BRELA system yenu ni kuharibu kazi au mmetega rushwa?

BRELA system yenu ni kuharibu kazi au mmetega rushwa?

Volcano Temperature

Senior Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
106
Reaction score
86
Ukiona hiyo System ya Brela ilivyopambwa na kuandikwa vitu vya maana.... Unaweza kufikiria kuwa vilivyomo ndani vina akili sana kumbe Uozo mtupu.
Uncle Magu pitia pale Brela kumbe unatupiwa lawama nyiiingi, kuhusu biashara - Wahuni wameisha jenga ngome yao pale Brela. wako kwa ajiri ya Maslahi yao, matumbo yao tu pale wala sio kazi ya Umma, Brela imefikia hatua kuombwa rushwa ni hadharani tena bila uoga kabisa.

Pole kijana uliyekumbwa na kadhia hii .... Wanasheria wa ma-kampuni najua mnajisikiaje na Brela yetu (Asanteni kwa kuliweka hili wazi)

BRELA NI SHIDA - NI USEMI ULIOZOELEKA SANA KWA WANASHERIA WA MA-KAMPUNI WANAOSHINDA PALE BRELA KWA AJIRI YA SYSTEM

Hivi huyu Waziri mpya wa Viwanda na Biashara - Joseph George Kakunda anajua kama Brela iko chini yake na anatakiwa kufanya kazi zake pale Brela.
au hata hajui majukumu yake ni nini ?

Mkurugenzi Mkuu wa Brela ndio hopeless Kabisa.... Unaingia Kazini kila siku lakini wateja wako ambao ndio wafanya Biashara na walipaji kodi wakubwa hutaki kukutana nao.... What the Hell are you doing in the Office au ndio you have team it up to solicit bribe from Investors.

Nashangaa sana kuona System iliyowekwa Brela imegeuka kuwa kikwazo kikubwa kwa wafanya Biashara, Ku-update information kwenye System badala iwe jambo la nusu saa umemaliza sasa limekuwa Jambo la Mwaka Mzima, na huwezi fanya kitu kingine hadi umemaliza ku-update information kwenye System, hivi mnajua mnainyima serikali kodi kiasi gani kwa ujinga wenu huu nyie Brela? Yaani Staff wa Brela wanafikiria wanajua sana kuliko hawa Entrepreneurs/Investors wenye ma-degree kibao, na wamejiajiri pia wakaajiri watu wengine kibao.

Brela badala ya kumwambia mtumiaji wa System kuwa unatakiwa kuwasilisha Nyaraka zifuatazo na ukaziorodhesha hapo chini zoote hata kama ni nyaraka 20 na ukamwambia mtu anatakiwa afanye kitu gani ? wewe unamwambia mtu aweke nyaraka moja kama vile amemaliza ? akiisha-upload hiyo nyaraka moja unamrudishia tena kuwa aweke tena nyaraka nyingine, kwa nini usimwambie aweke zote ? Ujinga sana baadae unamwambia aweke nyingine tena, na kila nyaraka inakaa huko kwenu zaidi ya wiki mbili ndio mnarudisha kwa mtumiaji... what the hell are you to consume investors working hours ??
Yule Mzee aliyepiga Kelele hapo Ofisini kwenu muoneeni huruma ametoka Mkoani kuja kushughulikia swala hilo tu baada ya kuona anacheleweshwa, mnajua ametumia pesa kiasi gani kwa kulala Hotelini, kuja na kushinda hapo kwenu kila siku, ameishakaa hapa Dar es Salaam zaidi ya mwezi mzima.

Sasa ndio nimeelewa kuwa kwanini wafanyabiashara wengi wanafunga Biashara wanakimbilia Rwanda na Zambia kumbe kisa ni Brela - JPM please pita pale Brela lile liwaziri uliloliweka na likurugenzi lake ni kazi Bure kabisa. Fukuza wote hapo hata hao wafanyakazi wa Brela rushwa tupu fukuza... vijana wako wengi wenye Degree na Masters za Business Administration huko mtaani watakushukuru sana ukiwaajiri.

Ushauri kwa Mkurugenzi wa Brela
1 - Toka hapo Ofisini kwako kila siku na uanze kuuliza wateja wako mmoja mmoja anahitaji nini utashangaa sana.
2 - Fungua Ofisi zote hapo/bomoa kabisa hayo ma-partition yenu, yanaficha walarushwa tu... hao Staff wako wakae na wateja uso kwa uso mezani,
akiinuka mteja mmoja anakaa mwingine anahudumiwa
sio wamejifungia wanakunywa chai masaa yote na kupiga umbea huko Ofisini
3 - Walipa kodi sio hao wahindi pekee mnaowaita Ofisini mnawahudumia alafu wa-Bongo mnawadharau... Hudumia watu wote sawa.
4 - Hakikisha unawapa malengo na namba hao Staff wako.... inaonekana Staff wanapiga stori na kula lunch tyuu jioni wanaondoka.

Ushauri kwa Waziri wa Viwanda na Biashara
1 - Tembelea Brela mara kwa mara... kwani ndio sehemu/kitovu kikuu chaa kazi zako, kagua kazi hadi za Junior Staff wa Brela na usiogope mtu
2 - Hakikisha unamuwekea Targets and Numbers huyo Mkurugenzi wa Brela hana mawazo ya kazi huyo anavyoonekana.
3 - Ongea na wafanyabiashara mara kwa mara watakueleza mengi sana.

Ushauri kwa Rais -JPM (The Field Marshall)
1 - Huku Mtaani kuna vijana wazuri sana kwenye kazi kama watu hawajui nini cha kufanya piga chini ajiri wataalaam walioko mtaani ni wazuri sana.
Hata wakurugenzi wapo pia Mtaani utawapata.
2 - Tuma timu yako ile ya kazi watakuthibitishia haya yaliyoandikwa hapa.

Naamini nimewakilisha vyema - Kuna watu najua wakiiona hii Taarifa watakuwa wamefarijika sana na wengine watakuwa wameumia hasa waliokuwa wameweka ndoano zao kunasa rushwa na kwa kuwa walizoea kuwaumiza wenzao

ANAYEJISIKIA KUTUKANA ATUKANE KWA RAHA ZAKE

Today the Volcano Temperature has decreased to 25,980 Degree Centigrade

1551808360273.png

Pole sana. Ni kweli serikali iangazie BRELA kwa ukaribu. Hiyo system yao ni kikwazo kikubwa sana kwa business. Wanasubiri mpaka Rais aje aseme? Rais ayafanya mambo mangapi? Na wao wanalipwa kwa kazi gani?

Uchumi wa viwanda tutaendelea kuusikia kwa wengine tu!
 
Mkuu ... Brela imekuwa kikwazo cha biashara badala ya kuwa mkombozi wa Biashara Tanzania, Nazijua Kampuni mbili zilikuwa zinataka kufungua sister company wakaambiwa hadi wamalize kuweka kumbukumbu zao sawa, lakini sasa hadi leo wameshindwa ni zaidi ya miezi tisa.
 
Pole sana. Ni kweli serikali iangazie BRELA kwa ukaribu. Hiyo system yao ni kikwazo kikubwa sana kwa business. Wanasubiri mpaka Rais aje aseme? Rais ayafanya mambo mangapi? Na wao wanalipwa kwa kazi gani?

Uchumi wa viwanda tutaendelea kuusikia kwa wengine tu!

Yaani Brela ni Tatizo kubwa sana.... Kinachokera sasa ni wale Staff kuwadharau wa-Tanzania na kuwajali sana wahindi, yaani nikero sana.
 
Ila tusiwalaumu sana BRELA kwasababu chanzo cha wao kufikia maamuzi ya kwenda Online kumetokana na move ya serikali ya awamu ya nne walikuja na kitu inaitwa Big Results Now/Matokeo Makubwa Sasa kitengo hiki kilikuwa pale ofisi ya Rais kwa lengo la kuhakikisha huduma zinazotolewa na serikali zinakwenda online ili kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi kuliko mtu kufunga safari kwaajili ya kufata huduma fulani katika ofisi za serikali.
Hiyo ndiyo mojawapo ya sababu ya BRELA kuja na mfumo wa Online Registration System kwaajili ya wateja na wadau wake; ninachoona aliye pewa kazi ya kutengeneza mfumo ndiyo kawatengenezea mfumo usio rafiki; lakini pia taasisi inaonyesha kuwa haikuwa imejiandaa kupokea huu mfumo na kuutendea haki, ninasema hivyo kwasababu huwezi ukataka kwenda online halafu mafaili yako kwenye papers katika shelves zilizoko masjala. Ilitakiwa documents zote ziwe kwenye mfumo halafu ndiyo uruhusu mfumo uanze kutumika kwa wateja kwa kuendelea pale alipokuwa ameishia mteja kwa mujibu wa faili liloko kwa msajili.
 
Mimi nilifanya name reservation, nimelipia 50k, (sipendi usumbufu wakati wa kujaza other forms kurudia rudia)

Nimemaliza kila kitu Memarts, form zote wanakuja kuniambia kuna company ina jina kama hilo kwahyo nitafute jina jingine, na hapo ni kama mwezi,

Wanakera, ikabidi nianze mchezo wa kubahatisha na ndo nasubiri hadi sasa.
 
Brela, NIDA, UDART/DART... Hizi ndizo taasisi za hovyo kabisa kuwahi kuwepo hapa tanzania kwa awamu hii.

Nashindwa kuelewa wanafanyaje kazi hizi taasisi..
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisaa, mm hivi sasa nina wiki ya 3 wananizungusha tu aisee. Yani inakatisha tamaa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkurugenzi pole sana kwa yanayokusibu na Brela.
Pale Brela nimepata taarifa kuwa ukiwa na laki mbili yaani unawapa tu namba ya Kampuni yako na Tracking number basi kila kitu wanakufanyia wenyewe..... sasa hii si uhujumu uchumi wa waziwazi kabisa alafu Magufuli anaamini kuwa ana watu wanafanya kazi pale. ndio maana kila siku wafanya Biashara wanailaumu serikali kumbe sababu kubwa ni Brela.
 
Ila tusiwalaumu sana BRELA kwasababu chanzo cha wao kufikia maamuzi ya kwenda Online kumetokana na move ya serikali ya awamu ya nne walikuja na kitu inaitwa Big Results Now/Matokeo Makubwa Sasa kitengo hiki kilikuwa pale ofisi ya Rais kwa lengo la kuhakikisha huduma zinazotolewa na serikali zinakwenda online ili kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi kuliko mtu kufunga safari kwaajili ya kufata huduma fulani katika ofisi za serikali.
Hiyo ndiyo mojawapo ya sababu ya BRELA kuja na mfumo wa Online Registration System kwaajili ya wateja na wadau wake; ninachoona aliye pewa kazi ya kutengeneza mfumo ndiyo kawatengenezea mfumo usio rafiki; lakini pia taasisi inaonyesha kuwa haikuwa imejiandaa kupokea huu mfumo na kuutendea haki, ninasema hivyo kwasababu huwezi ukataka kwenda online halafu mafaili yako kwenye papers katika shelves zilizoko masjala. Ilitakiwa documents zote ziwe kwenye mfumo halafu ndiyo uruhusu mfumo uanze kutumika kwa wateja kwa kuendelea pale alipokuwa ameishia mteja kwa mujibu wa faili liloko kwa msajili.

Kiongozi Uko sahihi kabisa lakini mimi sioni kama kuna tatizo lolote kwenda On-Line kama unawasomi wazuri ni suala rahisi sana.

Kwanza ni kuwa utakuwa umerahisisha kazi. Kama kuhamisha kumbukumbu za Clients kutoka kwenye Manual Documents Files ni watumiaji ndio wana-create their own accounts and upload their own records kwa hiyo haiwahitaji wao kuhangaika kuhamisha data kutoka kwenye mafaili.

Pili ni kuwa System yenyewe iko vizuri mmno ukiingia hadi unafurahia kuitumia.... sasa kitu ambacho mtumiaji yeyote wa System amekigundua ni kuwa, hakuna namna ya Staff wa Brela kukutana na Clients kwa hiyo Rushwa inakuwa haipo (Minimum Human Intervention - no Bribe) ndio maana wale Staff wa Brela wanaweka vikwazo vikwazo, mara wazuie kazi yako, mara System inaharibiwa makusudi ili waweze kukutana na wewe mtumiaji alafu uwape laki mbili kesho yake umehudumiwa Tayari.
 
Mimi nilifanya name reservation, nimelipia 50k, (sipendi usumbufu wakati wa kujaza other forms kurudia rudia)

Nimemaliza kila kitu Memarts, form zote wanakuja kuniambia kuna company ina jina kama hilo kwahyo nitafute jina jingine, na hapo ni kama mwezi,

Wanakera, ikabidi nianze mchezo wa kubahatisha na ndo nasubiri hadi sasa.

Pole sana Mkuu.... Sasa ukute walikuwa wanasubiri wewe ujiongeze na kuwaambia una shilingi ngapi ? ili wakuhudumie fasta walipoona unakomaa mwenyewe wakasema ngoja tumuache akipoteza pesa nyingi ndio hapo tumrudishe mwanzo aanze moja.
Pole sana Mkuu. sasa hawa dawa yao hii thread iende viral kwenye mitandao ya kijamii ndio wataelewa wakuu wao kuwa kuna jambo la kulifanyia kazi hapo.
 
Brela, NIDA, UDART/DART... Hizi ndizo taasisi za hovyo kabisa kuwahi kuwepo hapa tanzania kwa awamu hii.

Nashindwa kuelewa wanafanyaje kazi hizi taasisi..

Kaka....Hahahahaaaaa, kiukweli ni Tatizo kubwa sana, BRELA, NIDA, UDART/DART, SUMATRA/LATRA nahisi wanaona kama zile Taasisi ni za kwao wao Bianfsi... Serikali kama haioni hili basi kuna Watendaji wanabenefit na kwa hali hii basi waziri husika anahusika moja kwa moja. JPM inambidi aingilie kati.
 
Tiss ingieni mzigoni ...muwezesheni raisi kufanya kazi yake kwa urahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app

TISS waingie Kaka..... Tena pale Brela unafikiria watachukua Muda kujua kama kuna Matatizo ?? ni kitendo cha kwenda na kukaa pale dakika kumi basi wataoondoka na report nzuri kabisa, iliyosheheni picha halisi ya Brela.
Naamini siku hata Waziri Mkuu akitembelea pale basi tutashuhudia watu wakitimuliwa kazi.

Tena inapendeza sasa tuwaweke hadharani kwenye mitandao ili waziri awajibishwe fasta.
 
Shukurani kwa mjadala

Cha Kwanza ni kumtimua CEO na Management nzima na kutangaza upya nafasi hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukurani kwa mjadala

Cha Kwanza ni kumtimua CEO na Management nzima na kutangaza upya nafasi hizo

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu... Hili wazo lako ndio la msingi kabisa, maana Brela imekuwa kama mali yao wanafanya wanavyotaka wao.
Wametugeuza wa-Tanzania wote wajinga.... alafu nimeishapata majina ya wahusika wakuu wa Rushwa pale Brela.
Soon we are going to expose them here.
 
hakuna mtu mwenye email ya ikulu au ya waziri wa viwanda hapa tufanye kitu wazee au namba tu inatosha
 
Back
Top Bottom