Kwanini mliachana au uli amua kukiwasha. Kwanini
Ngoja ni rudi nyuma kidogo....
Baada ya kukutana na huyu mrembo kuna kitu nilihisi ambacho ni ngumu kueleza kwa lugha tulizonazo, ila kuna kama JE-DAVU flan nilihisi ambayo haielezeki... nimekumbana na pisi kali sana na tuliachana ila kwa huyu, nahisi upendo haukutokana na muonekano wa nje nahisi. Ingawa alikua kisu pia, so kama kawaida yangu sikutilia maanani hizo hisia nikawa najivungisha kama si care sana.
Siku 3 tu za kumjua nikama vile tumejuana maisha🤣 kulikuwa na chemistry flan ambayo ilinifanya nilewe kabisa nikawa vulnerable asee sikuwahi kujihisi nimependa kiasi kile, kwenye shoo nilijihisi peponi, hata productivity yangu kazini ilipungua sometime nadoji siendi nasingizia ugonjwa, ili tu nispend time naye. Mpk hapo mtu alikua haniambii kitu maana huu upendo ulikua next level..
Kupunguza stori, kwa mara ya kwanza nilihisi uhalisia wa kukutana na mtu sahihi. Wengine ilikua nikishaona ya ndani attraction kwisha. Ila huyu nilimpenda beyond that, nilitaka kabisa awe wa kufa kuzikana. Alinifanya nisiwe na tamaa tena, kwa madem wengine. She was my perfect match.
Ila wakuu kuna kitu kinaitwa
right person wrong timing.. kuna vitu viko nje ya uwezo wetu. Sitaki kuexpose nini kilitokea mpk kuachana ila kaeni mki jua mpk mungu aamue huwezi kuwa na mtu sahihi. Mtu sahihi huja baadae kabisa mpk uwe emotionally strong kucontrol desires.
Nahisi labda hakuona intensity ya upendo nilokua nao kwake? Sijui, labda alipitiliza kupenda mpka kuumia? Maana upendo halisi hufungua moyo na kuufanya uwe vulnerable? (It opens old wounds!) Sijui ila ni dhahiri tulipendana. Ilikua kama addiction hata tukizozana asubuhi, jioni sex kama kawa... so mimi nilihisi hii itakua sio sawa. Ile jeuri ya kila mmoja wetu ilikua inatutafuna na nilitaka kuondokana na huu upendo wenye utamu na uchungu ndani yake. So nika end things japo nilijua kabisa itanichukua mda kuja ku get over her. Ilinifunza vitu vingi kujihusu na jinsi nilivyochukulia mahusiano na wanawake pia.