Brevis Bei nafuu. WHY?

Brevis Bei nafuu. WHY?

Mkuu nataka nijiripue kununu Brevis used, Hebu nipe Wastani wa matumizi wa mafuta kwa kilometer. ( Nipo huku mikoani hakuna foleni ), kuna jamaa anasema 6Km/l ? real
 
Mi haya matatizo sijawahi kuexperience na ni mmoja wa watu ambao ukiniambia ninunue sedan comfortable ya bei nzuri leo ntaifikiria. Gari ni namba DCS na ilinunuliwa na km zaidi ya laki. Na imepiga mzigo hapa dar on daily basis na safari kadhaa including nyingi za dar-moro na 1 Dar - Arusha nikiendesha mwenyewe.

Kiufupi kama kweli hizi gari zina shida kiasi hiki basi mi ntakuwa nina bahati nayo. Engine haijawahi kuguswa labda umeme kuna kitu ilisumbua ila sikumbuki ni nini na halikuwa issue kubwa. Maintenance nyingine zilikuwa za kawaida kama za gari nyingine.
ulaji wanmafuta kwa wastani upoje?.
 
Mimi ninachokifahamu ni kwamba Tanzania gari yenye 2500CC na kuendelea ina resale value ndogo sana..pia watu wengi wanapenda kuweka mafuta ya 10,000-15,000 na wanataka wazunguke misele mingi huku kiyoyozi kipo na ukiangalia vizuri brevis inatumia kuanzia 5km/l - 6km/l sasa kwa mtu anayetaka kuweka mafuta ya 10,000-15,000 lazima alalamike gari za CC kubwa.

hivyo uunatakiwa walau uwe na uwezo wa kuweka 50,000-80,000 kwa siku 4-7 sasa kibongo bongo watu wenye uwezo huo ni wachahce sana ndo maana hadi leo hii Premio, IST resale value yake bado ipo juu Crown zenyewe watu hawakai nazo sababu ya gharama za uendeshaji
50,000/= per week mbona hela ya mkeka mmoja tu hapo WA siku moja!... hahaha
 
Ushauri maana usinunue gari inayouzwa na mtu mweusi agiza moja kwa moja anapouza jua ina tatizo au kuna tatizo linakuja kutokea
Ww hilo la kwako uliloagiza utakapolichoka utamuuzia nani kama watu wote watafanana na wewe mtazamo? Au Uta export na wewe?
Ndo maana unauziwa bei rahisi ukatengeneze.

Kila circle ya hii dunia lazima iheshimiwe, anayenunua 0km lazima amuheshimu anayenunua mkweche sababu anayenunua mkweche ndo alimpatia pesa aliyenunua used from Japan lililouzwa na aliyenunua 0km.
 
Isiibiwe kwa sababu Ni nzito au?
Haiwezekani brevis zote ziwe za wizi maana karibu zote zinauzwa cheap. Huwezi iba gari ukalitangaza kama lilivyo. Ukibadili namba itakulazimu kubadili kadi, mnunuzi ahakiki kadi tu TRA na polisi kujiridhisha. Kuna sababu nyingine zinazosababisha bei kuwa chini.
 
Back
Top Bottom