Breaking news: ndege yatua na tumbo Kilimanjaro airport

Tunafuatilia taarifa kutoka kwenye mamlaka husika kuhusu ajali ya ndege aina ya Embraer 120 iliyotua kwa tumbo katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro jioni ya leo.
Kwa sasa hatuna taarifa nyingine .
ok.🐒
 
Au walikuwa kwenye mazoezi ya uokozi hiyo
 
Mshana jr una vibwenga,ndege kutuwa kwa tumbo?
Hii ndo naisikia leo

Uwe comedian
Ndege kutua kwa tumbo (Belly Landing au Gear-Up Landing). Hutokea pale ndege inaposhindwa kushusha magurudumu (landing gear) au kuyafunga vizuri kabla ya kutua. Sababu zinaweza kuwa hitilafu ya mfumo wa hydraulic au umeme, kuharibika kwa mfumo wa magurudumu etc.

Rubani hufuata taratibu za dharura, huwasiliana na udhibiti wa safari za ndege (ATC), na huandaa ndege kutua kwa tahadhari kadiri inavyowezekana. Tahadhari na maandalizi ya vifaa vya uokozi hufanyika kwa haraka ikiwa ni pamoja na utayari wa magari ya zima moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…