BRELA system yenu ni kuharibu kazi au mmetega rushwa?

Brela wanavisingizio vingi mno, mara TRA mtandao uko chini unajiuliza walikabidhiwa dhamana wakwenda ofisini kufanya nini? Hawapo kikazi wapo kusubiri mshahara tu
 
Shida kubwa ya BRELA mishahara yao inatoka kwenye bajeti kuu na si mapato wanayoingiza wao; ili hawa BRELA wajitambue, wasipelekewe hela za kuendesha ofisi na mishahara badala yake watumie pesa zitokanazo na shughuli za BRELA. Miaka yote kabla ya ORS kampuni zilikuwa zinapeleka ritani na zinapokelewa na kulipiwa sasa iweje kuziingiza kwenye ORS zionekane zina shida?

Mimi naamini huu mfumo haujapokelewa "positively" na hao maofisa wa BRELA; matamanio yao ni mtindo wa zamani uendelee ili wapate kitu toka kwa wateja badala ya hizi huduma za ONLINE ambazo hawamwoni mwombaji
 
Hawa watu siwataki hata kuwasikia. Wamenivuruga sana.....
Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kiukweli umesema vyema kabisa... Mkuu hii System ya ORS inaonekana imepokelewa vibaya na watu wa BRELA, inaelekea inaenda kuondoa ubabaishaji wao ndio maana wanaipokea NEGATIVELY.
Return zimekuwa shida sana.... kulipia inachukua hadi mwaka mzima ... kweli Tanzania Shamba la Bibi.
 
Brela wanavisingizio vingi mno, mara TRA mtandao uko chini unajiuliza walikabidhiwa dhamana wakwenda ofisini kufanya nini? Hawapo kikazi wapo kusubiri mshahara tu


Mkuu... hawa BRELA sasa hivi wanafikiria wa-Tanzania wote hawajasoma ndio maana wanatutenda watakavyo wenyewe.
Akienda Muhindi pale utashangaa attention wanayompa utafikiria ni Malaika sasa nenda wewe mwenzangu na mimi wanakupita kama hawakuoni.
 
Hi i kitu inaitwa BRELA achana nayo kabisa
Nimefanya updates za kampuni ya mteja ni mwaka sasa hakuna kilichofanyika
Kila siku wanakurudishia Docs zako wanakuambia rekebisha hili au tuma hiki na hiki
Ukituma wanakaa wiki mbili kukujibu tena kuna hiki umesahau tunaomba ututumie au doc uliyotuma haikubaliani na system yetu au ni kubwa sana jaribu kufanya hiki na hiki
Mwaka mzima updates ya kampuni haijakamilika na mteja alitaka kusajili another sister company.
 


Tena Mkuu.... hawa BRELA wanafaa wapewe Performance Appraisal kwa sababu wnafanya kazi kana kwamba ile ni Kampuni yao Binafsi........ haiwezekani kwamba System iwe shida kuliko Manual Procedures.
 


Mkuu ... unachosema ni kweli 100% ukianza kusajiri au ku-update Kampuni wanakusumbua sana, Document moja unaweza ambiwa uirudie kuijaza hata mara saba, na baadae chukua ile waliyoisema uliiyokosea ya kwanza kabisa utashangaa wanaikubali, sasa hapo ndio utangundua kuwa hawajui wanafanya nini hapo BRELA... sasa nilichikisikia na nikaenda kukithibitisha BRELA ni kwamba... ukienda ukawaona wale maofisa ukawaambia utawapa kitu kidogo, nayo wamepanga bila ya laki mbili hawakusaidii, ukiwapa laki mbili fasta hata kama documents zinamakosa tayari wanakimbiza na kukamilisha wenyewe bila hata uwepo wako wewe.
 
Brela, NIDA, UDART/DART... Hizi ndizo taasisi za hovyo kabisa kuwahi kuwepo hapa tanzania kwa awamu hii.

Nashindwa kuelewa wanafanyaje kazi hizi taasisi..
Yaani ni balaa BRELA Ndio inafuata kwa rushwa sasahivi baada ya Traffic yaani mtu unaambiwa kusajiri kampuni awe na kitambulisho cha nida ukienda nida anaambiwa Cheti chake cha kuzaliwa lazima ki updatiwe Rita Ukienda RITA unaambiwa nenda mkoa uliko zaliwa uanzie kwa mwenyekiti wa mtaa..


Maana kuna vyeti havitambuliki wakati vilisainiwa na maafisa wa RITA.....

Imagine mtu yupo Songwe anataka kufungua kampuni na kwao ni kigoma inakuwaje hapo si mtaji unaishia kwenye nauli upuuzi wa nchi hii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mkuu ni balaa
Unaweza rudia the same docs hata mara kumi
Na tatizo hawakupi jibu kwa muda unaotaka ni mpaka wakae nazo hata wiki mbili au hata mwezi ndo wanakujibu ile doc uliyotuma ina makosa tafadhali rekebisha hiki na hiki
Na tatizo sasa docs zote wanazo badala wangeziweka kwenye system ili zile ambazo hawana wakuambie ujaze au uwatumie unaanza kujaza kuanzia Memart mpaka Annua Returns za miaka ya nyuma au changes zozote za kampuni ambazo tayari ulishapeleka kwao
System ina matatizo kibao na kuna sehem eti ukikosea mpaka IT wao atoke sijui Netherlands kuja kurekebisha au kufuta
 
Apart from Brela, naomba kujua ni taasisi gani ya serikali inayo fanya kazi vizuri? I mean wafanyakazi wapo committed, wanajali muda wa mteja nk
 


Mkuu.... wale BRELA wanatumia ujanja tuu, haiwezekani mtu wa System yaani IT atoke Netherland, wanakwambia hivyo ili ujiongeze tuu. Sasa Kama hadi atoke Netherland kwanini wao wanakitengo cha IT pale kwao, je huyo mtu atatoka Netherland mara ngapi kwa siku maana watumiaji wa mtandao wako wengi na wengi wanapata matatizo aina mbalimbali kwenye Mfuno huo wa BRELA.

Pole sana Kiongozi... lakini mimi nasema muda ni sasa, tufanye kitu watolewe hapo walipo na waajiriwe watu wengine kabisa.
 

Kabisa mkuu
Niliuliza hao IT wao wanafanya nini kama tatizo dogo tuu la kufuta account iliyokosewa mpata IT atoke nje
Na kuna mmoja aliniambia kuwa yeye baada ya kupata shida kama hiyo walimwambia awasilishe docs manual wakamsaidia maana client wake alikuwa anaomba working permit na muda wake ulishaisha
Walimfanyia kwa kuwa aliwafaham na ikawa pona yake
Ila kwa ssis sasa imekuwa hadithi toka May mwaka jana mpaka leo hakuna updates yoyote iliyomalizika
 

Mkuu.... Huyo jamaa waliomwambia awasilishe document ukute aliwaachia pesa, wale hawafanyi kazi bure hata kama wanakujua, Sijui kwanini Rais John Pombe Joseph Magufuli hajapata hii taarifa wakati kila siku watu wanawalalamikia. au wasaidizi wa Magufuli nao pia ni wazembe pia ?
 


Kiongozi kwenye hizi Taasis... Naona kama bado kabisa hatujafikia hatua ya kujivunia kuwa kuna Taasis inafanya kazi vizuri, wafanyakazi wamekuwa kama majambazi yanayopora haki zetu, Ukienda SUMATRA Shida, Ukienda TANESCO Shida, Ukienda TRA Shida, Ukienda NIDA Shida.... alafu tunaendelea kuwakumbatia wafanyakazi ambao wametawaliwa na Rushwa wakati kuna vijana wako mtaani wanaelimu nzuri na maadili mazuri kabisa, Vijana wana Degree zenye GPA nzuri za 4.5, 4.0, 3.8 nk wanasaka ajira hatuwapi tumekumbatia mafisadi kwenye Taasis zetu. Rais John Pombe Joseph Magufuli tafadhali liangalie hili naona huku kwenye Taasis zetu anataka kukuangusha kwa nguvu zote kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…