more than $2 million .kumbukeni kwamba hii game imeonyeshwa karibu nchi nyingi za ulaya na arabuni pamoja na america .
Jambo lililonitia uchungu ni uwekaji wa matangazo ni mbovu kabisa.watu wanaoshughulikia utalii inaonekana wamelala kabisa .
hapo umesema mkuu wale wazee wa watu washachoka waende zao wakapumzike jamani
 
Kwa taarifa yako ameongezewa mkataba.....maana analipwa na Ikulu

Ndiyo matatizo ya watu wasiojua lolote kuhusu mpira kujiingiza katika maamuzi yanayohusu mpira...Sasa Ikulu na kandanda wapi na wapi!!!! Huyu kocha wa halaiki kule kwao maana hata kujulikana katika anga za soka ndani ya nchi yake hajulikani sijui ni nani aliyemleta nchini....kama kawaida yetu tumeliwa kwa mara nyingine tena.
 
Ndiyo matatizo ya watu wasiojua lolote kuhusu mpira kujiingiza katika maamuzi yanayohusu mpira...Sasa Ikulu na kandanda wapi na wapi!!!! Huyu kocha wa halaiki kule kwao maana hata kujulikana katika anga za soka ndani ya nchi yake hajulikani sijui ni nani aliyemleta nchini....kama kawaida yetu tumeliwa kwa mara nyingine tena.

Leo ndio send off or talaka party ya Maximo, lawama lawama basi. Tuone huyo mdenmark sijui atatufikisha tunapotaka kwenda kisoka.
 
uwanja ulikuwa mweupeeeeeeeeeeeeeee...................ndio faida ya kuweko viingilio visivyokuwa realistic.

80000 kwa viti vya orange?! ......kwa mtu wa kima cha kati mwenye mshahara wa laki 3!

30000 kwa viti vya blue?! ...........kwa mtu wa kima cha chini anaelipwa mshahara wa laki moja na nusu!
 
Ukiangalia statistics utaona TZ ilikuwa na chance kubwa ya kufanya vizuri kuliko Brazili. Kama Brazil walikuwa wana possession ya zaidi ya asilimia 60 na kuweza kujaribu kulenga goli mara 20 na Tanzania ikiwa na possession ya asilimia 39 na kujaribu kuliona lango mara 18 (wakiwa na kona moja zaidi ya Brazil) ni wazi kuwa tatizo letu basi lilikuwa kwenye defense zaidi kuliko ushambuliaji. Kwa yeyote aliyeangalia atakumbuka kuona jinsi ambavyo tulishindwa kumalizia. NI kama tulikuwa tunaona aibu hivi kuwafunga Brazil wakati wao walikuwa very serious watufunge.
 
mwanakijiji ..............unafikiri brazil ilitumia nguvu zake zote hasa kwenye ile mechi?
 
Back
Top Bottom