Breakfast yako kuu kwa sasa ni ipi?

Breakfast yako kuu kwa sasa ni ipi?

Na pepsi baridi
 
Attachments

  • IMG_0730.jpeg
    IMG_0730.jpeg
    3.4 MB · Views: 5
Mimi nakula ugali asubuhi saa 4 mchana napiga ndefu mpaka usiku hapo msosi wowote nikiukuta home twende kazi.

Ila maziwa fresh ya baridi asubuhi muhimu sana friji lisikose paketi za Tanga fresh.
 
Supu ,chapati tatu mayai ya kukaanga 2 miago 5 then nashushia na juisi hizi za local za kutengeneza yani apo mchana nacheua tu
 
Ndio maana matumbo yanavimba kama mna mimba.

Asubuji mihogo
Mchana ugali
Usiku wali

Sasa utakuaje na afya kwa kula wanga uliotukuka na misukari.
Ukiambiwa ule samaki, ngano, kuku n.k unasema watonga na bajeti.

Kiruuuu.
Ngano sikushauri mkuu, hii ngano yetu iliyokobolewa haina faida yoyote
 
Wengine kila asubuhi chai Mkate wengine hupendelea Viazi mviringo kila asubuhi na wengine kiporo cha wali.
Mimi Kwa mazingira ninayokuwepo asubuh siwezi kukwepa Mihogo Kama mnavojua cassava Kwa sasa ndo ipo on chart bila kuchoka Maharage na Juice ya passion. Kwanini kwanza navikubali vitu hivo

Juice ya Passion ina vitamini C nyingi, ambayo ni antioxidant inAsaidia kulinda mwili .Vitamini C inaongeza kinga ya mwili, mwili unanyonya madini ya chuma zaidi kutoka kwa vyakula vinavyotokana na mimea, so juice yangu hio inaboresha uwezo wa mwili wa kupambana na maambukizi mwilini.

Ukija kwenye cassava hapo una kalori nyingi na wanga nyingi na vitamini na madini pia. Na wenyewe una vitamini C, thiamine, riboflauini n. k ingawa Kati ya muhogo na kiazi kitamu ambacho kipo juu Kwa nutrients ni kiazi kitamu.

Maharage hapo ndo penyewe sasa uhakika kwenye Protini ambayo ni kirutubisho muhimu kutengeneza mwili pamoja na folate. Maharage ni mazuri mnoooo Kwa afya ya moyo.yanapunguza hatari ya saratani,kisukari na mwisho kabisa hayana cholesterol.. Me daima nitakula Maharage hakuna cha vidonda vya tumbo wala kiungulia. Me nayatandika Mpaka mwisho.

Tubadilishane uzoefu we unakula nini asubuhi mara nyingi nyingi.

Starch na viazi vitamu every day
 
Mimi asubuhi nachukua bamia kumi zinakatwa vipande vidogovidogo, vitunguu maji 2, vitunguu Swaumu punje 6 vinakatwa vipande, tangawizi kidogo, hoho 1, na pilipili kipande kidogo.

Baada ya hapo naweka maji kiasi jikoni na chumvi Kwa mbali na mafuta ya kupikia nusu kijiko, maji yakichemka natia huo mchangangiko wangu wote wa mbogamboga na viungo vyote Kwa pamoja nauacha Kwa muda wa dakika 5 mpaka 10 vinakua tayari Kwa kula. Hapo Kwa pembeni nakuwepo na nusu lita ya maziwa fresh yaliyochemshwa vizuri. OVA

NB: Siku nyingine naweka karoti na biringanya badala ya bamia.
 
Mchana kula mlo kamili wenye wanga na protein, usiku ukimaliza kufanya MAZOEZI ya kuuweka mwili fit, unakula full plate ya mchanganyiko wa matunda pekee au unaweza ukaifanya kama salad unachanganya na mbogamboga na mbegu jamii ya karanga Kisha unapata tangawizi yako kikombe kimoja.

[emoji123][emoji123]NENDA KALALE NA MKEO[emoji160] ATAIMBA NYIMBO ZOTE ZA FURAHA.
 
Mie mama wa nyumbani ratiba yangu ni hii
Jumatatu napika mkate wa ufuta na maziwa
Jumanne : viazi vya kukaanga kachumbari na chachandu
Jumatano: mihogo mixer viazi na karanga za kuchemshwa
Alhmisi : maandazi na rost inategemea mzuka wa siku hiyo
Ijumaa : kiporo cha maharage na wali sababu alhamisi nina ratiba ya kupika maharage, kunde au choroko
Jumamosi: supu ya sangara na ndizi
Jumapili : supu ya kuku na viazi vya kuchemshwa tunachovya na mbegu za ufuta au mbegu za maboga zinakaangwa zinatwangwa utamu wake ni balaaa.. Mwanangu mmoja hapendagi hiyo mixer so huwa natoa kipande cha kuku namkaangia na viazi na kachumbari.

Uzani wa kilo zinasomaje mkuu?
 
Back
Top Bottom