Mimi ninachokifahamu ni kwamba Tanzania gari yenye 2500CC na kuendelea ina resale value ndogo sana..pia watu wengi wanapenda kuweka mafuta ya 10,000-15,000 na wanataka wazunguke misele mingi huku kiyoyozi kipo na ukiangalia vizuri brevis inatumia kuanzia 5km/l - 6km/l sasa kwa mtu anayetaka kuweka mafuta ya 10,000-15,000 lazima alalamike gari za CC kubwa.
hivyo uunatakiwa walau uwe na uwezo wa kuweka 50,000-80,000 kwa siku 4-7 sasa kibongo bongo watu wenye uwezo huo ni wachahce sana ndo maana hadi leo hii Premio, IST resale value yake bado ipo juu Crown zenyewe watu hawakai nazo sababu ya gharama za uendeshaji