Crown ghafla limekua Yebo Yebo.
Kweli mkuu...ila sabau kubwa nadhani ni vile Watz tunapenda mambo ya fashion.
Magari mengi ni fashion ikishapita inakuwa yeboyebo.
1. Nianze na GX 100 chaser, mark ii na cresta.
2.Tukaja GX 110
3.Verosa haikufanya vizuri saana
4.Brevis nayo ilivamiwa sasa hivi watu wanaikimbia kama ukoma
5.Mark x hapo napo watu kibao walikimbilia ila bado inafanya vizuri.
6.Crown ndiyo kila mtu anakimbilia hapo na wanazi company kwa kufuga ndevu...yaani sasa hivi ujanja ni kufuga ndevu nyingi kisha ukae ndani ya crown.
7.Tako la nyani lilikimbiliwa saaana lakini sasa hivi naona wanaume wengi wameamua kuziacha kwa wadada...wadada wanapendeza sana wakikaa humo.
8.IST hapa ndiyo balaa...hii imekuwa kama sare sare za vijana wa kiume na wakike wanaochipukia maisha....Kuigana nadhani ndiyo sababu kubwa...
Kwa upande wa Subaru naona
1.Impreza kama vile imevamiwa na watu wanaichukulia kama mvadala wa ist.
2.Foresteranazenyewe zimeendeshwa sana hasa lile toleo la kati....sasa hivi wameachiliwa madogo wanaonyoa viduku ndiyo wanakaa sana humo.
Kwa hiyo kibongo bongo kumiliki gari inakuwa kama ni fashion flani hivi..
Ila sasa hivi naona kufuga ndevu ndiyo kunatawala